Msomaji wangu alitoa maoni haya ambayo kwa kweli yalinigusa sana kufuatia kifo cha msanii John Maganga ambaye alikuwa anafanya vizuri katika kuelimisha umma wa Tanzania.
AnonymousNovember 28, 2012 7:15 AM:
YANI MTU KAFA KWASABABU DAKTARI HAKUWEPO,WAT
A SHAME JAMANI SISI WATANZANIA WAT A SHAME.
“Stephano aliingizwa chumba cha upasuaji, wakati sisi kwa
maana ya mimi na baba yake tukiwa tumekaa, dokta alitoka na kutuambia mashine
za kupumulia zina matatizo kwa hiyo tunafanya transfer ya kwenda Muhimbili kwa
matibabu zaidi, hivyo zilifanyika taratibu na Stephano aliingizwa kwenye gari
la wagojwa na kupelekwa hospitali ya Muhimbili.
Baada ya kufika Muhimbili, Stephano aliingizwa chumba cha
dharura (emergence room), na baada ya dakika kama 10 hivi, alitoka Doctor
ambaye tunafaamiana naye na kusema kuwa, kwa tatizo alilonalo John, hatakiwi
kufanyiwa upasuaji kama walivyofikiria madaktari wa Mwananyamala ambapo
walidhani kuna utumbo umekatika.
Daktari huyo wa Muhimbili aliendelea kutuambia sehemu
ambayo inaonekana kuleta matatizo ni sehemu ya kongosho ambapo vipimo
vinaonesha ina matatizo, ime fell kwa hiyo ina mwaga maji kwenye tumbo ndiyo
maana anapata maumivu kwenye tumbo na tumbo kujaa.
Baada ya maelezo hayo Dokta tunayejuana naye
alitueleza kwamba mtaalamu wa tatizo hili hayupo na kwamba anategemewa kuja
kesho yake asubuhi na kutuasa tuende nyumbani na kwamba watammwekea mashine ya
kupumua na sisi turudi kesho.”
Kwa
kweli kma msomaji ambaye ameeleza hisia
zake hapo jua, ukisoma maelezo haya kweli yanachefua na kuona kuwa hospitali
yetu bingwa ambayo tunaitegemea haina emergency protocol , kwa kweli ni aibu
ambayo kama taifa lazima tuitafutie mfumbuzi mara moja;
Je huyo daktari bingwa haruhusiwi kiitwa ili
aje kuokoa maisha ya mtanzania mwenzetu?
Je daktari huyo bingwa kwa wakati wa tukio
alikuwa Nje ya Mkoa wa Dar es salaam au alikuwa Nje ya Nchi?
Je madakatari wetu bingwa hawaruhusiwi kuitwa
kazini kama kuna issue ya dharua?
Au wanaitwa katika shughuli za dharua kwa
viongozi wa juu tu na familia zao tu?
Je matababu yetu ya dharua yanakwenda kwa
madaraja ili dakatari mhusika aweze kurudi kazini na kuokoa maisha ya mgonjwa?
Maelezo
haya kweli yamesikikisha na kuhudhunisha sana na tunajiuliza sisi watu wa hali
ya chini tukimbilie wapi sasa wakati wa dharura kama madaktari wetu ambao
wanafanya kazi zao kwa viapo ya kuokoa maisha ya watu, hawawezi kurudi kazini kutoa huduma mpaka siku
inayofuata;
Serikali yetu inamelionaje jambo hili, inakubaliana nautaratibu huu wa utendaji ambao hauonyeshi kujali maisha ya raia wake kupitia madakatari wetu bingwa na sekta nzima ya afya:
MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALI PEMA
PEPONI SISI TULIKUPENDA LAKINI MWENYEZI MUNGU AMEKUPENDA ZAIDI NDUGU YETU JOHN
MAGANGA.
No comments:
Post a Comment