WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;
A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy
“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere
Monday, November 19, 2012
Maalim Seif aendelea na Ziara ya kichama Kigoma
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikagua ujenzi wa skuli
ya sekondari ya Amahoro katika kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini, kabla ya kukagua ujenzi wa
Skuli yao ya Sekondari ya Amahoro.
Katibu
Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama
hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma mjini
Mwenyekiti
wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba akizungumza na wafuasi na wapenzi wa Chama
hicho katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kigoma mjini.
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema skuli nyingi za
vijijini bado zinakabiliwa na upungufu wa walimu pamoja na vifaa vya
kufundishia.
Amesema
hali hiyo inapelekea kutolewa kwa elimu isiyo bora ambayo husababisha vijana wengi
kushindwa kupata ajira baada ya kuhitimu masomo yao.
Maalim
Seif ameeleza hayo katika ziara yake ya kutembelea ujenzi wa skuli ya sekondari
ya Amahoro katika kijiji cha Mgaraganza Wilaya ya Kigoma Vijijini.
Amesema ili kuwajenga vijana kitaaluma, ni lazima
waandaliwe kwa kupatiwa elimu bora ambayo itaweza kuwasaidia katika maisha yao
ya baadae.
Katika
risala yao iliyosomwa na mjumbe wa kijiji hicho bwana Said Seif Wagara,
wameiomba serikali kuangalia uwezekano wa kuwasaidia ili waweze kukamilisha
jengo la utawala, ili hatimaye skuli hiyo iweze kufunguliwa na kuanza kazi.
Wakati
huo huo Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF amehutubia mkutano wa
hadhara wa chama hicho katika viwanja vya Kigoma Mjini, na kuwashauri wale
waliokihama chama hicho kurejea ili waweze kuongeza nguvu ya kutetea haki
za wananchi.
Amewaambia
wananchi wa Kigoma kuwa Chama cha CUF bado kipo na kinaendelea kuimarika katika
maeneo mbali mbali ya Tanzania, hasa baada ya kuzinduliwa kwa operesheni
mchakamchaka hadi mwaka 2015.
Amesema
CUF ni chama chenye malengo ya kuwakomboa Watanzania kiuchumi, kisiasa na
kijamii na kuwaomba wananchi wa Kigoma kuendelea kukiunga mkono chama hicho ili
kiweze kufikia malengo yake.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba amewataka vijana wa
Kigoma kusoma na kuifahamu historia ya nchi yao ili kujua malengo halisi ya
kupigania uhuru kutoka kwa wakoloni.
Imewekwa
na MAPARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment