Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal, amesema watuhumiwa walioficha fedha nje kinyume cha sheria watachukuliwa hatua bila kujali nafasi wala nyadhifa zao na kwamba suala hilo litawekwa wazi.
Kadhalika amejitetea kuwa yeye si mmoja wa viongozi walioficha fedha ng’ambo.
Dk. Bilal alilazimika kusema hayo, kufuatia swali lililoulizwa na mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), katika Mhadhara wa 13 wa Kumbukumbu ya Waziri Mkuu wa zamani, hayati Edward Moringe Sokoine uliofanyika katika kampasi ya Solomoni Mahlangu mjini hapa.
Katika swali lake mwanachuo John Robart alitaka kujua ni hatua gani serikali imewachukulia viongozi waliotajwa kuficha fedha nje ikiwa ni sehemu ya kumuenzi hayati Sokoine.
Alisema Sokoine alikuwa mwadilifu na aliyekemea rushwa katika ngazi zote ili kuleta usawa baina ya maskini na matajiri.
Akijibu swali hilo, Dk. Bilal alisema pamoja na kwamba yeye si miongoni mwa walioficha fedha nje, lakini kama wapo Watanzania na wakithibitika kuwa wameficha fedha kwenye benki za ng’ambo sheria na taratibu zitaongoza jinsi ya kuwashughulikia.
Alisema iwapo taarifa sahihi za watu hao walioficha fedha nje zitapatikana ,serikali itawachukulia hatua bila kujali nafasi zao na kwamba suala hilo litawekwa wazi bila kificho.
Watanzania zaidi ya 300 wanadaiwa kuficha mabilioni ya Dola za Marekani katika benki za kigeni ikiwemo Benki ya Uswisi ambapo hivi karibuni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Zitto Kabwe, aliwasilisha hoja binafsi bungeni kutaka uchunguzi wa kina ufanyike na wahusika washughulikiwe kisheria.
Taarifa hizo alizozitoa zilihusisha madai kuwa baadhi ya Watanzania wameficha Dola milioni 300 kwenye benki za Uswisi ikiwa ni rushwa walizopewa kwenye miradi ya utafiti wa gesi na mafuta inayofanywa na makampuni ya kigeni.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment