Na Abdi Suleiman Pemba 12/12/2012.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya
Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiznduzi, Dk Mwinyihaji Makame Mwadini,
amesema kuwa, yeye ni muumini wa mfumo wa Muungano uliopo na sio Muungano wa
mkataba kama baadhi ya wananchi wanavyotaka.
Alisema kuwa, katika hilo yeye
hamumunyi mdomo, wala hapati kigugumizi na anaamini mfumo uliopo hivi sasa wa
serikali mbili, ndio unaofaa kwa pande mbili za Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Bara na Visiwani Zanzibar.
Dk Mwinyihaji Makame
Mwadini, alitumia fursa hiyo, kueleza hayo, huko katika ukumbi wa Misali Sunset
Beach, Wesha Chake Chake Pemba, katika mkutano wa kikao cha tano cha
ushirikiano, baina ya Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serekali za mitaa
Zanzibar na wizara ya nchi ofisi ya waziri Mkuu tawala za mikoa na serikali za
mitaa Tanzania bara.
Alikiri kuwepo kwa kero za
Muungano ambapo, amesema kuwa zinafanyiwa ufumbuzi, na serikali zote mbili, na
wala sio kuwepo kwa serekali ya mkataba kamawananchi wanavyodai.
“Mimi ni muumini wa
Muungano wala hakuna Muungano wa mkataba kamabaadhi ya wananchi wanavyodai
katika sehemu mbali mbali”alisema Dk Mwinyihaji.
Alifahamisha kuwa, katika
kushinda goli, lazima wananchi wadumishe Muungano, kudumisha udugu na kupiga
vita adui ujinga na ukoloni mamboleo, sambamba na kuwataka wajumbe hao kusaidiana
katika kujenga Zanzibar yenye amani na utulivu.
Aliongeza kuwa, katika
kujenga nchi pamoja na kuendeleza elimu, mambo ya afya na huduma zote za
kijamii kwa ustawi wa wananchi wao kama ilivyo lengo la vikao hivyo,
ambavyo hujadili mada mbali mbali ambazo zitatoa mambo muhimu ambayo yatakayo
wasaidia wananchi wotepamoja na kujua changamoto zinazowakabili katika
ufanikishaji wa shuhuli zao.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serekali za mitaa Tanzania Bara
( ELIMU), Kassim Majaaliwa, alizitaka ofisi zote za bara na visiwani kulenga
kutoa huduma bora kwa wananchi, hususana katika suala zima la elimu kwa watoto.
Alisema kuwa umefika
wakati kwa wajumbe kuwa makini kuhakikisha wanatoa majibu mazuri, kama ililivyo
lengo la serekali zote mbaili kuwahudumia wananchi wake kikamilifu na
kuwatatulia kero zao.
“Niwajibu wetu
kuyatekeleza hayo kwa wananchi, kwani wananchi wanatarajia kuona matunda mazuri
kutoka katika kikao chetu hichi maalumu ambacho serikali nzima leo ipo hapa”alisema
Naibu waziri Majaliwa.
Alifahamisha kuwa,
kutokana na kuongezeka idadi ya watu, Rais Kikwete aliona ipo haja kwa kila
kijiji kuweka shule ya msingi li kweza kuwapatia elimu watoto na kuwajengea
mfumo mzima wamustakbali wa maisha yao ya baadae.
Naye Naibu Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Aggrey Mwanri, amesema kuwa, ziara
hizozitawasaidia katika kudumisha Muungano, kwa kujenga umoja, amani na upendo
kwa viongozi wa serikali na wananchi kwa ujumla.
Aliwataka wajumbe wa
mkutano huo, kujenga umoja na mshikamano ambao utakaoweza kuwapatia malengo
ambayo yatakayo weza kuwaletea ushindi katika kazi zao za baadae za kuwahudumia
wananchi
Imewekwa na MAPARA
No comments:
Post a Comment