Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika
mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kigogo Dar es Salaam jana
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika
mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kigogo Dar es Salaam jana
Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni Juma Nkumbi akihutubia
katika mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Kigogo Dar es Salaam jana
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
akimtwisha ndoo ya maji mwananchi wa mtaa wa “Msisiri B” baada ya kufungua
rasmi kisima cha maji katika mtaa huo. Picha na Salmin Said-Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
--
Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar na Katibu Mkuu wa CUF
Maalim Seif Sharif Hamad amesema vyama vya siasa vinaweza kufanya kazi pamoja
na kuleta mabadiliko makubwa ya kimaendeleo.
Amesema kitu cha
msingi ni kwa vyama hivyo kuwa na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi.
Maalim Seif ameeleza
hayo kwa nyakati tofauti wakati akiwa katika ziara ziara ya siku moja ya
kutembelea miradi ya maendeleo katika manispaa ya Kinondoni mjini Dar es
Salaam, ambapo baade alifanya mkutano wa hadhara katika eneo la Kigogo.
Amesema suala la vyama
vya siasa kushirikiana katika kuendesha nchi sio jambo geni na kutolea mfano
kwa nchi zilizoendelea zikiwemo za Ulaya.
Maalim Seif ambaye pia
ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar amefahamisha kuwa muda mfupi tangu
kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar imepata mafanikio makubwa
ambayo hayakuweza kupatikana kabla ya kuwepo kwa muundo huo wa serikali.
Ameyataja baadhi ya mafanikio yaliyopatikana kuwa ni pamoja na
kuwawezesha wakulima wa zao la karafuu kupata hadi asilimia 80 ya soko la
dunia, kuongezwa mishahara ya wafanya kazi kwa asilimia 25, pamoja na kupunguza
bei ya pembejeo za kilimo.
Kabla ya kufanya mkutano wa hadhara, Maalim Seif alifungua
kisima cha maji safi na salama katika mtaa wa Msisiri kata ya Mwananyamala,
kufungua Ofisi ya serikali ya mtaa wa Bwawani, pamoja na kufungua ofisi ya
serikali ya mtaa wa Mtambani.
Akizungumzia kuhusu sera za Chama hicho Maalim Seif amesema
lengo lao ni kuwatumikia wananchi ili waweze kupata haki zao kama inavyoeleza
ilani ya chama hicho.
Amesema CUF kinakusudia kuendeleza Umoja wa Kitaifa, na kwamba
iwapo watapata ridhaa ya kuongoza nchi mwaka 2015, chama hicho kitaunda
serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa pande zote mbili za Muungano.
Kuhusu raslimali za Taifa Maalim Seif amesema bado hazijatumika
ipasavyo kuwanufaisha wananchi, ambapo amesema Chama hicho kitaweka sera maalum
ya kuhakikisha kuwa Watanzania wananufaika kikamilifu na rasilimali za nchi
yao.
Ameelezea umuhimu wa kuzingatia matumizi ya rasilimali watu
ambayo imetumiwa na nchi zilizoendelea kuleta mabadiliko katika nchi zao.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara Bw.
Julius Mtatiro amesema mchakato wa kuundwa kwa katiba mpya ya Tanzania ni
changamoto ambayo inapaswa kufanyiwa kazi ili iwe fursa kwa Watanzania.
Amesema bila ya kuwepo na uwazi katika katiba, ujanja na ufisadi
utaendelea kukithiri na kuzorotesha maendeleo ya nchi.
Nao wananchi wa kata za Mwananyamala na Mtambani wameelezea
matumaini yao ya upatikanaji wa huduma bora katika mitaa yao baada ya kuibuka kwa
miradi mingi ya maendeleo ikiwemo ya maji safi na salama pamoja na kuimarika
kwa majengo ya serikali za mitaa.
Na Hassan Hamad
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar
source: Haki Ngowi
No comments:
Post a Comment