Mwalimu Julius Nyerere
Shekhe Abeid Karume
Rais Yoweri Museveni wa Uganda
---
Na Mtuwa Salira,EANA
Arusha, Juni 12,2013
(EANA)
Rais Yoweri Museveni wa Uganda (pichani juu) amewaelezea viongozi waanzilishi wa
taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Shekhe Abeid Karume kuwa walikuwa
viongozi wenye muono wa hali juu katika Afrika Mashariki walioacha ubinafsi wa
mamlaka ya nchi zao na kuunganisha watu wao kwa lengo la kuwa na umoja imara.
''Viongozi hao
wanastahili kutambuliwa kwa maamuzi yao ya busara ya kuunganisha Tanganyika na
Zanzibar kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,'' Rais Museveni aliwaambia
wajumbe wa semina ya mahusiano ya wabunge mjini Entebe, Uganda mwishoni mwa
wiki.
Hatua hiyo ya
kishujaa na ya kupongezwa haina budi kuigwa na nchi wananchama wa Jumuia ya
Afrika Mashariki (EAC), aliongeza, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki
(EANA) linaripoti.
Nyerere alistaafu urais
mwaka 1985 na kufariki mjini London Uingereza Oktoba 14, 1999 akiwa na umri wa
miaka 77. Shekhe Karume (67) aliuawa Aprili 1972 mjini Zanzibar.
Rais Muveni alikuwa
anahutubia semina ya siku mbili yenye kauli mbiu : ''Kukuza soko lenye misingi
ya watu wa Afrika Mashariki.''
''Huku ikiwa na idadi ya
watu milioni 140, Afrika Mashariki ina soko kubwa ambalo linaweza kuvutia kwa
urahisi wawekezaji ambao wanaweza kujenga viwanda katika kanda hii,'' Museveni
alitoa maoni yake juu ya kauli mbio hiyo, kwa mujibu wa gazeti la Monitor la
nchini Uganda.
Aliongeza: ''Ubaguzi
unaotokana na tofauti za kikabila na dini zinapingana na matakwa ya wote,
wazalishaji na wafanyabishara.''
Alitoa changamoto kwamba
kuunganishwa kwa Afrika Mashariki ilikuwa '' ni lazima kwa kuwa watu katika
kanda hiyo walikuwa tayari wameunganishwa kwa utamaduni na lugha zao.''
source: haki ngowi
No comments:
Post a Comment