Dk Willibrod Slaa
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemuagiza Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Godbless Lema wakati atakapokwenda Bungeni, kufufua hoja kuhusu Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kulidanga Bunge Febuari 10 mwaka huu.Dk Slaa alitoa agizo hilo jana makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na wafuasi walioandamana wakishangilia Lema kurejeshewa ubunge wake jana na Mahakama ya Rufaa.
Dk Slaa alisema huu ni wakati wa Lema kwenda kufufua hoja ya kwamba Waziri Mkuu alilidanganya Bunge kwani tayari udhibitisho wa jambo hilo ulikuwepo.
“Nakuagiza sasa Lema utakapo kwenda Bungeni uende ukambane Waziri Mkuu kwa kulidanganya Bunge kwani Spika wa bunge alisema hoja hiyo imefungwa kwa sababu ya wewe kutokuwepo bungeni,” alisema Slaa.
Waziri Mkuu Pinda akijibu swali bungeni aliseme chanzo cha vurugu zilizosababisha vifo mjini Arusha ni ni uamuzi wa madiwani wa Chadema kutokubali kushindwa katika uchaguzi wa jiji hilo.
Pinda alitoa kauli hiyo Febuari 10 mwaka huu wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe aliyetaka kujua msimamo wa Serikali kuhusu mauaji ya raia yaliyofanywa na Polisi wakati wa vurugu zilizotokea Arusha.
Kutokana na majibu hayo, Lema kabla ya ubunge wake kutenguliwa na mahakama, aliomba kupewa mwongozo wa spika akidai kwamba Pinda alikuwa amelidanganya Bunge.
Spika wa Bunge Anne Makinda hajawahi kutoa mwongozo kuhusu suala hilo na aliwahi kusema kuwa suala hilo limefungwa kwani aliyeuliza hayupo tena bungeni.
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment