Ray Kigosi aliwahi sema kuwa , “Ukweli si kama
tunapenda kuuza haki zetu kwa wasambazaji au wanaonunua filamu, sababu kubwa ni
ukosefu wa soko la uhakika pamoja na wawekezaji kushindwa kujitokeza”. Hii
ni sababu ambayo inaonyesha ukosefu wa sera nzuri za kulinda hakimiliki za
wasanii wetu ni jukumu la serikali yetu.
Ray Kigosi “lakini tuwe wakweli na kukumbuka
tulikotoka tulikuwa tunaigiza katika Televisheni kwa kulipwa 40,000/ tu kundi
la wasanii kibao, lakini leo hii tunamiliki kampuni na kumudu maisha yetu kwa
kununua magari na vitu vingine,” tatizo hapa ni wasanii wetu wanaangalia
na kufikiria zaidi faida ya muda mfupi elimu inahitajika hapa.
Swali la msingi hapa Je ni jukumu la serikali kuandaa mazingira yatayoweza kumsaidia
mmiliki kuweza kuzimiliki na kumpa mwenye hakimiliki haki zote katika
matumizi ya kazi yake au ni jukumu na mhusika mwenyewe kwanza kujiandalia
mazingira ya umiliki yeye mweyewe.
Je
sheria ya Tanzania inampa nani nguvu ya
hakimiliki? Je hakuna utaratibu ambao katika mazingira yeyote yale
yakamsaidia mtunzi kuwa na hisa nyingi katika kazi yake na sio kuishia
kuwa mwajiriwa, na kuishia tu kupewa
kiasi Fulani cha pesa mara moja?
Je hakimiliki ni mnyama gani huyu?
katika kifungu na 9(1) cha Sheria ya
Hakimiliki na Hakishiriki ya 1999.
Kifungu hiki cha sheria kinaonyesha
haki ambazo wasanii wakizielewa zitawasaidia katika kulinda haki zao kwa faida
yao na familia zao nazo ni:
Haki hizi ndio
msaafu wa kazi za wasanii, wanatakiwa kuuelewa ni ili waweze kuuelewa vizuri ni
ukweli ambao haupingiki kuwa wasanii wetu wanahitaji ufahamu na uelewa amba ni
rahisi kupatikana kupitia elimu.
Kama Pastor Emmanuel Myamba katika moja
ya Kongamano; alivyoshauri kuwa, wao kama wasanii wanahitaji elimu ili iweze kuwasaidia katika
kufaya kazi bora na elimu hiyo itawasaidia wao kujua haki za kazi zao.
Je wasanii wetu wakiangalia hiyo sheria
ya hakimili wanahaki ngapi? msambazaji anahaki ngapi?
Elimu itawasidia wasanii wetu kuwapa
uwezo wa kupapmabua na kujiamini katika maamuzi na umiliki wa kazi zao. Lakini
inapotokea msanii anauza haki zote
ategemee nini katika maisha yake kama sio umasikini? Ukifanya kosa hili kubwa
la kuuza haki zote basi ujue wewe kuwa umempa nguvu msambazaji
KWA NINI WASANII WANASHAUSHIKA KUZA HAKI ZAO?
Je ni kwa sababu ya umasikini?
Je ni kwa sababu ya Tamaa ya
maendeleo ya haraka haraka?
Je kwa sababu ya kushindwa
kuzielewa haki zao?
Je ni kwa sababu ya ushindani
miongoni mwao?
Je au ni kwa sababu ya uduni wa
kazi zao?
Pengine kwa wakati huu sikubaliani sana
na Msanii Vincent Kigosi ‘Ray the greatest’ ambaye aliwahi sema kuwa ni kweli
wasanii wanauza haki zao za filamu wanazotengeneza kwa wasambazaji kutokana na
hali halisi ya soko lenyewe kuwa finyu likimilikiwa na kampuni moja tu,
ambayo angalau imewatoa hapo walipo tofauti na siku za nyuma walivyoanza
kuigiza katika televisheni.
Nafikiri tatizo kubwa la wasanii wetu ni
Elimu ya uelewa, kujua sheria za kuwalinda kazi zao, na mbaya zaidi wasanii
wanatakiwa wapunguze kuridhika haraka na kuona kuwa soluhisho la tatizo la soko
na umasikini ambao unawazunguka ni kuuza haki zao zote kwa kipande cha muhogo
kumbe na baadae wanakumbuka kuwa kumbe walifanya kosa wakati wanakuwa
wameshachelewa kabisa.
Ikumbukwe kuwa watafiti wengi wa habari
za wasanii kama Bishop Hiluka wanasema kuwa sekta ya filamu ni sekta
iliyosheheni utajiri mkubwa lakini cha kushangaza ni pale ambapo wadau wake
wanaongoza kwa kuwa, na hasa pale ambapo kwa bahati mbaya wanatangulia mbele ya
haki warithi wao wanakuwa hawana chochote cha kiuchumi.
Swali hapa ni nini chanzo cha hali hii? Hapa tunapata mitazamo
tofauti pengine kutokupewa kipaumbele amabcho kinalenga sheria nzuri za
kuwalinda wasanii wetu hasa katika kumiliki kazi zao kwa faida yao wenyewe.
Nje ya sababu zote za kisheria na sera
mbovu za serikali kuhusu kazi za wasanii; mimi naona vile vile kunatatizo kubwa
sana linalotokana na dhana ya kutojiamini na kuridhika upesi kwa wasanii
wenyewe na kukosa sauti ya kushikilia kazi zao na hivyo kumpa sauti na nguvu
zaidi msambazaji ambaye kwa upande wake yeye anakuwa na pesa za kununua kazi
hiyo na kushikilia hakimiliki na kuwaacha wasanii wetu wakiendelea kushikilia
kuti kavu la maisha yao.
Katika kuhakikisha kuwa kilio cha
wasanii kinafikia mwisho na kuwawezesha kufaidi zaidi kazi zao na faida
itokanayo na kazi zao. Serikali imeazimia kuifanyia marekebisho sheria ya Ushuru wa Bidhaa, Sura 147, huku
akitambua kuwepo kwa kilio cha muda mrefu cha wasanii kurudufiwa kazi zao za
sanaa na kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya., Serikali kupitia Mamlaka ya
Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya
kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya
kurudufu kazi za sanaa hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa
nchini.Tumebakiwa na kipindi kifupi tu
kwa Mamlaka ya Mapato kuanza kuweka stampu kwenye bidhaa hizo ili uuzaji
wa kazi hizo uwe rasmi na kuwawezesha wasanii kupata kipato stahili kutokana na
kazi zao, uwekaji huo wa stampu utaanza kuanzaia tarehe 1 Januari, 2013.
Pamoja na nia nzuri ya serika bado
tunaendelea kuwahimiza wasanii kuwa, marekebisho ya sheria pekee hayatoshi
lakini wasanii wanahitaji zaidi vilevile elimu itakayo wasaidia kujiamini na
kuthubutu katika kazi zao, pamoja na nchi yetu kukosa kabisa mfumo mzuri ambao
ungesaidia kumuendeleza msanii wa Tanzania na hatuna vyuo vinavyotoa mafunzo
yanayojikita kwenye filamu tu kama ilivyo kwa jirani zetu.
KIFO CHA KANUMBA KIMETUFUNDISHA NINI KUHUSIANA NA HAKIMILIKI?
Kama kweli kama waandishi na
wadadisi wa mambo walivyowahi kuongea kuwa pamoja na sekta ya filamu kuwa na
nguvu na mvuto ndani ya jamii, lakini wahusika wake wamendelea kutofaidika sana
na kazi zao; mfano ambao wengi wanautoa ni ule wa Marehemu Steven Kanumba hasa
pale wanapouliza
Kanumba baada ya kufa amefaidika
vipi? Taathimini ya uchambuzi wa namna kanumba pengine alivyokuwa maarufu
lakini wakati wa kifo chake mengi yalijitokeza hata kamati ya mazishi ambayo
ilikuwa na wajumbe wake wengi wasanii wenzake waliwahi sema kuwa, imedai kanumba
amefariki dunia akiwa maskini, kinyume kabisa cha umaarufu mkubwa aliokuwa nao
wakati wa uhai wake. Kanumba alishiriki kwenye filamu zaidi ya 40 lakini
amekufa maskini.
Tatizo ni nini hasa? Jibu ni haki za wasanii na watayarishaji wa filamu
zitaendelea kuporwa, kwa kutumia unyonge wao na umasikini wao wataendelea
kutumika kwa maslahi ya wachache, na mwishowe watakufa wakiwa masikini lakini
wenye majina makubwa, tena bila hata kuwaachia wategemezi wao urithi
unaoeleweka. Mwandishi mmoja aliwahi sema “kuwa Kama mwandishi mmoja alivyowahi
sema kuwa;”Kwa wenzetu pesa inatengenezwa hata pale mtu anapokuwa amefariki
dunia, hii ni kutokana na nchi hizo kuwa na sheria nzuri za hakimiliki,
serikali kuwasimamia watu wake na viongozi kutimiza wajibu wao ipasavyo. msanii
anaeendelea kutengeneza fedha nyingi japo amefariki miaka
mingi sana iliyopita”.
Nakubaliana na falfasa hii kuwa “Kwa
mtu aliyefanya kazi nzuri, kufariki siyo mwisho. Anaweza kuendelea kuishi hata
baada ya kifo, kwani kazi zake, pamoja na nembo zake zinaweza kuendelea kuvuna
mashabiki ambao wanamkumbuka, na wale waliozaliwa muda mrefu baada ya kufa, na
kuingiza mapesa kibao kama inavyotokea kwa mastaa niliowataja hapo
juu”
Tatizo la ukosemu wa elimu na umakini
ndio umemfanya Marehemu Kanumba na wengine waliotangulia mbele ya haki kuwa
jasho lao kuendelea kufaidisha watu wachache kosa liko wapi?
Hebu tumtathimini maisha msanii maarufu, Kanumba alikuwa mmoja wa wale ambao walikuwa wanaojiona washindi
kwa kuingia mikataba inayowafanya kuuza haki zao kwa msambazaji na kuishia
kupewa gari na pesa zinazowasaidia kwa miezi michache, masikini hakujua kabisa
kuwa atakapoaga dunia haki yake itakuwa imeishia hapohapo, na hawa waliobaki
wanapaswa kujifunza kupitia yeye kwani siku 'wakichuja' na thamani yao kupungua
watarudi kwenye msoto kwani haki zao tayari zitakuwa zimeshapotea.
Baraza la sanaa Tanzania Basata
liendelee kuwaelimisha wasanii kuhusu nini maana ya haki miliki; kama
ilivyojadiliwa na waandisha kadhaa wa habari za sanaa na sheria za haki miliki
kuwa, Sheria ya Hakimiliki ya nchi yetu inasema wazi kuwa hakimiliki hudumu kwa
mwenye haki kwa maisha yake yote na miaka hamsini baada ya kifo chake. Kwa
nchi kama Marekani wameongeza hadi miaka sabini. Ndiyo maana utaona
kuwa kuna kazi nyingi ambazo zinaendelea kuwa maarufu miaka mingi baada ya
wenye kazi kufariki, huku zikiwanufaisha warithi wao.
Hebu tumsikilize Issa Mussa Claude anahoja nzito kama wasanii wameisikia itawasaidia sana kuamka mara moja, wakumbuke kuwa wakati ni ukuta wasanii wanatakiwa kubadilika ili waweze kufurahia vipaji vyao na faida inayotokana na kazi zao
na sio kuendelea kumtajirisha mtu mwingine kwa jasho lao linalopatikana kwa kazi ngumu ya kufikiri na
kutenda
wasanii wakifanikiwa kuyasimamia haya sanaa itakuwa ndio gurudumu nzuri kwa maendeleo yao na familia zao na fani ya sanaa haitaendelea kuwa ni fani ya kuganga njaa tena.
No comments:
Post a Comment