WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, January 23, 2011

VIONGOZI WETU WANA SIFA HIZI?

SWALI AMBALO MIMI NAJIULIZA NI HILI:



  • VIONGOZI WETU WAKUU WA NCHI NA VYAMA VYA SIASA WANATAKIWA WAWE NI WATU WA NAMNA GANI?

Nionavyo mimi kiongozi ni mtu yeyote ambaye anasifa za kuongoza, kusaidia, kupuuza mambo yasiyo na msingi na kuwasaidia wananchi walio mchagua yeye kuwa kiongozi; Je sasa viongozi wetu amabo tumewapa dhamana ya kuongoza nchi na vyama vyao vya siasa waweje?

Nafikiri wakiwa na sifa hizi watavisaidia sana  vyama vyao na wale wanaoongoza nchi wataharakisha kuwaletea maendeleao, amani na utulivu wananchi wao;

·       Awe ni mtu mzuri wa mfano wa kuigwa kiutendaji na kwa maisha yake katika matendo yake binafsi; Awe ni mtu wa mifano mizuri kwa kila mtu

·       Awe ni mtu ambaye anaweza kutofautisha kati ya baya na njema na yeye anafanya mambo ambayo ni mazuri kulingana na taratibu za nchi na kulingana na imani yake na namna anavyomwogopa Mungu wake.

·       Awe ni mtu ambaye ataifanya  nchi anayoiongoza na chama chake kuwa kimbilio la wanyonge wanaodhulumiwa haki zao;

·       Awe anaishi kwa misingi ya maadili yafuatayo;
1. “Trustworthiness” inayojumisha ; integrity – kuwa na msimamo kuhusu kile ambacho anatakiwa kusimamia hata kama hakitawafurahisha wengine hata kama wanatoka ndani ya chama au serikali anayoingoza, kwa kufanya hivyo utakijengea sifa chama chake na serikali anayoiongoza.

2. Awe mwaminifu (honesty) msema kweli na kuwa mwaminifu na sio kiongozi ambaye anaropoka ropoka kwa faida ya wachache, ndani ya serikali na chama chake matokeo yake atakuwa anakimaliza chama chake kwa kujenga hatari ya kukigawa chama chake.

3. Awe “Reliable na Responsible”  katika matendo na kufanya kile ambacho anatakiwa kufanya kulingana na kanuni zilizokuweka katika nafasi aliyonayo na sio kufanya kwa kumfurahisha mtu au kikundi cha watu wachache.
4. Respect  awe anaishi kwa misingi ya sheria ya Dhahabu “ mfanyie mwenzako vile ambavyo wewe unataka kufanyiwa” awe mtu anayeheshimu watu lakini asiwe Yule ambaye anabadilika badilika kama kinyonga;

5. Awe Mvumilivu na anayekubali ukweli na  sio mwepesi wa kuhukumu matendo ya wengine bila kuyapima kwanza, awe mwenye heshima na msikifu kwa hoja za wengine na yuko tayari kujadiliana ili kuondoa tofauti miongoni mwao.

6.Awe ni kiongozi ambaye anahubiri amani kwa vitendo/matendo (nonviolence) kwa kuondoa hoja zilizojaa vitisho na matusi na anayeweza kumaliza hasira zitokanazo na utashi wa kisiasa kwa amani na sio kwa nguvu na ushawishi wa kuvurugu amani ambayo iko;

7. “Courtesy”  mwenye hekima, sio mropokaji, mtusi, awe mpole kulingana na sheria(haki) yaani myenyekevu na sio mtumwa wa mawazo ya  wengine awe na msimamo binafsi ambao unamlinda kisheria na kimaadili ya uongozi  kulingana na nafasi ambayo anayo;

8. Awe tayari kuwajibika (accountability) anayekubali kuwajibika kwa utendaji wake mzuri au utendaji wake mbaya; asiwe mtu wa kushinikizwa kukubali jambo lolote;

9. “Self control” awe ni kiongozi ambaye anaweza kutawala hisia zake na maisha yake ambaye ananidhamu ya uwajinikaji; anayejua mipaka yake ya utendaji wa kazi na daima kwa kiasi kikubwa anaweza kufanya maamuzi yeye mwenyewe ambayo yakakubalika na wengi na sio kutegemea mtu au kikundi Fulani.

Kwa kifupi kiongozi tunayemtaka "tunaomba" awe, mwadilifu,  ambaye anayoyasema ndio anayotenda, na ni mpatanishi; kwa maneno mengine awe KIONGOZI ambaye hapendezwi na  rushwa  "Fisadi"; anayeweza kubadili mwelekeo wa kiuchumi kuwa endelevu kwa manufaa ya wote ( taifa) na sio kikundi kidogo cha watu.

No comments:

Post a Comment