MAKAMU mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Tanzania bara Bw Philip Mangula ametoa rai kwa vyama vya siasa nchini kuendelea kufanya mikutano yao kwa kunadi sera zao kwa amani na utulivu na kuacha tabia ya kuhatarisha amani ya Taifa kwa kuwatumia vijana .
Mangula alitoa rai hiyo jana katika viwanja vya CCM wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa Njombe mkoani hapa mara baada ya kuwasili mkoani kwake kwa mara ya kwanza baada ya kuchaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa CCM Taifa .
Alisema kuwa amani ambayo tunajivunia ipo siku itatoweka na iwapo vyama vya siasa vitaacha kufanya kazi yake ya kisiasa kwa kunadi sera za vyama vyao na kueneza chuki dhidi ya serikali kama ilivyo hivi sasa kwa baadhi ya vyama kuendesha siasa za chuki na kuwatumia vijana kuvuruga amani yetu.
Bila kuvitaja vyama hivyo Mangula aliwataka viongozi wote wa vyama vya siasa kuendelea kuendesha siasa safi kama kilivyochama cha mapinduzi na kuwataka vijana wa CCM kutoiga siasa za baadhi ya vyama vya upinzani siasa yenye lengo la kuvuruga amani ya Taifa.
" Nawaombeni sana vijana wa CCM kuendelea kuonyesha mfano kwa vijana wa vyama vya upinzani na kamwe msije iga siasa vya vyama vya upinzani siasa ya kufanya vurugu ..... hiyo ni siasa mbaya sana na itakuja kuliweka Taifa katika umwagaji damu"
Mangula alisema kuwa sehemu kubwa ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao wamekuwa wakichochoa vurugu wana paspoti mfukoni na mara baada ya kuona amani imetoweka wao hupanda ndege ni kukimbia mafichoni na kuwaacha watanzania na vijana ambao wametumika kuvuruga amani wakiendelea kupoteza maisha yao.
Mbali ya kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kutowatumia vijana hao katika kuvuruga amani pia aliwataka vijana kutokubali siasa chafu zenye chembe ya vurugu kwa watanzania.
Akielezea kuhusu msimamo wake ndani ya CCM alisema kuwa mbali ya kuwepo nje ya ulingo kwa kitambo kirefu ila kamwe hatafanya kazi hiyo kwa kulipa kisasi kwa mtu awaye yeyote na kuwa atahakikisha anafanya kazi kwa kuzingatia taratibu zote za chama na hatakurupuka katika utendaji wake
source: Francis Godwin blog
No comments:
Post a Comment