Mohamed Seif Khatib
Dr Hussein Mwinyi
Shamsi Vuai Nahodha.
Omar Yussuf Mze
Samia Suluhu Hassan
Profesa Makame Mbarawa
---
MATOKEO ya uchaguzi wa wajumbe wa NEC katika kura zilizopigwa juzi mjini Dodoma katika mkutano wa nane wa Chama cha Mapinduzi (CCM) yamevuja.
Huku Mwenyekiti wa chama hicho kinachoiongoza Serikali, Rais Jakaya Kikwete akitangaza jana kuwa matokeo hayo yatatangazwa leo pamoja na matokeo ya nafasi za Makamu Mwenyekiti lakini tayari hadi jana mchana zaidi ya asiliamia 90 ya wajumbe walisha jua matokeo hayo na kuanza kupongezana huku yale ya wagombea wa bara yakiwekwa na idadi ya kura zao.
Ingawa baadhi ya wajumbe wameoneshwa kushangazwa na idadi ya kura alizopata Katibu Mkuu wa Chama hicho Wilson Mukama kwa kushika nafasi ya 9 huku Steven Wasira akiwaongoza.
Wanaodaiwa kushinda nafasi 10 Zanzibar:
Mbunge wa Uzini, Mohamed Seif Khatib; Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Ali Mwinyi, Waziri wa Fedha Zanzibar, Omar Yussuf Mzee, Abdulhakim Chasama na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Shamsi Vuai Nahodha.Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Khadija Hassan Aboud, Bhaguanji Mansuria, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa na Khamis Mbeto
No comments:
Post a Comment