WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, December 4, 2012

TAARIFA YA KILICHOENDELEA KUHUSU KESI YA MWIGIZAJI LULU DEC 3 2012




Kesi ya mauaji ya marehemu Steven Kanumba inayomkabili movie star waTanzania Elizabeth Michael (Lulu) imeendelea kutajwa katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam huku suala la umri wa mshitakiwa huyo likiendelea kuwekwa kiporo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu AUGUSTINA MMBANDO, Wakili wa Serikali KENNETH SEKWAO amesema upelelezi bado haujakamilika na kwa sasa ipo katika hatua ya kutajwa.

Mapema baada ya LULU kufunguliwa mashitaka ya mauaji ya msanii mwenzake STEVEN KANUMBA April mwaka huu, mawakili wanaomtetea waliwasilisha hoja ya kupinga umri wa mshitakiwa huyo na kutaka achukuliwe kama mkosaji mtoto kutokana na umri wake kuwa chini ya miaka 18 hali iliyolazimu suala hilo kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania iliyoamua kulirejesha jambo hilo kwenye mahakama ya Kisutu.

Pamoja na kurejeshwa kwa suala hilo katika mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kumekuwa na ukimya wa muda sasa, kesi ya LULU imeahirishwa mpaka Disemba 17 mwaka huu ambapo itakwenda kwaajili ya kutajwa.

Picha kutoka( Millard ayo blog)

No comments:

Post a Comment