WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, November 19, 2012

Picha Nyingine Unapiga, Na Unabaki Na Huzuni...!




 Ndugu zangu,

Hutokea ninaporudi nyumbani kutoka ziara ya vijijini nikazama kwenye fikra. 
Hakika, ninapotembea huko vijijini hutokea nikaiona picha ya kupiga. Lakini, niwe mkweli, picha nyingine ninazopig a huniacha na huzuni kubwa.

 Hapo juu ni mfano wa picha hiyo; hapo ni Pawaga, Iringa. Nilimwona mtoto huyo kulia akilazimika kuvua kiatu chake kilichoachana na soli. Ni kiatu cha zamani na bila shaka ametembea nacho kilomita nyingi sana. Na kwa vile ardhi anayokanyaga ni ya moto kutokana na jua kali, basi, kwa mtoto huyo ni heri atembee na kiatu cha mguu mmoja. Ukiwa kwenye eneo hilo la tukio unamwelewa kabisa. 

Naam, katika yote tuyafanyayo, tusisahau kuwa kuna Watanzania wengi wenye kuishi katika mazingira haya. Na maana ya nchi kuwa huru ni pamoja na kuhakikisha kuwa watu wetu wanapata nafuu ya hali zao za maisha, ni jukumu letu. 
Maggid, 
Iringa.

No comments:

Post a Comment