WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, January 25, 2012

KATIBA HII NI YETU SOTE;

MARIDHIANO KATI YA VYAMA vYA UPINZANI NA ASASI ZINAZOTAKA KUSHIRIKI MCHAKATO HUU KWA MANUFAA YA WATANZANIA NI JAMBO LA BUSARA SANA;



"Kazi ya kutengeneza katiba ni ya wananchi, katiba ni ya wananchi, kwa manufaa ya wananchi," anasema Bw. Kiwanga

Kauli za makamu wa pili wa Rais Zanzibar Mheshimiwa Maalim Seif “Wananchi wanapaswa kujiandaa kutoa maoni bila ya uoga, na jambo muhimu ni kuhakikisha katika maoni yao hawamtukani mtu: Nyinyi Wazanzibari na ndugu zetu wa Tanzania Bara ndio tuliovaa kiyatu (Muungano) na aliyevaa kiyatu ndiye anayejua msumari unachomea wapi, au anayelala kwenye kitanda ndiye anayejua kunguni wake”,


Mheshimiwa Maalim Seif aliendelea kueleza kuwa “katika kuzingatia mambo yenye maslahi kwa Zanzibar wasitokee watu wakaweka maslahi binafsi mbele, alisema haitakuwa jambo la manufaa kwa Zanzibar iwapo watajitokeza baadhi ya viongozi wakaanza kujadili nafasi zao za Ubunge na uongozi, iwapo muundo Fulani wa Muungano utapita”

Kauli za Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia   “Tunakupongeza kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala zito ambalo litatupa uhai vizazi na vizazi vijavyo. Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya Katiba kwa amani na hoja bila kuvuruga amani yetu suala la Katiba linahitaji ushirikiano wa pamoja kwa nia njema, kwani taifa hili ni letu sote;  Ni jambo kubwa sana, wewe ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata katiba mpya na kuanzisha Mchakato wa kupata Katiba Mpya.”

WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, “Katiba mpya izingatie matakwa ya wananchi ili kuliweka taifa katika hali ya utulivu. Hili la Katiba mpya ni jambo mhimu na nyeti…tunataka Katiba ijayo ikidhi matakwa ya Watanzania. Tume itakayoundwa na rais kukusanya maoni ifanye hivyo bila konakona fulani fulani,”

Mheshimiwa John Mnyika “Izingatiwe kuwa kwa sasa Tanzania haifanyi marekebisho ya Katiba bali tunakwenda kufanya mapitio (review) na hatimaye kuwa na katiba mpya; hivyo suala la ushirikishwaji wa umma sio katika kutoa maoni tu bali kuamua misingi muhimu ya katiba ni suala lenye umuhimu wa pekee ili tuwe na katiba inayokubalika na umma mpana isije yakajirudia tena yaliyojitokeza kwenye kuandikwa kwa katiba ya mwaka 1977”.


Mheshimiwa Mbowe amekuwa akisisitiza kuwa "Suala la katiba mpya limetekwa na baadhi ya wanasiasa ambao hawajui ni fursa ya kila mtanzania, wapo wengine wanaona chadema inapinga kuwepo kwa katiba mpya, sisi tunahitaji sana na tunachokitaka wananchi washirikishwe na waamue wenyewe,”



Hivi karibuni tumeendelea kuona nia njema ya Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na majadiliano na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa ambavyo vinajenga kambi ya upinzani; kama waandishi wengi walivyoandika na kuendelea kuandika kuwa “ Tunachotaka kusema hapa ni kwamba viongozi hao wa pande hizo mbili wametupa matumaini mapya kwamba sasa upo uwezekano mkubwa wa kupata Katiba Mpya ya kuipeleka nchi yetu kwenye maendeleo katika misingi ya demokrasia na utawala bora. Tunasema hivyo kutokana na dhamira ya kweli iliyoonyeshwa na pande hizo mbili katika mazungumzo hayo ambayo vyanzo vyetu ndani ya Serikali vimethibitisha kuwa, mazungumzo hayo yalikuwa magumu na yasingefanikiwa iwapo pande hizo zingetanguliza ubinafsi na  itikadi za vyama vyao.”


Tunahitaji kuendelea kuelewa kuwa tutapata katiba mpya lakini tunahitaji katiba ya aina gani? Katiba ambayo itaelemea upande mmoja wa mlengo Fulani wa kikundi cha watu na chama chao; jibu ni hapana tunahitaji katiba ambayo italenga mpya kuwakwamua wananchi wa Tanzania wa pande zote bila ubaguzi; tunachohitaji sana wanasiasa wetu katika kipindi hiki wawe kweli wanaupeo  na  wawe na ukomavu wa kisiasa  ambao ni pamoja viongozi kuwa na uvumilivu na kujua jinsi ya kutatua matatizo bila kusababisha malumbano , na kujenga chuki miongoni mwa wananchi.

Majadiliano  ya hivi karibuni ya vyama vya CHADEMA, NCCR-MAGEUZI, CUF  pamoja na serikali ambayo ndio msimamizi mkuu wa mchakato huu wa katiba ambayo sasa tunaanza kuona kuwa inamwelekeo wa  unaoleta matumaini zaidi kwa masilahi ya Taifa na sio chama au kikundi Fulani cha watu; au kuingiza siasa  za vyama ndani ya mchakato kwa vile katiba itabeba  sheria mama ya nchi ni vizuri kutatoa ushirikiano wa dhati katika mchakato huu kwa maslahi ya nchi


Itakuwa ni kitu cha busara na cha kupongezwa sana kama vyama vya siasa kwa uwezo wao wa uenezi kuanza kuwaelimisha na  kuwashirikisha wananchi katika utoaji wa maoni  katika mchakato wa kutengeneza Katiba amabayo itaweza kutuvusha  sio tu katika  kuendeleza amani bali hata katika kuleta maendeleo ambayo tunayahitaji sasa kuliko wakati mwingine wowote; kama tutaweza kuhamasiha wananchi wetu waweze kuchangia tutakuwa  kumeipa (legitimacy ) yaani kweli ni katiba inayokubalika kwa kila mtu na hakutakuwa na malalamiko kuwa wananchi wameporwa mamlaka  ya utengenezaji katiba.
kama wataalamu wengi walivyowahi kuseaka kuwa Demokrasia kwa ufupi ni dhana inayolenga ushiriki wa wananchi, katika kuweka misingi sahihi ya uendeshaji wa nchi na wao wakiwa ndio msingi wa mamlaka yote ya nchi nawalio na uwezo wa mwisho wa kuipa serikali madaraka na mamlaka hayo ya kuongoza nchi. Kwa mantiki hii moja ya msingi mkuu unaokuza demokrasia ya namna hii ni Katiba ya Nchi. Katiba ni msingi mkuu wa uendeshji wa nchi,ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria. Yenyewe ndiyo sheria na ni kioo cha maisha bora  ya wananchi wake:



Tunahitaji Katiba iliyomadhubuti huwa  ambayo ni msingi mkubwawa utawala bora; kwani katiba bora  inazingatia uwazi, uwajibikaji na utawala wa sheria dhana ambayo kwa ujumla ni msingi wa kwanza wa  demokrasia na maendeleo ya nchi. Lazima tuendelee kusisitiza kuwa ukweli ni kuwa katiba inayopendekezwa  inatakiwa iwe ni  mradi wawananchi wa Tanzania Bara na Visiwani. Katiba mpya itakuwa ya watanzania wote na tusikubali ifanywe kuwa ya serikali iliyopo leo na itakayokuja kesho.

Katiba mpya ikikamilika tunatamani itufanyie haya yafuatayo:
·        Ituletea kiongozi Mzuri pamoja na serikali yake;
·        Ituletea chama chenye sera bora, kwa masilahi ya wanachi
·        Ituletea watumishi wa serikali na umma ambao ni waadilifu
·        Iendelee kutudumishia amani ambayo tumeifurahia kwa muda mrefu sasa


Nahitimisha kwa kusema hivi jamani watanzania wenzangu, wanasiasa, wananchi na wananchi wote kwa ujumla kuwa;

"Tanzania ni yetu, hatma ya taifa hili iko mikononi mwetu, tuwajibike, tuache woga, tujadili, tufikie mwafaka wa kitaifa. Katiba mpya ni jibu. Jibu la kurudisha maadili ya taifa na kulinda rasilimali za taifa. Tuchukue hatua, Hivyo Katiba inapaswa kuwa ni matokeo ya mwafaka wa kitaifa kwenye masuala yote ya msingi ya nchi husika”

No comments:

Post a Comment