- NI KWELI KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU?
- KAMA NCHI JIRANI TUMEJIFUNZA NINI?
Siasa
ni mfumo ambao unahusisha zaidi uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria,
sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wananchi wake
hasa katika kuwaleta maendeleo
wadau wakuu kwa maneno mengine wanahisa wakuu ambao ni wananchi.
Kwa
msingi wa utashi huu, wananchi wanakichagua kikundi cha watu au chama ambacho
wanawaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili iwaongoze kwa niaba yao.
Kwa hivyo hakuna nchi yeyote hapa duniani ambayo haina serikali. Tofauti
inayoweza kujitokeza ni namna serikali hiyo inavyoundwa katika misingi ipi? Na
inatekeleza vipi kanuni na taratibu zake? Je kuna uwazi katika shughuli zake? Viongozi
wanabebe dhamana ya watu katika utendaji wao na wawajibikaje kwa wananchi ambao
ndio waliowaweka ofisini; na viongozi wanatakiwa wawajibike na kuwaletea
maendeleo wananchi wao.
Misingi
ya siasa chafu imechochewa sana na mwanasalsafa Machiavelli ambaye
aliandika katika maandishi yeke kuhusu viongozi na madaraka; kitabu chake
kinawanufaisha sana viongozi katika kuimarisha nafasi zao za uongozi,
amewafundisha viongozi namna ya kuwa waongo (liar), wakatili, wanafiki,
kuwa na uchu wa mali, na hata ikibidi kuua ili kupata madaraka na kuudumisha
adhima yao ya kuendelea kunyonya na kujitajirisha. mwongozo huu wa Machiavelli
unatumiwa sana na watawala wa mabavu (dictators), kutoka nchi mbalimbali ambao
waliongoza au wanaongoza nchi zao kwa manufaa binafsi na sio kuwaletea
maendeleo wananchi bali huwajengea hofu na kuwasababishia wananchi wao maisha
magumu. Tumewaona watawala kama; Idd
Amin Dada, Mabuto, na kadhalika. Katika mlengo huu hakuna kuwajibishana,
kinachofanyika hapa wananchi wanatiwa tu kufuata na kusikiliza na kutii tuKila kiti ambacho
wananfanya na wanatakiwa kuwa watiifu kama usipotia au kama ukikidhana kimawzo
na viongozi hao unaishia pabaya tumeona vifo na maisha magumu ya baadhi ya
wananchi, ambao waliishia kuishi ughaibuni.
Uchafu
wa siasa ni pale tunapoilinganisha siasa kama wapiganaji katika mchezo wa
mieleka ule ambao hauna kanuni yeyote ili ushinde, unaweza kumchezee au kumpiga
au kumwangusha mpinzani wako kwa namna yeyote ile uwezayo ili mradi tu wewe uwe
mshindi; hapa hakuna kanuni yeyote inayohitajika refarii yuko pale
kutangaza mshindi tu kwani hana kanuni yeyote ambayo anafuata; hapo ndipo
tafsiri ya mchezo mchafu inapoanza.je nini kazi ya wanasheria wetu? Utetezi au
uonevu? Tatizo la mchezo huu ukiuanza huwezi kuuacha. Ushauri kama huuwezi
kamwe usiucheze waache wanaouweza waucheze, watu wenye kiburi na
wasiojali utu hata mara moja. Na ukiamua kuucheza kamwe usiuache au usiwasaliti
wenzako ukifanya hivyo safari yako yakuendelea kufurahia maisha ya siasa
yataishia kaburini.
Je
siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata
kiongozi wa juu wa nchi anapokiuka maadili ya uongozi?
mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya
akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na
taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini
na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani
ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida
kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.
Siasa
sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneyekevu na wenye huruma ya
kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa
kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke
kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa
yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu
mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo
tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii
iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi
nyingine?
Tukumbuke
kwa wale ambao wamesoma kitabu cha sharkespear nini alikifanya Macbeth
kwa kusababisha umwagaji wa damu ambao ulikuwa hauna sababu kwa sababu tu
ya siasa za ubinafsi na hatimaye kutekeleza mwonekano wa siasa kuwa
mchezo mchafu ambao mwisho wa siku ulimgeukia mwenyewe na kuuwawa. Tatizo la
uchafu wa siasa pengine huanzia kwa serikali kuona kuwa ofisi zao ndio biashara
yao hivyo hata ile mishahara ambayo wamewekewa kisheria haiwatoshi na huanza
kujiingiza katiak rushwa, mikataba mibovu ambayo inawapa masilahi wao binafsi,
na kuwaongezea nguvu ya kipesa na uwezo wa kuongoza kwa masilahi ya watu
wachache.
Siasa
sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneyekevu na wenye huruma ya
kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa
kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke
kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa
yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu
mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo
tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii
iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi
nyingine?
Katika
nchi zetu ambazo umasikini umekidhiri, tatizo la kukosekana kwa ajira, kupeana
kazi na vyeo kwa kufuata undugu na urafiki na sio sifa za elimu, kuwanunua watu
kwa kuwapa zawadi wakati wa kampeni na hatimaye wakati wa upigaji wa kura, kwa
misingi hiyo sio rahisi baada ya uchaguzi kwa wananchi kuwawajibisha viongozi
wao. Siasa taalumu nzuri sana na muhimu kwa jamii ikiwa itawapata viungozi
wazuri na waungwana ambao wamewaeka wananchi mbele ya maendeleo yao, lakini
siasa ikiwapata viongozi wabovu wala rushwa nchi imekwisha na wanyonge hawana
chao ndipo hapo siasa inapokuwa ni mchezo mchafu. Kwa msingi huu ni kuwa siasa
sio mchezo mchafu ni mchafu tu ikipata watu wala rushwa na sio waaminifu,
walafi wa madaraka,
Ni
mchezo mchafu tu kama utaratibu wote wa uchaguzi haukwenda vizuri na matokeo
yake baada ya hapo ni chuki binafsi baina ya vyama na hiyo mwisho wa siku
itamaanisha kuwa chama tawala na chama cha upinzani ni maadui na hakuna
wa umuhimu wa chama kingine kuwapo, vyama vya siasa katika nchi vinaweza
kuiongoza kwa kupokezana ni kama huko Marekani wakati wananchi wanapoona kuwa
nchi iko amani yao ina mashaka wanakipigia chama cha Republican lakini wakiona uchumi wao
unayumba wanakipigia chama cha Democratic;
Tukumbuke
maneno ya Raisi JF Kennedy wa Marekani alivyosema” hakuna mtu ambaye
atanishawishi mimi kufanya kitu ambacho nafikiri sio kwa masilahi ya nchi
yangu, kama wewe au mtu mwingine anafikiri kuwa ndiye, basi huyo ni
Mwendawazimu” Hii ndio tofauti ya kiongozi ambaye kwake siasa ni mchezo mzuri
kwa masilahi ya wananchi wake na taifa lake, ambaye ni mkweli mwadilifu na
ambaye anaweza kutoa maamuzi mazito kwa faida ya nchi yake;
LAKINI pale tunapokosa
maadili ya uiongozi tunakaribisha sana urafiki, undugu na kugeuza ofisi
zetu ambazo zimewekwa kwa masilahi ya Taifa kuwa sehemu za biashara na
kuwakaribisha zaidi wenye fedha kututawala kwa kutoa mwongozo nini kifanyike
hapo ndipo tunabadilisha tafsiri sahii ya siasa kuwa mchezo mchafu. Pengine
bora hata kiongozi ambaye ni mbabe wa maendeleo ya taifa ambaye anapinga uzembe
na hana rafiki wala ndugu ndugu yake ni maendeleo ya nchi yake. Je tunao
viongozi wa namna hii hasa barani Afrika. tumkumbuke Mzee wetu, Mandela Nyerere
na wengine wa namna kama yao.
Uchaguzi
wa Jamuhuri ya watu wa Kenya ambao ulifanyika
March 3 2013 tunamshukuru Mungu umeisha salama ambapo mgombea wa urais
wa Muungano wa Jubilee Bwana Uhuru Kenyatta amefanikiwa kuwashinda wagombea
wenzake nane akiwiwamo mshindani wake wa karibu na waziri Mkuu ambaye amemaliza
kipindi chake bwana Raila Odinga.
Kama
wanahabari wengi walivyoandika kuwa umekwenda vizuri pamoja na kasoro ambazo
zimejitokeza lakini demokrasia imeheshimiwa na wananchi wameyapokea matokea
wakiwa na nia mpya ya kuijenga Kenya mpya. Pengine uchaguzi wa mwaka 2007 ambao
ulishia na machafuko na mauaji ya wananchi ambao hawana hatia tayari limekuwa
ni somo nzuri na wananchi hawataki kurudi tena huko.
Kama
wadau wakuu wa siasa wananchi wameamua kuheshimu matokeo kwa faida ya Taifa.Tuchukue fursa hii pia kuwapongeza Wakenya
kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa amani na utulivu. Ni imani yetu kwamba
utulivu huo utadumishwa pasipo kuathiriwa na hila zinazohusisha uhasama wa aina
yoyote ile.Baada ya maamuzi ya Mahakama kuu kuhusu
Pingamizi ambayo Mheshimiwa Odinga aliweka na Mahakama kutupilia mbali
pingamizi hiyo na MAHAKAMA KUU YAAMUA UHURU NDIYE MSHINDI HALALI
“Mahakama ya Juu imefikia uamuzi kwa kauli moja kuhusu masuala manne yaliyoibuliwa kwenye kesi za uchaguzi. Uchaguzi ulifanyika kwa njia huru na ya haki na kwa kufuata Katiba na Sheria,” alisema Jaji Mutunga kabla ya kutangaza kuwa Uhuru Kenyatta na William Ruto walichaguliwa kwa njia huru na ya haki kuwa Rais na Naibu Rais mtawalia.
“Kesi za Raila na AFRiCOG zimetupwa. Kila mtu ajilipie gharama. Uamuzi wa kina utatolewa katika muda wa wiki mbili.”

Hebu tuangalie kauli mbalimbali
kufuatia uamuzi wa mahakama:
“Mahakama imetekeleza jukumu lake. Jukumu sasa ni kwa raia, viongozi wao, mashirika ya kijamii na wanahabari kuhakikisha umoja wa Kenya unadumu,” alisema Jaji Mutunga.
“Mahakama imetekeleza jukumu lake. Jukumu sasa ni kwa raia, viongozi wao, mashirika ya kijamii na wanahabari kuhakikisha umoja wa Kenya unadumu,” alisema Jaji Mutunga.
WAZIRI MKuu Raila Odinga amekubali
kushindwa baada ya Mahakama ya Juu kutupilia mbali kesi yake kupinga kupinga
kuchaguliwa kwa Uhuru Kenyatta. Bw Odinga amemtakia Rais Mteule kila la heri.
“Hatua yangu ya kwenda mahakamani ilikuwa ishara ya imani yangu katika Mahakama. Haikuwa ni ya kisasi. Tulijaribu kadiri ya uwezo wetu. Mawakili wetu wakiongozwa na Oraro walikusanya na kuwasilisha ushahidi mwingi.”
“Tunasikitika kwamba Mahakama ilikataa ushahidi kwa msingi kuwa uliwasilishwa kuchelewa au mahakama haikuwa na muda. Mwishowe, Wakenya walipoteza nafasi ya kujua nini kilitendeka.”
“Mimi na Kalonzo hatuna majuto kwa kuwasilisha kesi kortini. Ni matumaini yangu kwamba serikali ijayo itaheshimu Katiba na kuitekeleza. Namtakia Rais Mteule Uhuru Kenyatta na kundi lake kila la kheri. Pia, maseneta wabunge, wawakilishi wa wanawake na magavana ufanisi. Tusigawanywe na mtukio haya. Natoa wito kwa Wakenya na wafuasi wangu wakumbuke maneno ya Wimbo wa Taifa – “Haki iwe ngao na mlinzi.’”

Sasa ni wakati wa kuijenga Kenya mpya kwa
kuzika yote yaliyopita ambayo yalileta mtikisiko kama vile ukabila
uliosababisha maafa kama ilivyokuwa uchaguzi Mkuu mwaka 2007. Hakika Wakenya
wameonyesha ukomavu kisiasa na ndiyo maana uchaguzi huu umefanyika kwa amani na
utulivu wa hali ya juu. Bravo Kenya, bravo Wakenya.
Kama
alivyowahi kusema mheshimia James
Mbatia kuwa Uchaguzi wa Kenya ni mfano wa kuigwa kutokana na namna Wananchi walivyohamasika kushiriki katika zoezi la kupiga kura huku Tume ya Uchaguzi nchini humo ikionekana kujipanga ipasavyo kwa ajili ya zoezi hilo.

Tunawatakia
Ndugu zetu wa Jamhuri ya watu wa Kenya kila la kheri katika kendelea kulinda
demokrasia na kuhakikisha kuwa vurugu zilizotokea mwaka 2007 hazijirudii
tena. Uongozi wako Uhuru kama Rais wa
awamu ya nne ukizingatia maadili ya uongozi bora utawaletea faraja wakenya wote
bila kujali tofauti zao za kabila au dini.
God
Bless Kenya
No comments:
Post a Comment