- KUTHUBUTU KWA VIONGOZI WETU KWA FAIDA YA WANANCHI
Kauli ya Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere "TUMUACHE
BADO AKUWE KIDOGO"
- Inatufundisha nini katika maendeleo ya taifa hili na viongozi ambao wanashindwa kuchukua uamuzi mara moja?
Ili tuweze kuendelea tunahitaji, pamoja na mambo
mengine yote swala la uongozi bora ni muhimu sana;
- Je viongozi wetu wako tayari kutoa maamuzi magumu kwa faida ya watanzania bila woga?
- Je Viongozi wetu bado wana Utamaduni wa kuogapa kuwajibika katika utoaji maamuzi kwa ajili ya kikundi fulani cha watu?
- Je Viongozi wetu wanaweza kuthubutu wakati wanapo takiwa kuwajibika kufanya mambo kwa kuangalia masilahi watanzania walio wengi hata kama yatawauzi na kuwakwera wachache wenye nguvu kama alivyokuwa akifanya Hayati Edward Moringe Sokoine?
Ni ukweli ambao haupingiki tukiangalia maelekezo ya
Wanafalsafa kuwa “kukaa kimya bila kutolea msimamo wako katika jambo fulani
maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila unao woga wa uwazi”. Na
kama viongozi wetu wana tabia hii ni kasoro kubwa; kama wahenga walivyotuambia
kuwa; “ngoja ngoja huumiza matumbo” tukingoja kufanya maamuzi tunaruhusu mawazo
mabaya toka kwa wamanchi wenye hasira pale ambapo kuna kuwa na tatizo.
- Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi sema "Hatuwezi tukawa kweli chama cha watu ikiwa hatujishughulishi na shida za kawaida za watu wetu".Tujiulize,Je viongozi tulionao ambao hawajishughulishi na shida zetu, wapo kwa ajili ya nani?
Ni ukweli kuwa “Hekima na busara huzaa mafanikio ya
uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa uongozi”
Mkongwe wa siasa Mahatma Ghandi,
aliwahi sema, “tufikirie kesho lakini tutende kwa ajili
ya leo.Hivyo mustakbali wa maisha yetu ya kesho yatategemea maamuzi sahihi ya
leo”.
Kama taifa nini tunahitaji?
- vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuheshimu demokrasia,
- Bunge lenye nguvu za hoja lisilitawaliwa na itikadi ya chama chochote! Viongozi wenye kufikiri kwa faida ya wananchi
- Viongozi wanaweza kusimamia sheria
Rais Mstaafu awa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliwahi
kutamka hili kuwa sisi watanzania ni wagumu wa kufikiri;
Swali langu hapa Mheshimiwa Mkapa kama Rais mtaafu nini
kilimsukuma yeye kutoa kauli hii?
Je ni ugumu wa kuyakabili matatizo ya maisha au kama
ndugu yetuJuvenalis Ngowi alivyowahi andika kuwa “Bahati mbaya ni kwamba
inawezekana uvivu wetu huu wa kusoma mambo magumu ndio unatuingiza “mkenge”
hata kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama mikataba. Inafika mahali tunaingia
mikataba ya kusikitisha kiasi cha kujiuliza hivi Mwenyezi Mungu aliwapa watu hao
ubongo wa nini? Maana uti wa mgongo pekee ungewatosha watu hao”.
- Ndipo tunapoukumbuka wosia wa baba wa taifa’ "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO"
Kama wananchi ambao ni sehemu ya kuwachagua hawa
viongozi nafikiri inatupasa tuondoe uvivu wetu wa kufikiri, tuamke sasa na
tuache itikadi za kuwaacha kuwapa madaraka mtu yeyote ambaye inaonekana wazi
kuwa bado hajapata utashi wa kuwa kiongozi bora wa kuwatumikia wananchi wake.
Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema - Ukiweka dodoki
kwenye maji safi litanyonya maji safi! Ukiliweka kwenye maji taka, kadhalika
litanyonya maji taka! Hapo ndipo tulipo! Uvivu wetu wa kufikiri pengine huleta
tatizo hili.
Sisi wadau wa kuwaweka madarakani tukisimamam imara
tutawafanya viongozi wetu kuweza kuthubutu au kuchukua maamuzi ambayo
watawasaidia na kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi na kulinda mali ya
umma kwa nguvu zote, bila kujali kitu chochote.
Nafikiri viongozi wetu wa sasa
wanatakiwa kufuata busara na umakini ambao marehemu Sokoine alikuwa nao
katika uongozi wake Kwanini, wasikubali kujifunza kwake waone matokeo yake?
Kama kuna maamuzi magumu inatakiwa wayafanye; mbona Sokoine alifanya na kuwafanya
wahujumu uchumi kuiogopa serikali na kusalimu amri?
Viongozi wetu wanaweza kwani tunaimani kuwa kwa sasa
wameshakuwa kifikra na utendaji unaozingatia misingi ya haki na kujali
maendeleo ya watanzania wanyonge ndio maana tumewakabidhi nchi;
Mungu libariki Taifa letu hasa katika mwaka huu qa 2013
kwa faida ya watanzania wote na sio kikundi kidogo cha watu ndani ya Taifa.
No comments:
Post a Comment