WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 18, 2013

KASORO ZA SERIKALI YA MUUNGANO

 Waziri waNchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais  Mohd Aboud Mohd kulia akibadilishana mawazo na Waziri wa Afya Juma Duni Haji nje ya Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
Muwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohd Raza akisisitiza jambo kwa Naibu Waziri wa Thuwaiba Edington Kisasi wamwanzo kushoto na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir wa mwanzo kulia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar.
Muwakilishi wa Jimbo La Mji Mkongwe Ismail Jussa Ladhu wakwanza kushoto wakibadilishana mawazo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala bora Haji Omar Kheir katikati na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zanzibar Othman Masoud Othman katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi mbweni nje ya mji wa Zanzibar.Picha na Yussuf Simai-Habari Maelezo-Zanzibar
----
Na Khadija Khamis – Maelezo Zanzibar 17/06/2013
 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeeleza kuwa  kasoro zinazojitokeza katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania zinapaswa kuingizwa na kujadiliwa  katika mchakato wa Katiba unaoendelea.

 Hayo yalielezwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Muhammed Aboud Muhammed  katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, wakati akijibu suala la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi Saleh Nassour Juma  aliyetaka kujua vigenzo vya  uteuzi wa Waziri Mkuu unaofanywa na Rais na Zanzibar imetoa Mwaziri Wakuu wangapi tokea kuasisiwa Muungano.

 Alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ambayo hadi sasa ndio inayotuongoza haikueleza vigezo vya uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania bali imetoa mamlaka ya uteuzi huo kwa Rais, na tangu kuasisiwa kwa Muungano  hadi sasa Zanzibar imetoa  Waziri mkuu mmoja ambae ni Salim Ahmed Salim.

 Alifahamisha kuwa tangu kuasisiwa kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Zanzibar haijawahi kutoa Spika wala Naibu Spika isipokuwa imewahi kutoa Mwenyekiti wa Bunge Zubeir Ali Maulid katika kipindi cha mwaka 2005/2010.

 Hata hivyo Waziri Aboud alisema kuwa  nafasi bado ipo ya kuweza kueleza kero  zilizopo ambazo zinaonekana kwamba ni ukiukwaji wa Katiba ya Jamhuri ya Muuungano ya Tanzania.
 Alikiri kuwa ipo hati ya makubaliano na maridhiano ya kikatiba kwa nchi  zote mbili zilizokuwa huru na mamlaka yake kamili na pia si kweli kuwa Zanzibar haina wasomi .

 Waziri alieleza kuwa kero za Muungano bado zipo na ndio sababu moja wapo ya  kuanzisha mchakato wa katiba ili kuzitafutia ufumbuzi  kero hizo.

 Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamesema  kuwa wanavyojuwa  ni kua Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja kero zilizozopo zinafanywa kwa makusudi
 
source: Haki Ngowi

No comments:

Post a Comment