Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali, Gabriel Kivuyo (52) aliyelazwa Hospitali
ya Rufaa Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano
wa Chadema, mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu
wa Rais, jana Juni 17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali
majeruhi wa mlipuko huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru,
Selian na Mtakatifu Elizabeth.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali, mtoto aliyetambuliwa kwa jina moja la Fahad
(7) aliyelazwa katika chumba cha watu mahututi Hospitali ya Rufaa
Selian, baada ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano
wa Chadema,
mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni
17, alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko
huo waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu
Elizabeth.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akionyeshwa picha ya X-Ray, ya mmoja kati ya majeruhi waliolazwa
kwenye Hospitali ya Mount Meru, Joseph Anthony, mkazi wa Karoleni,
baada ya kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotokea wiki iliyopita
katika mkutano wa Chadema eneo la Soweto jijini Arusha. Imeelezwa kuwa
hadi jana Juni 17, 2013, wakati makamu alipowatembelea majeruhi hao watu watatu waliliripotiwa kufariki dunia.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimjulia hali, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Majengo
A, Sarah John (45) aliyelazwa Hospitali ya Mtakatifu Elizabeth, baada
ya kujeruhiwa na mlipuko wa bomu katika mkutano wa Chadema, mwishoni
mwa wiki iliyopita jijini Arusha. Makamu wa Rais, jana Juni 17,
alifanya ziara ya kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko huo
waliolazwa katika hospitali za Mount Meru, Selian na Mtakatifu
Elizabeth.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na wananchi wa jijini Arusha waliokusanyika nje
ya Hospitali ya Mount Meru jana, wakati Makamu alipokuwa na ziara ya
kuwatembelea kuwajulia hali majeruhi wa mlipuko wa Bomu uliotokea wiki
iliyopita katika mkutano wa Chadema jijini Arusha, ambapo jumla ya watu
70 walijeruhiwa na watatu walifariki dunia. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mwilongo.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment