Na Salma Said
RAIS wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein amesema licha ya serikali kutokuwa na msimamo juu ya suala la mfumo gani wa serikali, lakini Chama Cha Mapinduzi msimamo wake ni kutetea serikali mbili kama zilivyo huku akiukataa mfumo wa muungano wa mkataba.
Dk Shein ameyasema hayo katika mkutano wa CCM uliofanyika jana katika viwanja vya Kibanda Maiti Mkoa wa Mjini Magharibi ikiwa ni sherehe za kumkabirisha baada ya kumaliza mchakato wa uchaguzi wa chama hicho uliofanyika huko Dodoma wiki hii.
Katika mkutano huo Dk Shein alizungumzia jumla ya mambo sita ikiwemo suala la kutetea Muungano ambao asema muungano wa serikali mbili hauna budi kudumishwa kwa kuwa ndio muungano sahihi.
“Kwa hivyo muungano huu utadumu ni muungano imara na muungazo wa kidugu na ni muungano wa kihistoria na zipo nchi nyingi zenye muungano kama huu sitaki nizitaje, l na kuna faida nyingi sana katika muungano huu katika mambo mbali mbali, mambo ya afya, kilimo katika huduma za bahari kuu tunashirikiana na tunafaidika sote, muungano huu una faida kubwa kwetu sisi tuna faida kubwa sana katika serikali hizi mbili, soko la bara ni kubwa tulikuwa tukiagiza vyakula kutoka nje lakini leo hii tunaagiza bara, wengi wetu wanaishi bara wamejenga majumba makubwa ya fakhari, “ alisema Dk Shein
Dk Shein aliongeza kwamba “Muungano huu ni bora kuliko muungano yote duniani kwanza huo wa Muungano wa mkataba sisi hatuujui ….ukiwa na kitu ulichokizowea lazima wende na kitu ulichokizowea sisi tumezowea muungano wa serikali mbili.....,” alisema.
Aidha Dk Shein awali waliposhauriana na Rais Kikwete kuhusu suala la kufanyika kwa katiba mpya waliamua kwamba lengo ni kuendeleza na kuimarisha muungano na sio kuuvunja.
Licha ya kuwa na msimamo huo lakini alisema wananchi wapo huru kutoa maoni yao na hawalazimiki kufungika katika sera za vyama vyao na kila mmoja ajisikie yupo huru kutoa maoni yake huku akisiitiza kwamba CCM ina sera zake za serikali mbili na wengine wenye sera zao za vyama pia wanapaswa kutoa maoni yao.
Alisema “Tume ya katiba imepewa mamlaka ya kupokea maoni wache watu wakatoe sio lazima sote tuwe na maoni ya aina moja wao wana yao na sisi tuna yetu sio lazima tuwafuate nyie,” alisema Dk Shein na kushangiriwa.
Aidha Dk Shein aliwaambia wanachama wa chama hicho kwamba mchakato huu bado unaendelea hatua kwa hatua ingawa msimamo wa serikali bado hatujaotoa kwa sababu tunawaachia wananchi wenyewe, hii ni hatua ya kwanza tu zahma za nini na fujo wakati mchakato huu bado, nilisema mchakato unakuja tume itateuliwa na wenye wajumbe wa pande mbili za muungano na nikasema katoeni maoni yenu na Kikwete hivyo hivyo tumesema hivyo kila pahala wananchi mkatoe maoni yenu vyama vina sera zake” alihoji.
Akizungumzia suala la kuwepo wa muundo wa serikali ya umoja wa kitaifa Dk Shein alisema muundo huo utaendelea kuwepo na hakuna haja ya kuuvunja kwa kuwa lengo la ni kuleta umoja na mshikamano jambo ambalo ndio miongoni mwa malengo ya mapinduzi.
“Serikali ya mapinduzi zanzibar ina muundo wa kitaifa nataka nikuhakikishie kwamba serikali hii tutaiendeleza kwa mustakabali wa wanzanzibari wakiwa wamoja na hili ndio lengo la mapinduzi yetu na hili la umoja, mapenzi na mshikamano alilianzisha Mzee Karume yeye alisaini mkataba watu kuishi kwa umoja na mshikamano kwa hivyo hili sio jambo jipya madhumuni ni kuleta maendeleo katika nchi yetu tukiwa pamoja na mashikamano, vyama vya siasa vinafanya siasa lakini sio kutukanana sio kugombana sio kushutumiana” alisema Dk Shein.
Rais Shein alisema Serikali ya umoja wa kitaifa imetimiza miaka miwili na wamefanya kazi kubwa sana katika kipindi cha miaka miwili ingawa changamoto kadhaa” alisema.
Alisema yeye ndio rais wa serikali na anaongozwa kwa misingi ya sheria na kanuni na hivyo anasaidiwa kazi na wasaidizi wake wawili ambao ni makamo wa kwanza na makamo wa pili na amekuwa akipokea ushauri ambao anaona unafaa na kwa ushauri ambao anaona haufai anaupuuza na halazimiki kupokea ushauri na hapaswi kuulizwa kwa nini anapuuuza kwa kuwa katiba imempa mamlaka hiyo.
Dk Shein akizungumzia suala la kulind ana kuyaennzi mapinduzi alisema hakuna mtu atakayethubutu kuyachezea na hivyo kila mmoja anapaswa kuyaheshimu na kuyathamini kwa kuwa ndio misingi ya uendeshaji wa nchi.
“Suala la kuyalinda na kutatukuza mapinduzi matukufu hilo halina mjadala nitaendelea katika maisha yangu yote kuyatunza mapinduzi tutayalinda tutayatunza na kuyaendeleza ya kuwatumikia wazanzibari wote bila ya ubaguzi, kuondosha ubaguzi wa rangi na jinsia na kadhalika, kuleta maendeleo bila ya ubaguzi lengo lile lile lililotangazwa mwaka 1964 hili ni jambo la msingi hakuna wa kuyaondosha wala kuyabeza madhumuni ya mapinduzi tutahakikisha yale ambayo tumeahidi katika ilani yetu,” alieleza.
Alisema suala la kuheshimiana katika vyama ni muhimu kwa kuwa lengo la kuendeleza umoja na kuwashughuikia wote ambao watatumia fursa ya kuharibu umoja huo na mshikamano na kusistiza kuendeleza siasa za kistarabu bila ya kutukanana na kukashifiana.
“Kila mmoja ana sera za chama chake tutashindana kwa sera bila ya kutukanana bila ya kupigana na wakati wa uchaguzi mkuu tutashindana kwa sera na CCM itashinda tuna sababu nyingi za kushinda sio kwa hila wala sio kwa jambo jengine lolote kwa sababu CCM ina mambo mengi na ina watu wengi,” aliongeza.
Aliwaambia wana CCM suala la kulinda na kutunza amani katika ni ni muhimu na kamwe hatuwachia watu wachache kuvuruga amani iliyopo kwa visingizio vya dini na kuhararisha amani iliyopo nchini.
“Suala la kutunza amani hatutawavumilia na mimi sitamvumilia yeyote yule ambaye atatuharibia amani yetu, nasema hatutamvulia mtu yeyote kwa anayetumia siasa au anayefanya siasa kwa kutumia mwamvuli wa dini” Alisema.
Aidha alisema msimamo wa serikali sio kuwazuwia watu kuendeleza dini zao lakini lazima wafuate sheria za nchi na kuacha kutumia dini kwa kufanya hujuma katika nyumba za ibada au kuwavunjia watu mali zao na kuharibu miondombinu.
No comments:
Post a Comment