Ndugu zangu, Inahusu mila na tamaduni. Unafanyaje unapokuwa na duka na mteja aliye mbele yako ni mama mkwe wako?
Mwalimu, Profesa Mbele ameligusia hili la mila na destruri za Kiafrika kwenye kitabu chake kiitwacho African and Americans; Embracing Cultural Differences.
Kijinini unapokuwa na duka usifikiri tu hesabu za faida ya kibiashara, kuna hesabu za faida za kijamii pia.
Kawaida mama au baba wa mke uliyemuoa haji mwenyewe dukani kwako. Atamtuma mtu. Lakini siku ukimwona mkweo amekuja mwenyewe ujue nyumbani mambo hayajakaa sawa.
Atakutajia mahitaji yake. Atajifanya pia yuko tayari kukulipa. Lakini, unachotakiwa kufanya, ni kuchukua mahitaji yote ya mkweo. Kisha utoka kabisa nje ya duka kumkabidhi mwenyewe kwa mikono yako. Naye atajaribu kufungua mkoba wake atoe pesa. Umwombe radhi haraka, kuwa siku hiyo usingependa atoe hata senti tano!
Na usipofanya hivyo, mkwe atakuona kuwa ni mwanamme usie mwelewa wa mila na desturi.
Maana, Afrika mkwe hawezi kuja mwenyewe dukani kwako, na akija, ujue kaishiwa....Usisubiri akwambie! Ni Neno Fupi La Usiku Huu.
Maggid Mjengwa, Iringa
http://mjengwablog.co.tz
No comments:
Post a Comment