WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, November 1, 2014

YANGA SC YAPIGWA NA KAGERA SUGAR KAITABA LEO


BAO pekee la kiungo Paul Ngway, dakika ya 52 jioni ya leo limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Yanga SC ilimaliza mchezo huo pungufu, baada ya Nahodha wake, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 80 na refa Abdallah Kambuzi wa Shinyanga, baada ya kumpiga kichwa Rashid Mandawa wa Kagera.

Baada ya mchezo huo, mashabiki wa Yanga SC walimtisha refa kiasi cha kutolewa uwanjani kwa msaada wa askari wa Polisi.    
Kagera Sugar: Agathon Anthony, Benjamin Asukile, Abubakar Mtiro, Erick Kyaruzi, George Kavilla, Babu Ally, Julius Ambrose, Paul Maona, Rashid Mandawa, Atupele Green na Adam Kingwande.
Yanga SC: Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Mbuyu Twite, Hassan Dilunga, Haruna Niyonzima, Genilson Santos ‘Jaja’, Mrisho Ngassa na Andrey Coutinho. GPL
source. Matukiotz.com

No comments:

Post a Comment