Mahakama ya kimataifa imeamua kuwa
Naibu wa rais wa Kenya ambaye pia ni mshukiwa wa ghasia za baada ya
uchaguzi Kenya, William Ruto, awepo mahakamani Hague wakati kesi yake
ikisikilizwa.
Hasa mahakama inamtaka Ruto kushiriki
baadhi ya vikao muhimu katika mahakama hiyo wakati kesi yake itakapokuwa
ikisikilizwa kuanzia mwezi Septemba mwaka huu.
Bwana Ruto alikuwa ameiomba mahakama imruhusu ashiriki vikao hivyo kwa njia ya video kwenye mtandao wa Internet.
Mahakama imesema kuwa imemruhsu kutohudhuria vikao vingine kutokana na majukumu ya wadhifa wake.
Aidha Ruto alikanusha madai kuwa
alihusika katika ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007
ambapo mamia waliuawa na maelfu kuachwa bila makao baada ya kufukuzwa
makwao kufuatia vita vya kikabila.
Alishtakiwa na Rais Uhuru Kenyatta . Wawili hao walikuwa mahasimu wa kisiasa wakati wa uchaguzi miaka sita iliyopita.
Watu 1,200 walifariki na wengine laki
tano kuachwa bila makao katika vita ambavyo nusura vitumbukize nchi kwa
mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.
Mahakama ya ICC ilisema kuwa Ruto
atastahili kuhudhuria ufunguzi wa kesi yake pamoja na kikao cha mwisho
ambapo wahusika wa kesi watatoa kauli yao ya mwisho kabla ya uamuzi
kutolewa.
Pia atatakiwa kuhudhuria kikao ambapo jaji watatoa uamuzi katika kesi hiyo na siku ya kutolewa kwa hukumu ikiwa.
Mapema mwezi huu majaji katika
mahakama ya ICC, walikubali ombi la mawakili wa Ruto, kuakhirisha tarehe
ya kuanza kwa kesi dhidi yake ili wapate muda zaidi kujiandaa.
Mahakama pia imependekeza baadhi ya vikao vya kesi kusikilizwa nchini Kenya au Tanzania.
Tangazo lilijitokeza wiki chache baada
ya shinikizo kutoka kwa mataifa mengine ya kiafrika kuitaka mahakama
kufutilia mbali kesi dhidi ya Kenyatta na naibu wake Ruto.
Muungano wa Afrika ulisema kuwa
mahakama hiyo ina ubaguzi , tuhuma ambazo mwendesha mkuu wa mashtaka
katika mahakama hiyo alikanusha vikali.
Kesi dhidi ya rais Kenyatta inatarajiwa kuanza mwezi Julai.
Chanzo: bbcswahili
No comments:
Post a Comment