- KWA NINI BADO TUNAHITAJI ELIMU YA URAIA KWA WATANZANIA HASA WAISHIO VIJIJINI?
Demokrasia ina gharama
kubwa sana, ambayo pengine haionekani kwa haraka sana, kwa wananchi wa kawaida;
mfumo huu wa maisha unawahusisha wananchi katika kutekeleza sehemu hii kubwa ya
uchaguaji wa viongozi wao. Wananchi wengi hawapendi sana kujihusisha na swala
hili kwa vile wanaamini kuwa sio lazima sana wao wahusike wakati kuna wengine
wengi wanaweza fanya hivyo. Hivyo kila mmoja humsukumia mwenzake swala la
upigaji wa kura. Kuchagua kiongozi mzuri kwao hakuna maana yeyote hii kwa kweli inatokana na dhana ya kukata tamaa, kwani katika chaguzi nyingi ambazo wamefanya, bado hawajeona faida yeyote yeyote atakayechaguliwa ni kwa ajili yao ni sio kwa ajili yetu sisi walala hoi.
Leo nitazungumzia kwa nini
wananchi wengi hawajitokezi wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa
rais na wabunge wake: hebu tathimini tu kilichotokea katiak uchaguzi wa Raisi uliofanyika October
2010 kumekuwa na malalamiko ya wananchi kuto kujitokeza kwa wingi
katika upigaji wa kura, swali ni kwa nini?
Mtazamo wangu unalenga
zaidi katika ukosekanaji wa elimu ya uraia;
Kwa nini tunahitaji elimu
ya uraia?
Je hatuna kabisa mashirika au idara za serikali au za watu binafsi au
Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanajishughulisha na ufundishaji wa elimu
hiyo?
Kama tunayo kwa nini hakuna mabadiliko ya msingi ya uelewa huu kwa wananchi
kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijijini? Je idara na mashirika hayo yamelenga
zaidi katika ufundishaji wa elimu gani kwa ustawi wa demokrasia?
Lengo kubwa la elimu ya
uraia ni kuleta na kuimarisha uelewa wa wananchi katika kuzielewa na haki zao
zitokanazo na upigaji wa kura; Elimu ya uraia vile vile husaidia sana katika
kuondoa fikra tofauti ambazo zinaweza kuletwa na chama au vyama katika kujinadi
hasa wakati wa kampeni za uchaguzi, kama tu wananchi wameiva katika kuelewa
haki zao. Wananchi hawajui hata kama wao ndio wafanyanyi wa maamuzi makubwa
sana ya maendeleo yao;
Kwa nchi kama Tanzania kwa
hivi sana umasikini ndio umekuwa kielelezo cha kuwachagua viongozi, ukizingatia
kuwa kutokana na ugumu huo pesa utumika kununua kura, ambazo huwachagua
wawakilishi wa watanzania walio wengi ambao wanakuwa hawana sauti katika kujua
hatima ya maendeleo yao. Wananchi walio wengi hawana elimu kabisa ya uraia na
hawajui namna gani kura zao zina thamani kwa maendeleo ya nchi.
Kwa mfano
katika wananchi takribani karibu million 19 waliojiandikisha kupiga kura
ni ni pungufu ya nusu ndio waliopiga kura. Je hii inamaanisha nini?
Inaelekea kuwa elimu kama
inatolewa haitolewi kwa ukamilifu hasa kwa wananchi wa vijijini, ndio maana
hata leo katika nchi ya Tanzania bado kuna wananchi ambo wanafahamu fika kuwa
Mwalimu J. Nyerere bado ni rais wa Tanzania;
Je REDET wako wapi? Serikali na
mashirika yake pamoja na NGOS wako wapi katika kueleimisha hili?
Ifahamike kuwa
kuto kumpa mwananchi elimu ya uraia ni kumnyanyasa kifikra na kimaendeleo. Kwa
ufupi kukosekana kwa elimu ya uraia kumesababisha :
wananchi wasione umuhimu
wa kwenda kupiga kura kwa kujua kuwa kupiga kwao kura ama sivyo hakuwezi
kubadilisha chochote.
Wananchi hawajioni ni kama
wanaweza kudai haki yao kwa njia sahihi ya kupiga kura
Wakati umefika wa
kuwauliza wote wanaohusika kwa namna moja au nyingine kwa msaada tuko kwa wafadhili au kutoka katika serikali yetu kuwawamefanikiwa kwa kiasi gani?
kwani tunafahamu kuwa kwa elimu yeyote ambayo imetolewa au itatolewa kipimo cha ufanisi au
ubora wa kazi yao wanatathimini vipi?
tunaelewa kuwa kwa mwanafunzi kipimo cha elimu aliyepewa ni kuelewa
alichofundishwa, kufanya tathimini na hatimaye kuweza kufaulu
mitihani yake;
Je kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na utoaji wa elimu hii
kipimo chao ni nini kwa taifa?
Je wanaweza kuwapimaje wale wananchi hasa wa vijijini
ambao katika marejesho yao walionyesha kuwa wamepata elimu hiyo je ni kweli wameelewa au bado wanahitaji tena elimu zaidi na tukizingatia kuwa wananchi wengi wa vijijini kwa bahati mbaya ya mfumo wetu ni watu wenye "pengine" wanaviwango vidogo vya elimu na pengine hata Chini ya kiwango (below Basic) na pengine hawana elimu kabisa.
wananchi wengi ambao wanaishi mijini ni wale wengi wao wana elimu
ya kutosha kuhusu mada nzima ya haki zao na nani anawafaa kuwaongoza kwa maneno mengine wamebobea katika elimu ya uraia wanaijua nini wanataka na watapata vipi na hata wanaweza kutoa ushindani kwa wanasiasa wetu.
Bado tunasafari ndefu
lakini inahitaji umakini mkubwa sana; ambao unahitaji wananchi makini ambao
ndio wanaweza kutuletea viongozi makini, maendeleo yetu yataletwa na sisi
wenyewe na sio mtu mwingine yeyote Yule;
Tukumbuke kuwa kama hatutachukua hatua
ya haraka katika kuwaelimisha watu wetu kuhusu elimu ya uraia
tunaendelea kuwajaza wananchi wetu na ujinga hivyo na tutaendelea kuwajaza hofu
katika kufanya maamuzi, hivyo hakuna namna yeyote wataweza kumchagua mtu
sahihi kwa maendeleo ya Taifa letu.
tutaishi kulalamika kuhusu vitendo vya rushwa na uchakachuaji katika chaguzi zetu; wananchi hasa wa vijijini wataendelea kuchagua Chama na wagombea ambao watakuwa na uwezo wa fedha katika dhana nzima ya ulipaji wa fadhila kwa
vile ulinipa hiki name nakupa hiki.
Lakini kama elimu ya uraia itafundishwa vyema ni rada
ya kuongozea demokrasia katika nchi kwani huipeleka nchi katika njia sahihi kwa
faida ya taifa na sio tija binafsi wa wanjanja wachache.
Dr. Benson Bana Mwenyekiti wa REDET
Wananchi wazuri
ambao wanaelewa taarifa kuhusu mwelekeo wa serikali na siasa katika nchi yao
hawajezaliwa hivyo bali wamepikwa kutokana na elimu ya uraia ambayo ni kazi ya wataalamu wetu kwa kupitia misaada ya wafadhili na serikali yao kwa faida ya wananchi na sio kutumia mwanya huo kujitajirisha na kutotimiza wajibu wao wa kizalendo.
No comments:
Post a Comment