CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)
jana kilikamilisha safu yake ya uongozi kwa kuwapitisha kwa kishindo viongozi
wa ngazi za juu wa Chama hicho katika uchaguzi ambao ulionekana kuwa na nidhamu
kutokana na kutokuwa na uharibifu wa kura.
Katika uchaguzi wa safu za
juu za Chama hicho, Mwenyekiti, Makamu wa Mwenyekiti Zanzibar na Bara wajumbe
wa mkutano huo walitekeleza ombi la Yusuph Makamba la kumchagua kwa
kishindo Jakaya Kikwete kuongoza CCM .
Akitangaza matokeo hayo
Spika wa Bunge la Tanzania ambaye ndiye alikuwa msimamizi,Anne Makinda alisema
kwamba Mwenyekiti alipata ushindi wa kura 2,395 sawa na asilimia
99.92 huku kura mbili zikisema hapana.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar
Dk Ali Shein alipata kura 2,397 wakati makamu wa Bara Phillip Mangula naye
alipata idadi hizo za kura huku kukiwa hakuna kura zilizoharibika wala kusema
hapana kwa viongozi hao wawili.
Awali kabla ya kutamka
ushindi wa viongozi wa juu, walitamkwa wajumbe 20 wa viti vya Bara na Zanzibar
No comments:
Post a Comment