Ndugu zangu,
Nimepata kuandika, kuwa Delirium ni hali ya mwanadamu kuwa katika mkanganyiko ( kuchanganyikiwa). Ni maradhi.
Tunayoyashuhudia sasa ni dalili za kuwa tumo kwenye hali ya Mkanganyiko- Delirium.
Katika dunia hii fasihi imetusaidia sana kutujengea uwezo wa kuyapembua mambo. Kuchagua kati ya chuya na mchele.
Wengine elimu yao ni ya darasani tu, mitaani humu tunamoishi haiwasaidii. Ni kama punguani tu.

Leo katika Tanzania hii kuna watu wanakwenda kuombewa ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao. Ni kuchanganyikiwa.
Na tatizo ni hili. Mwanadamu huyu akisimama mtaani na kutamka kwa sauti kuwa anamwomba Mungu wa mbinguni amsaidie anayemdai asahau deni lake, basi, sisi tunaopita njia tutamtazama na kuambiana; " Mwendawazimu yule!".
Lakini, ' mwendawazimu' yule akikusanyika na wengine wakafika hamsini, na mbele akasimama anayefanya maombezi, ambaye kimsingi anafanya kazi kama ya ' waganga' wa kienyeji, akitamka; " Nawaombea kwa Mungu enyi mnaodaiwa na NBC au CRDB, Mungu awasaidie wenye kuwadai wasayasahau madeni yao!"
Hapo tunaopita njia tutaambiana; " Aisee, pale kuna muhubiri anayewaombea wenye kudaiwa wadai wao wayasahau madeni yao!"
Kumbe, lile ni kusanyiko tu la wenye kuota ndoto za mchana. Wenye kuota kuwa NBC au CRDB itayasahau madeni yao waliyokopa. Na watatokea wengine wenye kutoa ushuhuda wa kusamehewa madeni yao na NBC na CRDB.
Kwenye kitabu cha ' Things Fall Apart' hata Unoka, baba yake Okonkwo anayesemwa kuwa alikuwa dhaifu na mtu ambaye Okwonkwo hakupenda afanane naye, alikuwa na cha kutufundisha.
Kuwa kwa mwanadamu anayedaiwa lazima atambue kuwa anadaiwa. Kama umekopa ni sharti ulikubali deni lako. Ndio uungwana.
Anayekudai hawezi kirahisi kusahau deni lake. Wakati wewe utaomba kwa Mungu asahau deni lake, naye pia ataomba kwa Mungu huyo huyo deni lake ulilipe!
Wenye kudai kuwa wanaweza kuwaombea wanadamu wengine ili wenye kuwadai wayasahau madeni yao, hao kimsingi wanajipatia fedha kirahisi kutoka kwa wenye kudaiwa.
Na wengine wenye kudaiwa elimu zao ni za darasani tu, mitaani ni punguani!
Ni Neno La Leo.
Maggid,
Iringa.
http://mjengwablog.co.tz/
No comments:
Post a Comment