Nilienda kumwona jamaa yangu aliyelazwa hospitalini hapo. Katika saa nzima niliyokuwamo wodini mle, nilijifunza mengi.
Niliona, kuwa manesi wengi , tofauti na zamani, hawan a ari ya kazi. Kuna wanaokwenda kuombwa ili watoe huduma.
Wagonjwa wengi wanaandikiwa dawa, lakini, tofauti na zamani, kwamba nesi alikwenda kumchukulia mgonjwa dawa, au ndugu walikwenda dirisha la madawa hospitalini kuchukua dawa bure, siku hizi karibu kila dawa mgonjwa anatakiwa akainunue kwenye duka la madawa.
Hivyo, kuna wanyonge wasio na pesa wenye kupoteza maisha mahospitalini kwa kukosa shilingi elfu kumi ya kununulia dawa. Mfumo wa Huduma za Afya Bure unakosa maana.
Nakumbuka, miaka ile ya 70 wakati tukikua, Huduma Bure za Afya kwa jamii ilikuwa na maana hiyo. Nakumbuka pale Zahanati ya Amana, Ilala mgonjwa alikuwa akiandikishwa mpaka jina la mtaa na namba ya nyumba, kwamba kama mgonjwa hajamalizia sindano zake , basi, manesi walifika mpaka nyumbani kwa mgonjwa kumfuatilia.
Nakumbuka wazee wenye kisukari walifuatwa majumbani na manesi ili wadungwe sindano zao. Akina mama wajawazito walifuatwa majumbani mwao na gari la wagonjwa ili wawahishwe Ocean Road.
Kuna waliorudishwa majumbani kwao pia kwa gharama za Serikali, walipa kodi.
Hata kama wakati umebadilika, bado naamini, sera za Kijamaa, zenye kuhakikisha kuwa rasilimali za nchi zinagawanywa kwa kuwajali zaidi walio wengi na hususan zenye kuhakikisha kodi inakatwa kwa wenye nacho ili kuwasaidia wasio nacho, inaweza kuwasaidia wanyonge wengi watoke kwenye unyonge walio nao.
Maana, ukweli unabaki, kuwa wengi kama mimi, tusingefika hapa tulipo kama si kwa Sera za Kijamaa, ambazo Mwalimu aliziamini na kuzisimamia hadi kufa kwake.
Wikiendi Njema.
Maggid Mjengwa,
Iringa.

No comments:
Post a Comment