Waandishi wa habari na wanaharakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Waandishi wa habari na wanaharakati wakisubiri kumpokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Umati wa waandishi wa habari pamoja na wanaharakati wakiwa katika mapokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri.
Baadhi ya wapiga picha wakiwa Uwanja wa Ndege wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom kibanda.
Waandishi wa habari na wanaharakati wakimsubiri kumpokea Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.
Mjumbe
wa Bodi wa Jukwaa la wahariri, Theophil Makunga akimlaki Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda alipowasili jana kwenye Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akitokea Afrika Kusini kwa
matibabu.
Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya New Habari 2006 Ltd, Absolom Kibanda, akiwasili
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere,jana mchana. Hapa
akiina na kuanza kulia baada ya kuonana na sura za watu wake wa karibu.
Kibanda akihojiwa na wanahabari baada ya kuwasili.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jana
Kibanda akiwasili jana.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda akitokwa na machozi muda mfupi baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Jana.Picha na Mdau Mroki Mroki na Muhidini Sufiani
---
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda
amerejea chini jana kutoka Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa na
kusisitiza kwamba hatanyamaza kuzungumzia janga la kushambuliwa kwake.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,
Kibanda alisema asingependa kuona jambo hilo linamtokea mwandishi
mwingine wa habari.
Kibanda, ambaye pia ni Mhariri Mtendaji
wa Kampuni
ya New Habari (2006) Ltd, alikuwa akitibiwa huko baada ya kushambuliwa
na kuumizwa vibaya na watu wasiofahamika usiku wa Machi 5, mwaka
huu.Alisema kutokana na hali hiyo, waandishi wanapaswa kuwa na
mshikamano ili kuhakikisha matukio ya aina hiyo hayajirudii.
“Waandishi wana nafasi kubwa ya kuliondoa taifa
katika hali hii. Waendelee kuandika na kuelimisha wananchi ili nao
wasaidie kuzuia ukatili wa aina hii. Hatuwezi kuishi katika nchi ambayo
watu wanafanyiwa ukatili mkubwa kiasi hiki halafu wanaachwa hivihivi,”
alisema Kibanda.
SOURCE: HAKI NGOWI
No comments:
Post a Comment