WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, November 3, 2012

JK akiri makosa ya serikali katika ujenzi wa sekondari

 
Rais Jakaya Kikwete 
 
Jackson Odoyo na Happy Lazaro, Arusha
RAIS Kikwete amesema Serikali ilifanya makosa makubwa wakati wa
ujenzi wa shule za sekondari kwa kushindwa kujenga maabara katika shule
hizo kiasi cha kuchangia kudidimiza sekta ya elimu ya Sayansi na
Teknolojia nchini.
“Tulifanya makosa wakati tunajenga madarasa ile ya mikondo minne kwa
sababu hatukukumbuka kujenga maabara mapema katika shule hizo kiasi cha
kuchangia kudidimiza elimu ya Sayansi na Teknolojia tangu awali. Lakini
hivi sasa Serikali imeliona hilo na ndiyo maana tukaamua kujenga Chuo
Kikuu cha Utafiti wa Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela
kilichojengwa kwa fedha za Serikali,” alisema Rais Kikwete.

Chuo hicho mwaka jana kilidahili ya wanafunzi 83, huku wanafunzi 30 wakichukua masomo ya uzamivu na 53 ni mafunzo ya uzamili.

Mwaka huu kimedahili
wanafunzi 135 wa kundi la pili,  wakiwamo 46 wa masomo ya
uzamivu na 89 wa uzamili huku asilimia 22  wakiwa wanawake.

Rais alisema kwamba wasomi watakaosoma  katika chuo hicho ni wale wenye shahada ya kwanza baada ya kusoma katika vyuo vingine na watakapofika katika chuo hicho watakuwa na kazi ya kuzama zaidi katika elimu ya utafiti wa Sayansi na Teknolojia.

Rais Kikwete alisema hayo wakati akizungumza na wageni mbalimbali
walioalikwa katika uzinduzi wa chuo hicho jijini Arusha, huku akifafanua
kwamba Tanzania hivi sasa imeanza kuingia katika idadi ya nchi tajiri na
kuondokana na umasikini kama Chuo hicho kitakuwa na maendeleo.
Katika hatua nyingine Rais Kikwete aliwataka wakuu wa chuo hicho,
wakiongozwa na Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal na Profesa David Mwakyusa pamoja na Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Burton
Mwamila  kusimamia maendelea ya chuo hicho kwa dhati.

Naye Mkuu wa Chuo hicho, ambaye ni Makamu wa Rais, Dk Mohamed Gharib Bilal  akizungumnza alisema Serikali itajitahidi kukiboresha chuo hicho ili kiwe chachu ya maendelea barani Afrika.

Katika hatua nyingine Rais Jakaya Kikwete, alisema ili  Nchi ya Tanzania iweze kukua  katika viwango vya nchi ambazo zinaendelea ulimwenguni ni lazima ihakikishe kuwa kwanza inawekeza  zaidi kwenye maendeleo ya Sayansi na Teknolojia.

Katika hatua nyingine  Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Burton
Mwamila alisema kuwa, chuo hicho kitakuwa  na faida kwa jamii.

”Tunategemea mabadiliko makubwa hasa kwa nchi ya Tanzania kwani
chuo hiki kina uwezo mkubwa wa kuwapa fursa Watanzania kuwa na
ujuzi wa kutosha hasa katika maswala ya tafiti na sayansi na kama
Watanzania wataweza kukitumia vyema ni wazi kuwa fursa nyingi
zitaongezeka sana”, alisema Profesa Mwamila.

Source Mwananchi

No comments:

Post a Comment