WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, June 11, 2011

SEMINA ELEKEZI VS MAADILI YA UTENDAJI KAZI

UKOSEKANAJI WA MAADILI KATIKA UTENDAJI WA KAZI NDANI YA SERIKALI;



Siku za hivi karibuni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania alifanya semina iliyoitwa”Elekezi” kwa watendaji wakuu wa serikali; lengo la semina hiyo ilikuwa ni kujaribu kuwakumbusha watendaji hao kuhusu wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku katika utendaji wao;

Je lengo la jumla la semina hiyo ilikuwa nini?

Kuwakumbusha watendaji juu ya utendaji wao ambao hauna tija?

Kujisafisha mbele ya wananchi wa Tanzania kuhusu kushindwa kwa serikali kufikia malengo ya mipango yao ya utendaji?

Kwa nini Rais  amewataka wateule wake katika ngazi zote za uongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa; wawe watu wa kupigiwa mfano, wasinyooshewe kidole kwa ulevi, uchelewaji kazini na kuwahi kuondoka, kwa uzembe, wizi, kutumia ofisi kujinufaisha, kwa uzinzi na ubabe?.

Je watendaji wake wengi ni mzigo kwa serikali?
Nani amewachagua kushika wadhifa huo mkubwa na kama ni mzigo kwa nini wasitemwe?

Kwa nini Rais amewashauri kujielimisha kuhusu kusoma na kujua zaidi kuhusu katiba, sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazoongoza utendaji kazi katika sehemu zao za kazi.
Kwanini amewataka watendaji hao kuacha umangimeza, badala yake watoke ofisini kujionea matatizo ya wananchi. Mawaziri na makatibu wakuu lazima mtoke. Hiyo ndiyo njia bora zaidi ya kujua mambo yahusuyo wizara zenu na ndiyo njia bora ya kuongoza: kuona wenyewe na kutenda?

Nani aliwachagua kushika nafasi hizo, je ni vigezo gani vilitumika kuwachagua watendaji hao, je ni watendaji ambao hawana uzoefu au elimu yao inatia mashaka, au wamejikita zaidi katika rushwa?

je kwa nini baraza la mawaziri halifanyi kazi kupitia utaratibu wa  “uwajibikaji wa pamoja? Kwani walipochaguliwa hawakueleza utendaji wao ni wa pamoja? Nani kavuruga uwajibikaji huu wa pamoja? Hata miswada ya sheria bungeni ni ya mawaziri wote; Ni kinyume cha maadili Waziri kupinga muswada wa Waziri mwenzake?
Kwa nini wanapingana wao kwa wao? Who is behind the scene?

Lakini nafikiri sio sahihi kwa mheshimiwa Rais kuwapa nafasi ya kujiondoa kama hawafai; nafikiri wanatakiwa waondolewe kama hawafai? Tusiogope kuharibu urafiki kwa kuwaacha watendaji wabovu katika nafasi zao za kazi waendelee kuharibu na kutowajibika.

Je watendaji wetu wanafanya kazi kulingana na kiapo wanachoapa wanapokabidhiwa madaraka? Kama wanafanya ndivyo sivyo kwa nini tuwaachie muda wajiondoe, tuwaondoe.

Semina hii yote ililenga katika kuwakumbusha watendaji wetu umuhimu wa kufuata maadili ya uadilifu na utawala bora;

Kwa hiyo nasema tena hapa tatizo letu kuu ni maadili. Maadili yamemomonyoka kabisa. Watu wanafanya kazi kwa mazoea mno. Hakuna umakini na wala ufanisi. Watendaji hawaguswi na hali mbaya za wanaowahudumia. Rushwa ufisadi na kutojali mahitaji ya wanaohudumiwa ni kigezo kikuu cha kushindwa kutatua matatizo.

No comments:

Post a Comment