WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, November 24, 2012

Neno La Leo: Hakuna Chozi Lenye Kuzima Moto Uliowashwa Na Mpumbavu...



Ndugu zangu, 

Ninapofuatilia yanayoendelea Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kichwani mwangu ananijia Joseph Mobutu. Utawala wa Mobutu ulifanana sana na ki sa nilichopata kukisoma huko nyuma, kuna kitabu kinaitwa ”Herufi Zilizofanya Maasi”. 

 Alitokea jenerali mdogo, alikuwa ni mtu mdogo hata kwa maumbile, lakini, mwenye mamlaka makubwa sana. Alikuwa mtawala wa imla, dikteta. Hakuruhusu fikra huru katika nchi yake. Alijifanya ni mwerevu wa kila jambo, ingawa hakuwa mwerevu hivyo. Alikuwa ni mtu mjinga aliyeupata utawala kwa bahati tu. 

Na kwa vile alipenda sana kutawala na kuamua kila jambo, alidhani ana uwezo hata wa kuamua juu ya fikra na hisia za watu wa nchi ile. 

Hivyo basi, alitaka watu wa nchi ile wasikie tu kile anachotaka yeye wasikie, na zaidi habari nzuri juu yake na nchi yake. Hakupenda kabisa kusikia habari mbaya zenye shutuma dhidi yake au juu ya mwenendo wa nchi na hali za wananchi. Alitaka udhibiti wa mambo, alipiga marufuku maandiko yote ikiwemo vitabu na magazeti. 

Hakukuwa na ruksa ya kusoma ,kuandika wala kuchapisha maneno huru, fikra huru. Watu wa nchi ile walizipata habari zote juu ya nchi hiyo na za dunia kupitia baragumu la jenerali mdogo. Baragumu lilitangaza yale ambayo jenerali mdogo aliyaelekeza na alitaka wananchi wake wayajue. 

 Lakini, katika nchi ile, aliishi bwana mmoja aliyeitwa Placido. Bwana huyu alikuwa msomaji mzuri wa vitabu ,alipenda pia kuandika. Aliutaka na aliupenda uhuru wa kujiamulia mwenyewe juu ya fikra na hisia zake. 

 Licha ya jenerali mdogo kupiga marufuku ya kusoma na kuandika, Placido aliyafanya yote mawili kwa usiri mkubwa. Alisambaza pia maandiko yake kwa usiri mkubwa. Alitaka watu wayasome, na watu walikuwa na kiu ya kusoma. 

 Mara ile jenerali mdogo alipogundua, kuwa kuna maandiko yanayosambazwa, maandiko yaliyosheheni habari zenye maarifa mbalimbali ikiwemo maarifa ya ukombozi, basi, amri ilitolewa, kwa askari kusaka kila karatasi yenye maandiko. Ulifanyika msako wa mtaa kwa mtaa na hata nyumba kwa nyumba. 

Placido, Bwana yule mwandishi, naye alikamatwa na kufungwa gerezani. Karatasi zote zenye maandiko zilikusanywa, ikawa kama kichuguu kirefu. Zikawashwa moto. Majina ya watu, historia na mengineyo yenye kuelezea nchi ile, yote yaliteketea. 

Wengi walitokwa machozi. Lakini, hakuna chozi lenye kuzima moto uliowashwa na mpumbavu, mjinga. 

Na hilo ni Neno La Leo, tafakari. 

 Maggid Mjengwa,

No comments:

Post a Comment