WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, December 2, 2010

JE NI KWELI KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU? ( IS IT TRUE THAT POLITICS IS A DIRTY GAME?)

Siasa ni mfumo ambao unahusisha zaidi uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria, sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wnanchi wake;katika kuwaleta maendeleo  wadau wakuu ambao ni wananchi.

Kwa msingi wa utashi huu, wananchi wanakichagua kikundi cha watu ambao wanawaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili iwaongoze kwa niaba yao.  Kwa hivyo hakuna nchi yeyote hapa duniani ambayo haina serikali. Tofauti inayoweza kujitokeza ni namna serikali hiyo inavyoundwa katika misingi ipi? Na inatekeleza vipi kanuni na taratibu zake? Je kuna uwazi katika shughuli zake? Viongozi wanabebe dhamana ya watu katika utendaji wao na wawajibikaje kwa wananchi ambao ndio waliowaweka ofisini; na viongozi wanatakiwa wawajibike na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Siasa kama siasa sio mchezo mchafu;siasa inageuka kuwa mchezo mchafu pale tu serilali ambayo imekabidhiwa dhamana na wananchi inaanza kwenda kinyume na utaratibu na kanuni sahihi,  na kuto fuata   maadili ya uongozi (code of conduct) ndipo tafsiri ya siasa inaanza kugeuka na kuwa mchezo mchafu. 
                                                                        Amin Dada



Misingi ya siasa chafu imechochewa sana na mwanasalsafa Machiavelli  ambaye aliandika katika maandishi yeke kuhusu viongozi na madaraka; kitabu chake kinawanufaisha sana viongozi katika kuimarisha  nafasi zao za uongozi, amewafundisha viongozi namna ya kuwa waongo (liar), wakatili, wanafiki,  kuwa na uchu wa mali, na hata ikibidi kuua ili kupata madaraka na kuudumisha adhima yao ya kuendelea kunyonya na kujitajirisha. mwongozo huu wa Machiavelli unatumiwa sana na watawala wa mabavu (dictators), kutoka nchi mbalimbali ambao waliongoza au wanaongoza nchi zao kwa manufaa binafsi na sio kuwaletea maendeleo wananchi bali huwajengea hofu na kuwasababishia wananchi wao maisha magumu, watawala kama; Idd Amin Dada, Mabuto, na kadhalika. Katika mlengo huu hakuna kuwajibishana, kinachofanyika hapa wananchi ni kusikiliza na kutii tu



                                                                                        Mabutu                                                                                

Uchafu wa siasa ni pale tunapoilinganisha siasa kama wapiganaji katika mchezo wa mieleka ule ambao hauna kanuni yeyote ili ushinde, unaweza kumchezee au kumpiga au kumwangusha mpinzani wako kwa namna yeyote ile uwezayo ili mradi tu wewe uwe mshindi; hapa hakuna  kanuni yeyote inayohitajika refarii yuko pale kutangaza mshindi tu kwani hana kanuni yeyote ambayo anafuata; hapo ndipo tafsiri ya mchezo mchafu inapoanza.je nini kazi ya wanasheria wetu? Utetezi au uonevu? Tatizo la mchezo huu ukiuanza huwezi kuuacha. Ushauri kama huuwezi kamwe usiucheze waache wanaouweza waucheze,  watu wenye kiburi na wasiojali utu hata mara moja. Na ukiamua kuucheza kamwe usiuache au usiwasaliti wenzako ukifanya hivyo safari yako yakuendelea kufurahia maisha ya siasa yataishia kaburini.


Je siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata kiongozi wa juu wa    nchi anapokiuka maadili ya uongozi? mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.



                                                                                    Nixon
                                                                   
Siasa sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneykevu na wenye huruma ya kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi nyingine?


Tukumbuke kwa wale ambao wamesoma kitabu cha sharkespear  nini alikifanya Macbeth kwa kusababisha umwagaji wa damu ambao ulikuwa hauna sababu kwa sababu tu ya  siasa  za ubinafsi na hatimaye kutekeleza mwonekano wa siasa kuwa mchezo mchafu ambao mwisho wa siku ulimgeukia mwenyewe na kuuwawa. Tatizo la uchafu wa siasa pengine huanzia kwa serikali kuona kuwa ofisi zao ndio biashara yao hivyo hata ile mishahara ambayo wamewekewa kisheria haiwatoshi na huanza kujiingiza katiak rushwa, mikataba mibovu ambayo inawapa masilahi wao binafsi, na kuwaongezea nguvu ya kipesa na uwezo wa kuongoza kwa masilahi ya watu wachache.

Katika nchi zetu ambazo umasikini umekidhiri, tatizo la kukosekana kwa ajira, kupeana kazi na vyeo kwa kufuata undugu na urafiki na sio sifa za elimu, kuwanunua watu kwa kuwapa zawadi wakati wa kampeni na hatimaye wakati wa upigaji wa kura, kwa misingi hiyo sio rahisi baada ya uchaguzi kwa wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Siasa taalumu nzuri sana na muhimu kwa jamii ikiwa itawapata viungozi wazuri na waungwana ambao wamewaeka wananchi mbele ya maendeleo yao, lakini siasa ikiwapata viongozi wabovu wala rushwa nchi imekwisha na wanyonge hawana chao ndipo hapo siasa inapokuwa ni mchezo mchafu. Kwa msingi huu ni kuwa siasa sio mchezo mchafu ni mchafu tu ikipata watu wala rushwa  na sio waaminifu, walafi wa madaraka,

Ni mchezo mchafu tu kama utaratibu wote wa uchaguzi haukwenda vizuri na matokeo yake baada ya hapo ni chuki binafsi baina ya vyama na hiyo mwisho wa siku itamaanisha kuwa chama tawala na  chama cha upinzani ni maadui na hakuna wa umuhimu wa chama kingine kuwapo, vyama vya siasa katika nchi vinaweza kuiongoza kwa kupokezana ni kama huko Marekani wakati wananchi wanapoona kuwa nchi iko amani yao ina mashaka wanakipigia Republican lakini wakiona uchumi wao unayumba wanakipigia Democratic;

Tukumbuke maneno ya Raisi JF Kennedy wa Marekani alivyosema” hakuna mtu ambaye atanishawishi mimi kufanya kitu ambacho nafikiri sio kwa masilahi ya nchi yangu, kama wewe au mtu mwingine anafikiri kuwa ndiye, basi huyo ni Mwendawazimu” Hii ndio tofauti ya kiongozi ambaye kwake siasa ni mchezo mzuri kwa masilahi ya wananchi wake na taifa lake, ambaye ni mkweli mwadilifu na ambaye anaweza kutoa maamuzi mazito kwa faida ya nchi yake, LAKINI pale tunapokosa maadili ya uiongozi tunakaribisha sana  urafiki, undugu na kugeuza ofisi zetu ambazo zimewekwa kwa masilahi ya Taifa kuwa sehemu za biashara na kuwakaribisha zaidi wenye fedha kututawala kwa kutoa mwongozo nini kifanyike hapo ndipo tunabadilisha tafsiri sahii ya siasa kuwa mchezo mchafu. Pengine bora hata kiongozi ambaye ni mbabe wa maendeleo ya taifa ambaye anapinga uzembe na hana rafiki wala ndugu ndugu yake ni maendeleo ya nchi yake. Je tunao viongozi wa namna hii hasa barani Afrika. tumkumbuke Mzee wetu, Mandela Nyerere na wengine wa namna kama yao

                                                                                         Mandela
                                                                                
Nukuu:


Politics is the gentle art of getting votes from the poor and campaign funds from the rich, by promising to protect each from the other.
Oscar Ameringer



Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason.
Author Unknown



Blessed are the young, for they shall inherit the National Debt."
Herbert Hoover



Richard Nixon is a no good, lying bastard. He can lie out of both sides of his mouth at the same time, and if he ever caught himself telling the truth, he'd lie just to keep his hand in."
Harry S. Truman.


No comments:

Post a Comment