Tukiwa tumebakisha miaka takribani mitatu, taifa letu
liingie tena katika mchakato wa uchaguzi wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania na Uchaguzi wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar; nafikiri ni
wakati muuafaka sasa wa kuanza kufikiri viongozi wa namna gani wanahitajika
katika taifa letu hasa wakati huu ambapo nchi yetu ipo katika mawimbi ya
mabadiliko ya fikra hasa kutoka mabadiliko makubwa ya Katiba katika historia ya
Taifa letu.
Ni matarajio yetu kuwa uchaguzi wa mwaka 2015 pengine
utakuwa na historaia ya pekee; upekee wa uchaguzi huu ni matarajio ya wananchi
wengi kuwa uchaguzi huu utafanyika katika kipindi ambacho taifa litakuwa
limekwisha pata Katiba yake mpya;
swali ambalo tuanalojiuliza sasa ni je Katiba hiyo itakuwa imekizi matakwa ya Taifa ambalo linataka kusonga mbele kimaendeleo?
swali ambalo tuanalojiuliza sasa ni je Katiba hiyo itakuwa imekizi matakwa ya Taifa ambalo linataka kusonga mbele kimaendeleo?
Kama taifa litakuwa limefanikiwa kupata Katiba bora
basi hatuna budi tupate viongozi ambao kwa kweli nao watakuwa bora katika
kuongoza Taifa letu kuelekea kwenye maisha bora kwa kila mtanzania. Ni ukweli
ambao haupindiki kuwa Katiba bora ni msingi wa maendeleo ya nchi kwani ni
msaafa wa sheria na kanuni sahihi kufuatwa na itamlazimisha kiongozi kuongoza kwa uwajibikaji; kuonyesha uzalendo
na kuwa mfano bora kwa viongozi wengine.
Pengine katika msingi huu tutahitaji kiongozi ambaye anauelewa mpana wa kuielewa Katiba ili aweze kuisimamia kwa dhati kabisa; tutahitaji viongozi wenye UWEZO wa kufikiri kwa usahihi, kuamua kwa usahihi na kutenda kwa usahihi wakitambua dhamana ya uongozi ambao taifa linawapa. Kwa hivyo tutahitaji RAIS pamoja na mambo mengine awe na UWEZO kuongoza kwa usahihi.
Vile vile tunahitaji viongozi wajao katika serikali zetu mbili wawe ni watu wa WATU; viongozi ambao wataweza kuona matatizo ya wananchi wao ni yao na yanawakera wanawanyima usingizi, yana wafanya waongeze nguvu ya uwajibikaji wa kusimamia rasilimali za Taifa. Nasi kama wananchi tuwe na uwezo wa kuwapima kwa watakacho kifanya wakiwa madarakani.
Pengine tutahitaji kidogo aina ya viongozi wetu wawe
wakali japo sio sahihi katika nchi ya kidemokrasia kutumia msemo huu lakini wakati mwingine ile tuweze
kupiga hatua ya maendeleo tutahitaji viongozi wenye mawazo ya kidikteta ili tuweze kubadilisha kidogo maadili ya utendaji kwa Watanzania hasa viongozi wetu katika mawizara
na idara zake:Tunahitaji Maraisi katika
serikali zetu mbili ambao wanaweza kuwawajibisha
mara moja watendaji wake ambao wanashindwa kuwajibika, tuwapate viongozi ambao
wanaweka pembeni huruma na urafiki ambao hauna faida kwa Taifa;
Nafikiri itakuwa ni jambo la busara kama sisi kama
watanzania na wapiga kura tukiweza kuepuka tabia ya kuwachagua viongozi wetu
kwa Mazoea, Mkumbo na kwa kutumia Hisia na
mapenzi binafsi juu ya wagombea. Nafikiri umefika wakati tuwachagua viongozi
wetu kwa upeo wao wa kuona mambo mbalimbali nauwezo wao wa uongozi hapa nazungumzia
uzoefu wa kiongozi kabla ya kuchaguliwa kuwa rais je amefanikiwa kwa kiasi gani
katika idara ambayo amewahi kuongoza?
kama taifa tunafahamu kuwa taifa letu bado linaogelea sana katika tope nzito la matumizi mabaya ya rasilimali ya Taifa Rushwa na Ufisadi basi tunahitaji Rais ambaye analiona hili kuwa Lazima tukubali kuwa mabadiliko yoyote ya kisiasa, kijamii na kiuchumi yenye kulenga kuletea faida wananchi walio wengi hayawezi kufanikiwa bila ya kutokomeza rushwa na ufisadi. Kiongozi wetu aweze kuliona hili na kuwa tayari kupambana nalo akiamini kuwa Tanzania yetu tatizo la rushwa limeshaota mizizi:Watanzania wengi kwa mamilioni wamepoteza matumaini na hali zao za maisha lakini Maraisi wetu wapya watakuwa tayari kulitatua tatizo hili na kuwachukulia sheria wale wote ambao wamehusika katika uchafu huu,
Tunahitaji vile vile kiongozi ambaye ataweza kuyatekeleza kwa vitendo manemo haya
ya Mheshimiwa Yusuph Makamba “maendeleo
ya Watanzania yataletwa na wao wenyewe, kwa kufanya kazi. Watanzania wamekuwa
wavivu wa kufanya kazi na kwamba kila kitu wanategemea kitafanywa na serikali …
Watanzania wataendelea kulia umaskini kwa kuwa hatuna tabia ya kushirikiana na
kufanya kazi,”. Kauli hii
ni nzito kiongozi wetu anayetaka kuongoza taifa hili lazima awe kuwahamasisha wananchi bila kuogopa kwa kuwaeleza ukweli huu bila kuogopa kukosa kura katika kipindi kingine cha
uchaguzi.
Daima tunapofikiria kuwachagua viongozi wa juu wa Taifa letu tunayakumbuka maneno ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliwahi sema kuwa kazi ya urais ni ngumu na inahitaji busara na kuchukua maamuzi magumu, ili kuweza kutimiza haki wananchi wanyonge “ walala hoi ”; aliendelea kushauri kuwa “Ole wale wanaokimbilia Ikulu, wanakimbilia nini, Ikulu hakuna biashara ya kufanya, Ikulu ni mahali patakatifu na kama kuna mtu anadhani kuwa kukaa Ikulu ni raha basi angeniuliza mimi katika kipindi cha miaka 21 niliyokaa Ikulu nimefanya biashara gani,Ikulu ni mzigo mzito”
Mwandishi Nyenyembe aliwahi andika kuwa “Kwa maana
hiyo mtu anapoamua kuulilia urais,urais sio pambo la nchi,urais ni jalala,
urais ni chumba cha kuhifadhia maiti,urais ni njaa,urais ni magonjwa,urais ni
bakuli la kukingia machozi ya watu wanyonge wanaolia kila siku wakihitaji
msaada na kama hawapati anayetazamwa hapo ni rais”
Je katika hawa yupi unafikira anafaa kuongoza serikali ya Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania na Ile Ya Serikali
ya Mapinduzi ya Zanznibar ifikapo mwaka 2015: Na kwa sababu Gani?
Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed Shein
Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe
Mheshimiwa Edward Ngoyai Lowassa.
Dr. Wilbrod Slaa
Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe
Mheshimiwa Samuel John Sitta
Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro
Mheshimiwa JOHN SHIBUDA MAGALE
Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed
Mheshimiwa Dr. Anna Kajumulo Tibaijuka
mheshimiwa Dr. Mohamed Gharib Bilal
Professor Haruna Ibrahim LIPUMBA
Rev. Christopher Mtikila
Mheshimiwa January Makamba
Mheshimiwa Bernard Kamillius Membe
Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha
Mheshimiwa Seif Sharif Hamad
mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi
No comments:
Post a Comment