NDIE MSANII ALIYEKUWA
KIOO CHA JAMII KWA KUIMBA UKWELI HATA KAMA ULIKUWA HAUPENDEZI WENGI;
“Kifupi alinipa taswira
ya mtu aliyeshajijenga; aliyechangia muziki wetu na kutukuza utamaduni wa Bongo
ingawa hakuzaliwa hapa. Miaka yote alinisisitizia kuwa yeye ni Mwafrika na
kwamba popote alipoishi au kutembea barani palikuwa nyumbani kwake. Mungu
ailaze roho yake pema peponi” Fredy Macha
“Dk Remmy Ongala ni
miongoni mwa wanamuziki wachache sana wanaoheshimika, na kuenziwa kwa uwezo wao
mkubwa wa kufikiri, kubuni, kutoa burudani, nakuweka mikakati ya kuinua vipaji
vyao. Licha ya uwezo mkubwa wa kutunga na kuimba nyimbo zenye kufikirisha
(mantiki) Dk Remmy alikuwa muungwana na anaejua anachokifanya. Siku zote
alihakikisha anatengeneza muziki bora na si bora muziki kama wafanyavyo watu
wengi waliovamia tasnia ya muziki leo hii kwa lengo la kuchuma na kujipatia
umaarufu. Naam, jina la Ramadhani Mtoro Ongala halitafutika kamwe katika
historia ya wanamuziki nguli wa” Mwana dikala blog
NINI TUMEJIFUNZA TOKA KWA HAYATI REMMY ONGALA
aka DOCTOR?
Ni takibrani miaka miwili tangu mwenyezi Mungu alipomwita
mpendwa wetu Doctor Remmy Ongala katika
makao yake ya milele tarehe 13/12/2010.
Swali la msingi kwa nini kifo chake kiliwagusa wengi katika
masiaha yetu ya kila siku?
Majibu ya swali hili ni mengi sana kulingana na kila mtu na
mtazamo wake na kwa namna ambavyo alikuwa anamfahamu na Doctor Remmy kupitia
nyimbo zake na upendo wake kwa jamii iliyokuwa inamzunguka.
Kwa upande wangu nitazungumzia hasa URITHI gani
ambao Remmy ametuachia sisi kama wananchi wa Tanzania. Marehemu Remmy
ametuachia jambo moja kubwa la kuwa wakweli katika kutekeleza majukumu yetu
bila kumwogomba mtu yeyote Yule; ni Mwenyezi Mungu tu wa kuogopewa. Remmy
alikuwa mkweli, muungwana na mwelimishaji wa aina yake. Kama Fredy Macha alivyowahi
andika kuwa
“Kati ya 1988 hadi 1998 Remmy aliwaka dunia nzima. Alizunguka na
Super Matimila akiimba nyimbo zilizoangalia maisha ya walala hoi, wasifu wa
Mwalimu Nyerere (kwa kuondoa ukabila Tanzania) na kuchangia vita dhidi ya
Ukimwi (“Mambo kwa Soksi”)”.
Aliweza kukitumia kipaji chake katika kuwatetea wanyonge kwa
kupitia muziki wake, alikuwa anajitahidi sana kutoimba sana nyimbo za mapenzi
na badala yake kuimba zaidi nyimbo zilizokuwa zinagusa na kueleza matatizo ya
wanyonge watu wa kipato cha chini, ambao hawana sauti ambayo wakiitumia inaweza
kuwasaidia kutatua mataizo yao.
Aliwahi kusema huko nyuma katika kazi zake kuwa kuwa dunia hii ni sawa na gereza hasa kwa wanyonge ambao hawana uwezo wa
kuyafurahia maisha kwa vile hawana uwezo; hivyo wao ni wakuamuriwa tu nini
wafanye ni sawa na wafungwa. Mafanikio ya wanyonge lazima yatokane na furaha ya
matajiri ambao furaha yao ndio nafuu ya wanyonge na hasira yao ni kiyama kwa
wanyonge.
Doctor Remmy kwa kweli Alifanikiwa sana kueleza ukweli wa maisha
ya wanyonge kama umasikini, tatizo la ukimwi na namna ya kujikinga na
maambukizo, ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu, rushwa mapenzi na
uvumilivu kwa kupitia muziki wake; ndio maana alikuwa na wapenzi wengi sana wa
muziki wake hata ulikuwa ukitembelea kumbi za alipokuwa anatumbuiza daima
zilikuwa zinawapenzi wengi wakifurahia muziki na kupata ujembe muruwa kabisa.
Nakumbuka sana ule wimbo wake wa Mambo kwa soksi ambao
ulikuwa unahamasisha sana watu watumie kondom katika swala la mapenzi ili
kujikinga na maambukizo ya ukimwi; wimbo huu ulionekana kupingana na maadili
kwa wakati huu ya jamii ya kitanzania; lakini ukweli Doctor Remmy alikuwa
miongoni mwa elimishaji wa kwanza kabisa wa ngono salama kwa jamii.
Aliitumia sanaa yake kuwa kweli ni kioo cha jamii katika kutatua
tatizo. Hatukuwa tayari kuukubali ukweli huu, tukitumia kigezo ujumbe huu
ulikuwa umewasilishwa kunyume na utamaduni wetu. Bila kuogopa ukweli na akijua
kuwa jamii bado iko kwenye giza na serikali zetu zilikuwa bado hazifanya jazi
ya kutosha katika kuwaelimisha wananchi wake madhara ya ukimwi; lakini ujumbe
huu wa Remmy aliuweka bayana.
Je leo hii Jamii yetu inaelimishwa vipi matumizi ya kondumu? Sio
kama alivyokuwa akielimisha mwanamuziki Remmy? Ujumbe wa picha au wa maigizo
unaifikia jamii kiharaka na umakini mkubwa:
Tukubali au tukatae myonge myongee lakini haki yake mpe Remmy
alikuwa ameona mbali na alikuwa anawaonyesha wanyonge haki hiyo ya gharama
nafuu kwa usalama wa maisha yao;
Yako mengi ya kusema la msingi tu muziki ambao ulikuwa ukipigwa
na kutungwa na Doctor Remmy ulikuwa na hisia kali za kuelimisha jamii yetu kulingana
na mazingira; tutamkumbuka sana kupitia nyimbo zake: tutamkosa kwa sababu
hatutapata tena mashairi na na uimbaji wa hisia kwama wake;
Mwenyezi
Mungu amempa Baraka za maisha yake kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia kwa
kumuwezesha kutumia muda wake wa kutosha kabla ya kifo chake kumwimbia yeye; na
kwa kulisoma neno lake kwa utulivu zaidi na kwa makini mpaka pale alipowita
kwake katika mapumziko ya milele;
Kama wengi
walivyosema tumempenda sana mpendwa wetu Remmy lakini Mungu alimpenda zaidi;
Yeye alitoa na Yeye Ametwaa, jina lake na lihimidiwe milele. Tutaendelea kukumbuka
kwa mchango wako mkubwa ambao jamii hii haitaweza kusahau.
Dr.Remmy Ongala ameandika
Historia ambayo hakuna yeyote ambaye ataweza kuifuta na mchango wake utabaki
palepale; ni wakati mzuri kwa wasanii wengine kufuata nmna hi nzuri ya kuelimisha
jamii, na kuachana na kashfa zinazohusiha ukiukaji wa maadili na kubadilisha
kabisa mwonekano wa sanaa kutoka kioo cha jamii ambaka upotoshaji wa maadili;
Sanaa inatakiwa
ibaki kama kioo cha jamii. Tutaendelea kukuenzi daima
unaweza mwangalia Dr Remmy Ongala akiwajibika
Sehemu ya Mazishi Marehemu Dr. Remmy Ongola
turuendelea kukumbuka Mkongwe wa muziki Remmy RIP kwa kuwaimbia nakuwatafutia haki wanyonge
ReplyDelete