WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, December 19, 2012

Neno La Leo: Kitendawili Cha Embe Dodo Na Tunakokwenda..



Ndugu zangu, 

  Jana alasiri pale Bagamoyo nilisimama kununua embe dodo. Akina mama wale wakarimu walinipokea kama mwenzao. Bei ya dodo niliyotajiwa ilinifanya pia nitafakari sana, niingiwe na huzuni pia. 

Maana, ni ukweli, kuwa mama yule anaanza kuzitafuta dodo zinakotoka, kisha anazipanga pale chini mchangani. Bei ya dodo kubwa kabisa ni shilingi mia sita! 

Nilinunua dodo saba. Na hesabu ya dodo saba ikampa tabu sana mama yule. Akaniomba nimsaidie hesabu ya haraka. Nikamwambia ni shilingi 4,200. Kwenye noti ya elfu tano niliyompa alihitaji kunirudishia shilingi mia nane. Nikamwambia aitunze chenji hiyo. 

Akashukuru , lakini, wakati akinifungia dodo zangu akaniongeza dodo mbili! Hivyo, kimsingi ameniongeza dodo za thamnani ya 1200! Hivyo, ile mia nane niliyomwachia haina faida kwake. Unafanyaje? 

  Njiani niliwaza juu ya tunakokwenda kama nchi.Tujiulize; hivi rasilimali zetu za nchi ikiwamo madini, gesi na mafuta tunayoambiwa tunayo kwa wingi yatamsaidia vipi mama yule wa Bagamoyo mwuza embe dodo ambaye yumkini hajui kusoma, kuandika na kuhesabu? 

Na idadi yao inazidi kuongezeka. Takwimu zinasema; asilimia 39 ya Watanzania milioni 45 hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu. Na hawa wanawaririthisha nini watoto wao?

  Kila kizazi na Jukumu Lake; Tafakari,Chukua Jukumu La Kizazi Chako.... Na hilo Ni Neno La Leo. 

Maggid Mjengwa,

No comments:

Post a Comment