Jana club ya Simba
ilitangaza kumuuza mchezaji wake Mrisho Ngassa anaecheza Simba kwa mkopo kwa
El-mereikh ya Sudan ambapo taarifa iliyotolewa na Azam ilisema mchezaji huyo
ameuzwa kwa dola za kimarekani zaidi ya elfu hamsini na sasa anasubiri kumaliza
michuano ya Cecafa kisha aende Sudan kucheki mazingira.
Baada ya hiyo taarifa
kutoka Uongozi wa Simba umetoa tamko kupitia mwenyekiti Ismail Aden Rage kwenye
Sports Extra ya Clouds fm na kusema kilichofanywa na Azam Fc ni kitendo cha
kihuni.
Namkariri akisema “jambo
hili limetusikitisha sana, halikufata taratibu kanuni na sheria za mpira wa
miguu kwa sababu mchezaji Ngassa tulitangaziwa anauzwa na kwamba club
itakayotoa pesa nyingi ndio itamchukua hivyo sisi tukatoa milioni 25 na
tukasaini mkataba kwamba kwa hizo milioni 25 tutamtumia kwa mwaka mmoja baada
ya hapo hatutakua na haki nae labda kama tutakubaliana tena”
Ngassa alipoingia
mazoezini baada ya kujiunga na Simba na gari lake jipya.
Kwenye sentensi nyingine
Rage amesema “vilevile katika huo mwaka mmoja tulikubaliana tutamlipa mshahara
na marupurupu, sasa jambo la kusikitisha hawa ndugu zangu wameongea kwamba wametupa
kwa mkopo, ukishalipa pesa lile neno la mkopo halipo tena yule ni mchezaji wetu
halali kabisa na wala hawana mamlaka yoyote ya kumuuza bila idhini yetu, swala
hili tutalipigania mpaka dakika ya mwisho na tumewasiliana na TFF
wakatuhakikishia haiwezekani hata kidogo Azam wakafanya hivyo bila kufata
utaratibu”
Ameamplfy zaidi kwamba El
Mereikh walimfata Ngassa kabla ya kwenda Azam akawaambia yeye hawezi kuzungumza
chochote hivyo wakaenda kwa uongozi wa Simba ambao uliitaka timu hiyo ya Sudan
kuweka mezani dola laki mbili na nusu na sio laki moja na nusu waliyokua nayo.
Alipoulizwa kama kwenye
makubaliano ya mkataba na Azam kuna neno mkopo Aden Rage kwa ufupi jibu
alilotoa linamaanisha hakuna neno mkopo, anasema Ngassa hakutolewa kwa mkopo ni
kwamba alinunuliwa.
Source Millardy Ayo.com
They also provide far fewer selections for cash-strapped graduates struggling with payments,
ReplyDeletelike deferment, lengthy forbearance periods and income-based relief my website honestly, it's hard to think of an situation where it could be preferable to use a 3rd party
'help' you receive credit modification negotiated.