"Sauti ya
mtu imesikika jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake. Kila bonde litafukiwa, kila
mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika patanyooshwa, njia mbaya
zitatengenezwa. Na, watu
wote watauona wokovu utokao kwa Mungu."`
"Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani
aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja? Basi, onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu”.
Umati wa watu ukamwuliza, “Tufanye nini basi? Akawajibu, Aliye na nguo
mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo. Nao watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, Mwalimu,
tufanye nini? Naye
akawaambia, Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa. Nao askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye
nini? Naye akawajibu, Msichukue vitu vya
mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara
yenu."
Leo natamani
kulizungumzia neon hili Toshekeni na mishahara yenu:
Neno hili ni zito japo lilizungumzwa kipindi
kirefu nyuma lakini tunaendelea kulishuhudia leo tunapowaangalia watendaji wetu
katika serikali zetu; Neno hili linatufundisha uadilifu, uwajibikaji kulingana
na maadali na kanuni za kazi ambazo
zinatulazimu sisi kama watendaji wa Taifa kuweka mbele matakwa ya Taifa na sio
masihahi binafsi;
Najiuliza
tena Neon hili linamaana gani kwa taifa
letu?
Kama nchi na
wananchi wake tunahitajii uhuru wa kiuchumi ambao unatokana na viongozi wetu waridhike
na mishahara yao; kinyume chake kama hawataridhika na mishahara yoa na kuweka
mbele masilahi yao vitendo vya rushwa na
ufisadi ambao unarudisha maendeleo ya Taifa nyuma sana vitadhidi kuendelea.
Ujumbe wa Pasaka ya mwaka 2013 utukumbushe sisi Kama Taifa na kama Raia na watendaji ambao
tumekula kiapo cha utii na maadili bora ya uwajibikaji kwa Taifa letu kuwapa
wananchi wanyonge zawadi kubwa ya
uhuru wa kiuchumi ili kila mmoja wetu aweze kuyafurahia hii zawadi pekee ya rasilimali ambayo Mungu amelijalia Taifa hakuna
atayepingana nami kuwa nchi yetu
imefurika kwa uwingi wa asali na maziwa tatizo ni huluka ya kushindwa kutosheka na tukipatacho kwa watendaji wetu na kusababisha, wachache tu ambao wanafaidi rasilimali hii tuliyojaliwa na Muumba wetu.
kwa kipindi kirefu tumeona kuwa nchi yetu Tanzania iliyokuwa ikifurika neema ya rasilimali sasa imegeuka; kwa wengine imekuwa ni nchi inayofurika machungu; matendo yaleyale ya kifisadi, ya ukandamizaji, ya unyanyasaji ambao Farao aliwatendea wana wa Israeli huko misri miaka hiyo; lakini kwa kuangalia falsafa hiyo ya matendo ya Farao ndio tunaona Namna watendaji wetu walikokabidhiwa dhamana ndani ya Taifa letu ambao sio waadilifu wananyatenda sasa yanaenda kinyume na uhuru tuliopewa kama zawadi kuto kwa Mungu ambao kila mmoja anastahili kufurahia na kufaidi asali na maziwa yanayofurika katika nchi hii. Na sio kwa kikundi kidogo cha watu.
Yohane Mbatizaji kwa usitadhi kabisa anayafafanua makundi yaliyokusanyika kwa kuwaeleza uwiano sahihi wa toba. Kulingana na Yohane matajiri wanaotakiwa kuangalia haki ya masikini, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo."(Lk 3,11), kwa watoza ushuru waepuke rushwa na matendo ya kifisadi "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."(Lk 3,13) na kwa maaskari wazingatie haki "Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo. Toshekeni na mishahara yenu."(Lk 3,14).
Leo hii ndani ya Taifa vitendo hivi vimeshamiri tena kwa kiasi kikubwa katika jamii yetu, na pengine kila mmoja ameshiriki kwa namna moja au nyingine katika uovu huu, moja kwa moja au kwa kutokuwajibika ipasavyo katika eneo lake la kazi na hivyo kusababisha mianya katika kukua kwa matendo haya maovu. Wito wakati tusherekea Pasaka 2013 sisi kama Taifa inatupasa tubadilike na kuhakikisha haki na upendo vinashamiri katika jamii yetu.
Kama tutafanikiwa kuishi kwa ujumbe huu wa Yohani Mbatizaji kuwa tutosheke na mishahara yetu mimi naamini kuwa tukiweka mbele maslahi ya nchi, taifa letu na wananchi wake hasa wanyonge tutasonga mbele. TUKUMBUKE KAULI YA YOHANA MBATIZAJI KWA WALE ASKARI kuhusu dhuruma: TOSHEKENI NA MISHAHARA YENU, watu wana madaraka makubwa mishahara mikubwa na masurufu manono lakini bado wanaiibia nchi.

Hebu tujaribu
kuangalia kauli ya Mheshimiwa Lusinde alidai kwamba “Malipo
yetu ni kidogo sana, hayatoshelezi kabisa lakini wananchi tunaowawakilisha
hawatuelewi katika hili, maana wanadhani tuna fedha nyingi, sasa hapa kuna
tatizo. Nadhani kuwapo utaratibu wa kuwaelimisha, wajue hata kazi nyingine
tunazofanya siyo wajibu wetu ila tunajitolea na nyingine hizi zina gharama
kubwa.”
Kama mwandishi
mmoja alivyowahi andika kuwa “Tatizo la waheshimiwa hawa wakishapata kura
wanageuka viumbe tofauti kabisa na wale waliokuwa wakijifanya wana uchungu
kweli na wapiga kura wao. Wanasahau kuwa wengi wa wananchi waliowapigia kura
waheshimiwa hao kuingia bungeni ni masikini wa kutupwa na hawana wa
kumlalamikia (na hata wakilalamika ni kazi bure maana wawakilishi wao nao wapo
‘bize’ kulalamikia mishahara na posho)”.
Je watendaji wetu wako tayari kutoa hesabu za utendaji wao siku
watakapotakiwa na Mwenyei Mungu tukiamini kuwa kazi zote hutoka kwa Mungu “Sisi
tunajielewa kuwa ni watendakazi wa saa ya kumi-na-moja katika shamba la Bwana
la siku za mwisho, na kwamba ingawa mishahara yetu haijulikani na mapema,
lakini hatuna mashaka kwa sababu Bwana wetu ni mkarimu”.
Nafiki Pasaka hii kujifunze kitu kingine kipya kuwa “Jihadharini
na tabia ya kupenda fedha, na “toshekeni na mlivyonavyo” kwa sababu Mungu
mwenyewe alisema,
“Kwa vyo vyote sitakupungukia kabisa, wala sitakutelekeza na
kukuacha bila msaada. Kamwe, kamwe, sitakuacha hata kwa kiwango kidogo,
kukuacha bila msaada, au kukuacha, au kukuangusha, au kulegeza mkono wangu
kwako. Hakika sitafanya hivyo! Kwahiyo tunafarijika na kutiwa moyo, na kwa
uhakika na ujasiri twathubutu kusema, ‘Bwana ndiye anisaidiaye” (Ebr 13:5, 6)
Kwa kutosheka na mishahara yetu na kwa kuamini kuwa sisi ni
wachache ambao tumechaguliwa na Mwenyezi Mungu kuwa saidia wengine ili waweze
kupata ridhiki zao; au kufurahia asali na maziwa kwa vipaji vyetu kwa kutimiza
ibu wetu tutakuwa tunatekeleza ujumbe huu wa “Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu
na haki yake na hivi vitu vingine vyote mtapewa k maelefu.
Tukitenda kila kitu kwa haki kamwe hatutakosa chochote
tunachohitaji ambacho kitakuwa ziada. Mwenyezi Mungu atakupa namna
ya pekee kukidhi mahitaji ya ziada.
Imani yangu ni kama ile ya Paulo kama tutatosheka na mishahara
yetu,na kuwajali wanyonge katika Kupata Riziki
zao basi “Na Mungu wangu
atawajazeni na kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu…”.
Tunaona mambo mengi yanaendelea ndani ya Taifa letu ikiwa na
matokeo ya ubinafsi na ufisadi; tumeshuhudia
- matokeo mabaya ya vijana wetu ambao wamefanya mitihani ya kidato cha nne mwaka 2012; na matokeo haya yameitwa ni janga la Taifa;
- tunaendelea kushuhudia huduma za afya ambazo hazikidhi kiwango kwa wananchi wanyonge
- tunaendelea kushuhudia mauaji ambayo yanaendelea ndani ya jamii yetuna mengine mengi.
Kwa nini haya yote yanatokea jibu ni moja tu watendaji wetu
hawatosheki na mishahra yao na hawan muda wa kulisaidia Taifa wako bize na
shughuli binafsi ambazo ziko nje ya maadili na hata hawana muda wa kuangalia
mitaala mizuri ya elimu ya vijana wetu huu ni mfano mdogo tu.
"Mungu hatakosa kuwajazi wale wote wanaoifanya kazi yake
sawasawa na mapenzi yake" huu ndio ujumbe wa Pasaka 2013
Emmanuel Turuka
Kalamazoo Michigan
madobole@gmail.com
No comments:
Post a Comment