MADIWANI wa Chadema waliogoma kumtambua Meya wa Arusha, Gaudence Lyimo sasa wanadaiwa kuanza kumtambua kupitia ‘mlango wa nyuma’.Tangu ufanyike uchaguzi wa meya, kuliibuka mvutano wa kisiasa uliosababisha Chadema kutangaza kutomtambua meya huyo.
Akizungumzia gharama za uzinduzi wa jiji juzi, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, Omari Mkombole alisema madiwani wa vyama vyote walishiriki vikao muhimu vya kufanikisha sherehe hizo.
Itakumbukwa msimamo wa madiwani wa Chadema ni kutomtambua meya huyo, huku wakisusia vikao kama ishara ya kuonyesha msimamo wao.
Tayari, baadhi ya makada wa Chadema mjini hapa walitoa msimamo wao kwa nyakati tofauti wakihojiwa kuhusiana na hali hiyo, huku wakilaani kitendo hicho na kwamba kitendo hicho ni unafiki mkubwa.
“Taarifa zilizonukuliwa nje kama ni siri zilikuwa ni makisio ya bajeti ambayo baada ya kupitiwa ilibadilishwa na kupata bajeti halisi ya sherehe, siyo siri nyaraka madiwani waliohudhuria wanazo, vikao vyote hivi vilifanyika kwa ushirikiano wa madiwani wa TLP, Chadema wasiokuwa na mivutano na chama chao na CCM chini ya Meya wa Jiji la Arusha,” alisema Mkombole.
Akichanganua fedha hizo, Mkombole alisema zilikuwa ni Sh123,689,550, Mamlaka ya Maji safi na Majitaka Arusha (Auwsa) walichangia Sh18,156,500 ambazo zilitumika kukarabati mnara wa Azimio la Arusha.
Alisema Kampuni ya Jiangxi Geo Engeneering (Group) Corporation inayojenga barabara za Jiji la Arusha ilichangia Sh12 milioni na China Railway Seventh Group Co Ltd ilichangia Sh4 milioni.
“Halmashauri yenyewe imetumia Sh89,533,050 milioni kugharamia sherehe hizo kwa shughuli mbalimbali zilizobakia, ikiwamo kuwalipa wasanii mbalimbali walioalikwa, kugharamia chakula cha Rais, msafara wake na wageni waalikwa kwenye Hoteli ya Mt. Meru,” alisema.
“Halmashauri yenyewe imetumia Sh89,533,050 milioni kugharamia sherehe hizo kwa shughuli mbalimbali zilizobakia, ikiwamo kuwalipa wasanii mbalimbali walioalikwa, kugharamia chakula cha Rais, msafara wake na wageni waalikwa kwenye Hoteli ya Mt. Meru,” alisema.
Mkombole alisema kamati iliyokuwa inasimamia chakula cha Rais ilikuwa ikiongozwa na Efatha Nanyaro (Chadema), ambaye ni Diwani wa Kata ya Levolosi akishirikiana na Paul Mathysen (CCM), Diwani wa Moshono.
Alisema ushiriki wa viongozi hao ambao ni wawakilishi wa wananchi, unaonyesha suala hilo lilifanyika kwa ridhaa ya Baraza la Madiwani kwa niaba ya wananchi.
Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema, Isaya Doita alikiri kushiriki hatua zote za maandalizi ya uzinduzi wa jiji hilo.
Mwenyekiti wa madiwani wa Chadema, Isaya Doita alikiri kushiriki hatua zote za maandalizi ya uzinduzi wa jiji hilo.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment