WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, January 6, 2011

KATIBA MPYA TANZANIA




JE TUNAHITAJI BUSARA KWA KIASI GANI SASA KUELEKEA MCHAKATO WA KATIBA MPYA?

Rais wa Jamuhuri ya Muungano ya Tanzania Mh Jakaya.M. Kikwete katika salamu za mwaka mpya wa 2011,; ametoa tamko la “kuanzisha mchakato wa kuitazama upya Katiba ya Nchi yetu kwa lengo la kuihuisha ili hatimaye tuwe na Katiba inayoendana na taifa lenye umri wa nusu karne” kwa upande wangu hii ni dalili njema ambayo Taifa lilikuwa linaisubiri kwa kipindi kirefu;

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na malalamiko kutoka hasa katika vyama vya siasa kutokupewa na kutotendewa haki katika maswala yanayohusu ushindani  wa siasa kwa misingi kuwa chanzo cha tatizo ni Katiba. Kwa maelezo na malalamiko mengi katiba ambayo inatumika sasa inaipendelea sana chama  Tawala (CCM) na serikali yake.

Katiba yeyote ile ili uweze kukizi haja lazima ilenge katika kumkomboa mwananchi wa kawaida; na mwananchi wa kawaida ndiye muhimili wa nchi kwani yeye anayetoa idhini ya utekelezaji wa katiba ya nchi kupitia kura yake ya kuichagua serikali kupitia siasa. Serikali baada ya ridhaa ya wananchi hutekeleza majukumu yake kupitia Katiba.

Katiba haitamsaidia mwananchi wa kawaida kama haijui na kuilewa; ni jukumu la msingi wananchi waelemishwe kuhusu nini maana ya katiba na vipengele vyake vya msingi. Kama  mtaalamu mashuhuri wa mambo ya Katiba Profesa Shivji alivyosema suala la kuandikwa katiba mpya lazima wananchi washirikishwe; ushirikishwaji ambao Prof Shivji anauainisha hapa ni elimu ya Katiba ambayo inapatikana ndani ya elimu ya uraia.

Elimu hiyo itawasaidia wananchi kuweza kujibu maswali haya katika kipindi hiki cha mchakato wa Katiba ya Nchi yetu;
·        Je katiba yote ni mbaya au kuna baadhi ya vifungu hivyo vya katiba ni vibaya? Na vipengele gani hata kama katiba itaamuriwa kuandikwa yote lazima vibaki?. Je kuna umuhimu wa kuiandika upya na nini maana ya kuiandika upya?

Tusipoluwa makini mjadala huu wa katiba utatawaliwa na wanjanja wachache ambao wao watajiita ni wawakilishi wa wananchi, hao ndio wanasiasa wetu; wasomi wetu; wanafanya biashara wakubwa; lazima tukubali kuwa tunahitaji busara, uvumilivu na ushirikano wa hali ya juu katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mpito wa katiba wan chi yetu; u mimi na u sisi utatuweka pabaya katika kulivusha taifa letu salama katika nchi ya matumaini na maendeleo ya kila mwananchi wetu;
Nukuu
·        "Suala la katiba mpya kwa sasa haliepukiki na serikali inapaswa kushirikiana na vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa, kuhakikisha kuwa katiba inayoliliwa na wananchi, inapatikana na kukidhi matakwa yao," nafikiri hapa tuongeze  suala la katiba ni suala la Watanzania wote lisilofungamana na itikadi ya mtu (tusiwaache wale ambao hawana mapenzi na vyama vya siasa)
Je ni njia gani zitumike katika kuipata katiba yenye hadhi ya utaifa kwa maendeleo ya nchi, nafikiri hili linajadilika;
·        Parliamentary constitutional review commissions ( iwe chini ya Bunge)

  • ·        State-dominated special commissions ( iwe Chini ya Rais)
  • ·        constituent assemblies with citizen participation (iwe chini majimbo kwa kuwashirikisha sana wananchi)
kama wengi wanavyofikiria na ni wazo nzuri iwe kupinga kitendo cha tume hii kuwa chini ya Rais. Itapendeza kama hii tume ingekuwa chini ya bunge, kwani tume za Rais mara nyingi zinakuwa sio transparent na chances za kuwa biased au colluded ni kubwa. Wataalamu kama Dr. Slaa na waandishi wa habari kama Maggig Mjengwa, na wengine wengi wana mtazamo huu.


Daima tukumbuke kuwa  Kesho inaweza tu kupatikana kutokana na  watu watakao fanya maandalizi leo (elimu ya uraia kwa wananchi wetu), japo tunaishi leo bali tunatakiwa kuiandaa kesho yenye nuru tukumbuke kuwa Nyota Njema huonekana Alfajiri. Kama tutazingatia kuwa tunatakiwa kuitumikia nchi yetu na watu wake wote,  kujito kwa moyo katika  kuondosha umaskini, ujinga, magonjwa na dhuluma, kuikataa Rushwa na kuiona kuwa ni adui wa haki,  na hivyo kutoitapokea wala kutoa rushwa na hatimaye  kushjirikiana na wenzangu wote kujenga nchi yetu na kuwa muwazi katika kusema  kweli daima, fitina kwangu mwiko. Hili ni jukumu la kila mtanzania katika ngazi yeyote. Nina imani inchi yetu itakuwa  ni mahala pazuri sana pa kuishi, tukumbuke kuwa hata Marekani haikujengwa siku moja tunatakiwa kuchapa kazi na kuwa wakweli waungwana na waaminifu katika majukumu yetu. 

TANZANIA NCHI YETU TUNAIPENDA 

No comments:

Post a Comment