WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 17, 2012

Taarifa ya CUF kuhusu - Katiba Mpya; Hatima ya Muungano; Uozo wa CCM; Haki za Binadamu; Nishati ya Gesi; Operesheni Mchakamchaka



 

KIKAO CHA BARAZA KUU CUF-CHAMA CHA WANANCHI
17/12/2012-18/12/2012
UKUMBI WA SHABANI MLOO-MAKAO MAKUU CUF-BUGURUNI,DAR ES SAAM


TAARIFA YA KWA UMMA


Wajumbe waliohudhuria ni  50 kati ya 55 (wasiohudhuria:kwa udhuru)

KATIBA MPYA NA HATMA YA MUUNGANO

Mwanzo wa Nukuu wa haya Hotuba ya Ufunguzi Mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba  kwa wajumbe wa mkutano na waandishi wa habari:

“Tunakutana wakati nchi ikiwa katika mchakato wa akatiba mpya.Nasisi kama cha ma tutaatoa maoni kuhusu jambo hili la katiba kwa ni katiba yetu inamatatizo makubwa yanayoweza kuathiri muungano wetu.

Mfano serikali ya muungano inaweza kuchaguliwa na kujiita yenyewe Serikali ya muungano hata kama chama kilichochaguliwa hakijapata hata kula moja ya Wazanzibar ama kupata hata kura moja Tanganyika ama  bila mwakilishi mmoja Zanzibar.Kwa katiba ya sasa hili swala liunalowezekana kabisa.Tunaposikia wazanzibar wanakuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu maswala haya ya muungano  Lazima wasiwasi wao na maswala yao ni ya msingi.Kama kweli tunataka kuendeleza muungano wenye haki sawa kwa  wote ni lazima tupate katiba itakayoridhisha pande zote mbili za muungano.

Ni muhimu katika mambo yale mabayo ni machache tutakayokubaliana kwamba haya ndiyo ya muungano ,yale mengine yote pamoja na masuala ya mashirikano ya kiuchumi lazima serikali za nchi mbili Zanzibar na Tanzania ziweze kuwa na mamlaka kamili katika mambo yale yaliyomengi yanayokidhi mahitaji ya Wananchi katika pande mbili.Na nimuhimu tukawa wavumilivu katika kusikiliza hoja na tusiwe wepesi wa kutoa majina ya wale wanao kiri kwamba mfumo uliopo wa muungano haukidhi mahitaji ya Wananchi wa pande zote mbili za muungano.

Hivyo ni matuamaini yangu tume ya katiba ya Warioba itapokea maoni ya wananchi na hayaitachakachua  na kutuletea  katiba ambayo tayari  wanayo mfukoni na ikawa hii ya kukusanya maoni ikawa ni danganya toto,lakini wakaya tayari wamesahatufungia mgulai,wanakitu ambacho wanataka kukileta  bila kujua kwamba kunamaoni ya  Wananchi.

Chama cha CUF kinahitaji kuimarisha muungano.Sera ya chama cha CUF imekuwa ni sera ya serikali TATU lakini ni muhimu kutumia mfumo huu wa mchakato wa katiba lakini sio tu kufanya marekebesho ya Jamhuhuri ya Muungano lakini pia kurejea  Article of Union ama ule mkataba wa Muungano ulioainisha mambo 11 ya muungano na mambo mengine yaliyozungumzwa kuweza kuyatazama na kuona kama yanakitdhi mahitaji ya kisiasa,kiuchumi na kijamii ya hivi sasa.Hivyo wajumbe mna kazi kubwa ya kuweza kulijadili swala hili kwa uwazi katika hali ya kwamba sisi ni chama cha kidemokrasia bila kuwa na woga wowote katika kutoa hoja zako ilimradi tu unaijengea hoja,hoja unayoitoa.

MCHAKATO WA KATIBA MPYA

Vile vile katika huu mchakato wa kutoa maoni katika katiba muda tuliopewa ni miezi 18 kukamilisha zoezi.Wenzetu wa Kenya walianza mchakato wa katiba,mkutano wa Boma toka mwaka 1997 wamekuja kupata katiba mpya mwaka 2010 kwa hiyo ni kitu ambacho kinachukua muda kwa hiyo katika kutafuta katiba ambayo itakidhi mahitaji ni muhimu tusifanye papara,tusije tukaja na kitu ambacho badala ya kutujenga,kikatugawa zaidi kama watanzania.

Ni vizuri basi wakati ambapo huu mchakato wa kutafuta katiba unaendelea pawepo na mchakato mwingine wa kuhakikisha kwamba tunakuwa na tume huru ya uchaguzi,ni kweli kwamba tumehuru ya uchaguzi ni tume huru ya katiba,lakini tumehuru ya uchaguzi mambo ambayo  yanakidhi tumehuru ya uchaguzi yanajulikaa tusisubiri mpaka kukamilisha lasimu ya katiba kwamba mpaka ratiba imekamilishwa ikapigiwa kura ndio tukaanza utaratibu wa kutafuta tume huru ya uchaguzi.

Kwa sababu tumehuru ya uchaguzi ina mambo mengi ya kufanya ikiwa ni pamoja nakuandikisha wapiga kura na kuhakikisha kwamba tuna daftari safi la wapigakura ,kwa hiyo miongoni mwa mambo ambayo tutayajadili ni umuhimu wa tume huru ya uchaguzi iweze kuandaliwa mapema kwa sababu tumehuru  ya katiba ndiyo itakayopitisha rasimu yoyote ya katiba itakayopitishwa na baraza la kutunga sheria.Baraza la kutunga katiba litakuwa ni pamoja na wabunge pamoja na wawakilishi.Raisi atateua,sasa raisi katika kuteua kwake asitupelekee tukajikuta kwamba katika baraza la kutunga sheria tunabaraza la  CCM,ikawa katiba mbaya ikapelekwa kwa sababu imepitishwa na CCM bila kuwa na ridhaa ya wadau wengine,tutakuwa turudi kulekule kwenye katiba ya 1977 wakati tulipokuwa na ukiritimba wa Chama cha Mapinduzi.

Kwa hiyo ni muhimu rasis akatumia busara kwamba tayari CCM wako wengi  mno,kwa wale watakao teuliwa wateuliwe watu ambao  watokane na jamii kwa ujumla na si CCM ili kuwe na bara la kutunga sheria ambalo linajumujisha watu wote”Mwisho wa Nukuu

UOZO WA CCM KUELEKEA 2015

Mwenyekiti wa CUF Prof.Lipumba pia alielezea suala la Uozo ulipo ndani ya CCM na kueleza jinsi ilivyotafunwa na na rushwa na kwamba Mafisadi wakubwa wa CCM wamejiandaa kuandaa  kuleta seriukali nyingine ya Kifisadi kwani mtandao wa watu wenye pesa umefanikiwa kupitisha zaidi ya asilimia 75 ya wajumbe wa NEC na wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi .

”Kwa hiyo Taifa liweze kuelewa kwamba CCM hivi sasa imekamatwa shingani na wala rushwa na wenye fedha,kwamba CCM ni mtandao wa walarushwa na wenyefedha waliojiandaaa kuchukua uongozi 2015,Hivyo ni kazi ya baraza hili na watanzanzania kwa ujumla kuhakikisha kwamba tunajenga mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba kikundi hiki cha  mafisadi na walarushwa hakipati naafasi ya kuingi amdarakani 2015”Alisema Prof.Lipumba.

HAKI ZA BINADAMU

Akizungumzia suala la haki za Binadamu Prof.Lipumba alisistiza kila mtanzania apewe haki yake kwa nmujibu wa katiba ya nchi yetu hata kama serikali ama mtu hakubaliani na mtazamo wa mtu Fulani basi ni muhimu mtu huyo akapewa zile haki zake za msingi kama binadamu na raia wa Tanzania.Alitolea mfano wa Ponda na wengine walionyimwa  dhamana  na kusi yake kuendeshwa ndivyo sivyo  iulihali anastahili kupewa dhamana kama watu wengine.

NISHATI YA GESI

Kuhusu gesi Prof Lipumba alisemaa kwamba gesi iliyozinduliwa kusini mwa Tanzania lazima iweze kuwanuafaisha watanzania.Prof lipumba pia alisema kwa mujibu wa wataalamu kunauwezekano mkubwa maeneo hayo yaliyovumbuliwa Gesi kunuwezekano mkubwa wa kuwepo nishati ya Pertroli chini yake .

Prof Lipumba pia alkisikitishwa na jinsi ambavyo nchi ahaijajipanga kunaufaika na utajiri huu kwani mataifa ya jirani ndiyo hivi sasa wananufaika na gesi hii.Alitoa mfano wa huduma nyingi za helkopita katika migodi ya gesi inatoka Kenya.Alihoji kwa nini serikali isiwajengee uwezo Wajasiriamali wa kitanzania ili waweze kuto a huduma hii na fursa zingine nyingi zinazochukuliwa na nchi jirani.

OPARESHENI MCHAKAMCHAKA MPAKA 2015

Kuhusu oparesheni mchakamchaka Prof.Lipumba pia alielezea Jinsi Oparesheni mchakamcaha kuelekea 2015 ilivyofanikiwa na katika mikoa yote ya Dar es  salaam,Arusha ,Kagera,Kigoma na kwingine  walikopita ambapo CUF imepata wafuasi .Pia Opresheni machakamchaka imekuwa chachu kubwa ya mabadiliko na kiu kubwa ya mabadiliko ya kisiasa na uchumi kwa nchi yetu kwa watanzaia kila ilikopita.

Imetolewa na

Ofisi ya Habari na Mahusiano CUF

17/12/2012


Source: 
http://www.wavuti.com

No comments:

Post a Comment