KWA NINI
SWALA LA MIGOMO LINACHUKUA MUDA MREFU KUPATA UFUMBUZI?
Kama wataalamu wengi
walivyowahi kusema huku nyuma kuwa chanzo cha migomo mingi kutokea na kuchukua
sura mpya inatokana na kupungua
kwa mawasiliano miongoni mwa pande
mbili ambazo zinatofautiana au kama kuna mawasiliano mawasiliano hayo yanakuwa
hayakubaliki kwa upande mmoja au kutohusishwa moja kwa moja katika majadiliano
husika katika kututua tatizo
husika.
Tatizo wakati mwingine wakati wa majadiliano mhusika mkuu mara nyingi Serikali anachokizungumza pengine kinatia mashaka ya ukweli wa suluhu; Baba Wa Taifa akikuwa akisuluhisha Mgomo wengi walikuwa wakijenga imani kwani alichokuwa akikiongea unaona kabisa anachosema ndio anachomaanisha. Tofauti na viongozi wetu wa sasa mara nyingi wanachoongea na hali halisi ni tofauti kwani wanachukua mno hali ya kujilinda zaidi na mbaya zaidi wanakimbilia kutupa taarifa ambazo zinaongeza wasiwasi baada ya kutatua tatizo.
Nafikiri katika hali yeyote ile serikali kama msimamizi wa sera na taratibu za maisha ya watanzania katika hali ya migomo ambayo imeendelea kujitokeza katika taifa letu, tunahitaji uthubutu katika kutatua tatizo hili;
Katika sakata la mgomo wa
serikali na madaktari ambao umedumu kwa
takribani wiki tatu sasa;
- Swali ambalo tunahitaji kujuuliza leo ni hili Hivi serikali imeonyesha nia ya kumaliza mgogoro huo katika meza ya majadiliano mapema?
- Je madaktari wanajisikia vipi wakiona ndugu zao marafiki au watanzania wakipoteza maisha kwa kukosa hudumu muhimu ya afya ikiwa ni sehemu haki ya wananchi kikatiba?
- Nafikiri Majadiliano na maelewano ni sehemu muhimu katika kufikia muafaka wa migogoro
Hii ni vita ya mafahari
wawili na wanaoumia kwa kiasi kukubwa ni wananchi ambao hawana kosa pamoja na
mchango mkubwa mkubwa wa kodi zao wameishaia kupoteza maisha na kwa mvutano unaoendelea;
Ni kweli kuwa Ikumbukwe
kuwa, serikali ikitenda wajibu wake na na kutoa haki kwa wahusiaka bila
upendeleo kwa wakati sahihi kwa kila jamii ambayo inahusika
kulingana na tatizo linalosababisha mgomo. Migomo mingi ambayo inajitokeza
katika taifa letu inahusiana na tatizo la uwiano wa masilahi (mishahara) katika
jamii pale panapotokea tofauti ya
mishahara iliyowekwa kwa makusudi ya kuwapa nafuu wafanyakazi wa kundi moja
ndiyo inayotumiwa katika kudai nafuu ya wajibu na haki kwa kundi lingine.
Pengine hata swala la
mgomo huu wa madaktari katika kipindi hiki unaweza kusababisha na mvutano wa
posha za viongozi wetu watunga sheria (wabunge) ambao walitaka walipwe posho ya
shilling 200,000 kutoka elfu sabini;(70,000) hii ni assumption moja ambayo
imekuwa kichocheo cha mgomo;
Kama ni kweli kwa nini wanasiasa wanajifikira sana wao wenyewe na kujijengea
hoja na kubeza hoja za wananchi au
makundi mengine ndani ya jamii hasa wanapozungumzia masilahi; ni ukweli ambao haufichi kuwa wanasiasa ambao
ni watawala amabo tumewapa dhamana ya kutuongoza mara nyingi wanajitengenezea masilahi bora,
posho nono na marupurupu mengine
yanayowafanya waishi maisha bora na pale wanapoumwa na familia zao wanatibiwa
nje ya nchi.
Mwalimu Nyererealiwahi sema kuwa , “leo ukigoma unamgomea nani;
tafakari matokeo!” Jibu ni rahisi kada
zinagoma kwa kukosa majibu sahihi ya maswali yao, na kukosekana kwa effective
communication ya madaia husika.
Mwalimu Nyerere kwenye
alitukumbusha kuwa , “Wafanyakazi wa Tanzania wanayo haki ya kuheshimiwa na
wafanyakazi wengine na wananchi wote. Lakini kwa heshima yao wanayoipata,
lazima wafanyakazi wote wakubali kufanya kazi kwa bidii. Ndiyo kusema kwamba
kila mfanyakazi lazima afuate masharti ya kazi anayopewa. Kama kwa sababu
fulani hayapendi masharti hayo, anaweza kupeleka shauri hilo katika kikao kwa
utaratibu uliokubaliwa. Lakini kwa sasa lazima atafuata masharti yaliyopo.”
Tatizo la wakati
wetu tabaka la masilahi bora linaongezeka na kusababisha migomo
miongoni mwa jamii; kwa viongozi wetu na wanansiasa wetu nafikiri ni
wakati mwafaka wa kuitafakari hali hii na kuijengea mikakati ya kuhakikisha
kuwa migomo inatokomea kabisa ndani ya jamii zetu; Hakuna lisikowezekana;
Pamoja tukisima tutaendelea kwa faida ya wote
No comments:
Post a Comment