- Ni kweli kwa sasa vyama vyetu vikuu CCM, CHADEMA na CUF vimeamua kuendelea kuona kuwa ni jambo la kawaida kwa damu ya wananchi wasio na hatia inaendelea kumwagika kwa sababu tu ya ushindani wa siasa?
- Je wanao kufa katika matukio haya ya vurugu ni viongozi au wananchi ambao hawana hatia?
- Kuna siri gani kubwa inayoendelea ndani ya vyama vya siasa kushabikia vurugu na sio amani
Kauli kama
- “CCM wamepanga njama ya kulipua bomu kwenye mkutano wa CHADEMA ili wananchi waogope kuhudhulia mikutano ya chadema”.
- “CHADEMA wamejilipua wenyewe ili kutafuta umaarufu na huruma ya wapiga kura pamoja na kuipaka matope serikali ya CCM pamoja na jeshi lake”.
- Nashindwa kuelewa je siasa ni sera au malumbano yanayoishia kuvunja amani?
Zitto Kabwe aliwahi kusema
kuwa “sisi kama watu ambao tumepewa wajibi na wananchi wa kuitunza nchi hii na
kuipeleka pamoja tumejikuta tukiingia katika kutoa kauli, maneno na
vitendo ambavyo ni “irresponsible” vinavyopelekea kugawanya nchi; na
yanayotokea sasa ni matumizi ya nyufa hizo.”
Kwa matukio haya ambayo
yameisha tokea na yanayoendelea kutokea; Leo hii ni Tanzania gani tunaijenga ni
Tanzania yenye mshikamamo wa kujenga
utaifa, utanzania ambao utakuwepo siku zote hata kama watanzania wote waliopo
sasa wata toweka.
Nafikir tatizo la viongozi
wa siasa huwa hawaoni utashi wa kuleta mazungumzo yenye tija kwa Taifa bali
wanachoona wao nini kifanyike ili kukifanya chama kishinde; lakini kama
tutaendelea kuleta vurugu ambazo zinasababisha vurugu na watu kuuwawa mwisho wa
siku hakutakuwa na chama na wananchi wa kuwaeleza hizi propaganda za kisiasa kwani tutakapo
ukaribisha ukimbizi ndani ya nchi yetu ndio utakuwa mwisho wa siasa hizi za
amani na matokeo yake yatakuwa ukimbizi. Hebu tuwaangalie jirani zetu ambao
nchi zao zilihusika katika vurugu na hatimaye vita za wenyewe kwa wenyewe
wameishia wapi?
Ni
chanzo cha vurugu na hatimaye umwagaji wa damu; mimi naona ni kauli za viongozi
wa vyama pale ambapo wanaweka busara nyuma na masilahi binafsi mbele; unaweza
kuwapima kwa kauli zao ndizo zinazoashiria vurugu inasikitisha sana.
Nakubaliana na kauli
ambayo iliwahi kutolewa na mwanazuoni mmoja aliyesema kuwa “Siasa zilizo
gubikwa na umamluki ndiyo zinazo yumbisha taifa kupitia propaganda ndani ya
vyama vya siasa.”
Taifa hili kwa miaka 50 ya
uhuru, tumeweza kuishi kama ndugu, kwa
amani na maelewano makubwa; kwa nini leo hali imebadilika ghafla je hii ndio
demokrasia tunayoipenda ya vurugu?
Mwandishi wa raia mwema
aliwahi kuandika kuwa “hakuna
chombo au taasisi inayoweza kuitisha Serikali iliyowekwa madarakani na wananchi”
kwa mtazamo wangu hata kama utakuwa huipendi kwa vile imewekwa na wananchi
walio wengi basi inatakiwa iheshimiwe tukiamua kuleta vurugu tujue kuwa mwisho
wa siku vurugu hizo zitamgusa kila mtu. Amani inatafutwa kwa muda mrefu, lakini
fujo hazina muda. LAKINI Kwa upande mwingine vyombo vya ulinzi na usalama lazima
vitumie busara zaidi katika kukabiri vurugu; ikiwezekana kwa vile wana mbinu
zote za kulinda amani ikiwezekana waepuke umwagaji wa damu pasipo na ulazima wa
kufanya hivyo;
Wananchi
tujiulize je kama taifa wananchi tumaini letu ni lini dhidi ya viongozi wetu wa
siasa? Jibu ni moja tu watupeleke kwenye nchi yenye neema na amani kwa watu
wote bila kujali itikadi, hali yao kiuchumi, kisasa, kidini .
Lakini
hivi sasa tunaona mbio za vyama vyetu vya siasa ni fikara ya kuwa madarakani, je
madaraka haya yana siri gani mpaka wako tayari kupoteza maisha ya wapiga kura
wao.
Niliwahi andika huko nyuma
kuwa wanasiasasa tukiwaendekeza sana wanaweza kutufanya tusiendelee;tukumbuke
kuwa maendeleo yetu kwanza yatatokana na sisi wenyewe, juhudi zetu na misimamo
yetu; tukiangalia kwa ujumla
wanasiasa wanpoteza muda mwingi katika
propaganda na sio kutuelimisha ili tuweze kujua kwa undani matatizo na mahitaji
yetu yanatokana na nini na tutaweza vipi kuyaondoa.
Wanasiasa wetu ndio wapiga
majungu namba moja; aaa siasa zetu zimejaa majungu, chuki tusipoangalia sisi
wananchi tutaendelea kuwa wajinga; tusifanye ujinga kuwa ni sehemu ya utamaduni
wa siasa za Tanzania
Kwa takibrani miaka kumi
sasa sioni dira katika siasa zetu zaidi ya vurugu; tufahamu kuwa Uongozi ni
uwezo wa kuota dira na kuhamasisha maono na matarajio yaliyoko mbele na
kuwafanya watu kusimamia na kuuboresha mfumo kwa moyo wao wote huku wakiamini
na kushiriki kuyafikia matumaini yao ya kufikia maono yanayotolewa na uongozi
kupitia mfumo uliowekwa.
Kiongozi tunaemtaka tunataka asimamie maono ya kule tunakotaka kwenda na hata kama ana maono yake basi kwa kipindi tunachompa dhamana awe na uwezo wa kuweka misingi ya kufuatilia maono ya kule tunakotaka kwenda.
Je viongozi wa sasa wana mbinu gani za Kujenga uchumi wa ndani, kukuza kipato cha watu wa hali ya chini na kuhakikisha huduma zote muhimu zinamfikia kila mtu hasa wale wananchi wa vijiji ambao ndio wapiga kura namba moja?
Vurugu za Mtwara, Dar es salaam Zanzibar Arusha Mbeya Mwanza na kadhalika ni
kipimo tosha kuwa bado tunahitaji wanasiasa wawajibikaji na ambao wako tayari kutumia muda wao mwingi
katika kuhubiri amani kwani bila amani kwa kweli hakuna kitu kinaitwa
maendeleo, tunawaomba wajipange vizuri na kuja na sera mbadala ambazo
zitawawezesha kujipanga vizuri kuliongoza taifa hili.
Wananchi tunatakiwa tuamke
na tusiwape nafasi wanasiasa kutufanya sisi kuwa daraja lao la wao kuweza kutimiza malengo yao
bila sisi kujitambua kwa haraka; matokeo yake ni sisi ambao ndio tunapigwa,
tunauwawa na tunaendelea kuwa masikini.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
No comments:
Post a Comment