WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, December 31, 2012

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2013 KWA TAIFA LETU.


  • KUTHUBUTU KWA VIONGOZI WETU KWA FAIDA YA WANANCHI


 


Kauli ya Baba Wa Taifa Mwalimu Nyerere "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO"

  • Inatufundisha nini katika maendeleo ya taifa hili na viongozi ambao wanashindwa kuchukua uamuzi mara moja?


Ili tuweze kuendelea tunahitaji, pamoja na mambo mengine yote  swala la uongozi bora ni muhimu sana;

  • Je viongozi wetu wako tayari kutoa maamuzi magumu kwa faida ya watanzania bila woga?


  • Je Viongozi wetu bado wana Utamaduni wa kuogapa kuwajibika katika utoaji maamuzi kwa ajili ya kikundi fulani cha watu?


  • Je Viongozi wetu wanaweza kuthubutu wakati wanapo takiwa kuwajibika kufanya mambo kwa kuangalia masilahi watanzania walio wengi hata kama yatawauzi na kuwakwera wachache wenye nguvu kama alivyokuwa akifanya Hayati Edward Moringe Sokoine?


Ni ukweli ambao haupingiki tukiangalia maelekezo ya Wanafalsafa kuwa “kukaa kimya bila kutolea msimamo wako katika jambo fulani maana yake ni kwamba unakubali au unapinga ila unao woga wa uwazi”.  Na kama viongozi wetu wana tabia hii ni kasoro kubwa; kama wahenga walivyotuambia kuwa; “ngoja ngoja huumiza matumbo” tukingoja kufanya maamuzi tunaruhusu mawazo mabaya toka kwa wamanchi wenye hasira pale ambapo kuna kuwa na tatizo. 

  • Mwalimu J.K.Nyerere aliwahi sema  "Hatuwezi tukawa kweli chama cha watu ikiwa hatujishughulishi na shida za   kawaida za watu wetu".Tujiulize,Je viongozi tulionao ambao hawajishughulishi na shida zetu, wapo kwa ajili ya nani?


Ni ukweli kuwa “Hekima na busara huzaa mafanikio ya uongozi bora, lakini machafuko ni udhaifu wa uongozi”

Mkongwe wa siasa Mahatma Ghandi, aliwahi sema,   “tufikirie kesho lakini tutende kwa ajili ya leo.Hivyo mustakbali wa maisha yetu ya kesho yatategemea maamuzi sahihi ya leo”.
Kama taifa nini tunahitaji?

  • vyama vya siasa vyenye nguvu na vyenye kuheshimu demokrasia,

  • Bunge lenye nguvu za hoja lisilitawaliwa na itikadi ya chama chochote! Viongozi wenye kufikiri kwa faida ya wananchi


  • Viongozi wanaweza kusimamia sheria


Rais Mstaafu awa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa aliwahi kutamka hili kuwa sisi watanzania ni wagumu wa kufikiri;

Swali langu hapa Mheshimiwa Mkapa kama Rais mtaafu nini kilimsukuma yeye kutoa kauli hii?

Je ni ugumu wa kuyakabili matatizo ya maisha au kama ndugu yetuJuvenalis Ngowi alivyowahi andika kuwa “Bahati mbaya ni kwamba inawezekana uvivu wetu huu wa kusoma mambo magumu ndio unatuingiza “mkenge” hata kwenye mambo muhimu ya kitaifa kama mikataba. Inafika mahali tunaingia mikataba ya kusikitisha kiasi cha kujiuliza hivi Mwenyezi Mungu aliwapa watu hao ubongo wa nini? Maana uti wa mgongo pekee ungewatosha watu hao”.

  • Ndipo tunapoukumbuka wosia wa baba wa taifa’ "TUMUACHE BADO AKUWE KIDOGO" 


Kama wananchi ambao ni sehemu ya kuwachagua hawa viongozi nafikiri inatupasa tuondoe uvivu wetu wa kufikiri, tuamke sasa na tuache itikadi za kuwaacha kuwapa madaraka mtu yeyote ambaye inaonekana wazi kuwa bado hajapata utashi wa kuwa kiongozi bora wa kuwatumikia wananchi wake.

Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kusema - Ukiweka dodoki kwenye maji safi litanyonya maji safi! Ukiliweka kwenye maji taka, kadhalika litanyonya maji taka! Hapo ndipo tulipo! Uvivu wetu wa kufikiri pengine huleta tatizo hili.

Sisi wadau wa kuwaweka madarakani tukisimamam imara tutawafanya viongozi wetu kuweza kuthubutu au kuchukua maamuzi ambayo watawasaidia na kuwaletea maendeleo ya haraka wananchi na kulinda  mali ya umma kwa nguvu zote, bila kujali kitu chochote. 

 Nafikiri viongozi wetu wa sasa  wanatakiwa kufuata busara na umakini ambao marehemu Sokoine alikuwa nao katika uongozi wake Kwanini, wasikubali kujifunza kwake waone matokeo yake? Kama kuna maamuzi magumu inatakiwa wayafanye; mbona Sokoine alifanya na kuwafanya wahujumu uchumi kuiogopa serikali na kusalimu amri?

Viongozi wetu wanaweza kwani tunaimani kuwa kwa sasa wameshakuwa kifikra na utendaji unaozingatia misingi ya haki na kujali maendeleo ya watanzania wanyonge ndio maana tumewakabidhi nchi;

Mungu libariki Taifa letu hasa katika mwaka huu qa 2013 kwa faida ya watanzania wote na sio kikundi kidogo cha watu ndani ya Taifa.

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi Tanzania.


Picture
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waliohudhuria uzinduzi wa matokea ya awali ya sense ya watu na mazi Mjini Dar es Salaam
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar


Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ina idadi ya watu Milioni 44,929,002 kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya watu na Makazi iliyofanyika mwezi Agosti mwaka huu wa 2012.

Matokeo hayo yanaonyesha ongezeko la idadi ya watu Nchini Tanzania lililofikia watu Milioni 33,000,000 ikilinganishwa na lile la sensa ya watu la Milioni 12,313,054 baada ya Uhuru .

Akitangaza matokeo ya awali ya sensa ya idadi ya watu katika viwanja vya Mnazi Mmoja Mjini Dar es salaam Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alisema matokeo hayo yanaifanya Tanzania bara kuwa na Idadi ya Watu Milioni 43,625,434 wakati Zanzibar ina watu Milioni 1,303,568.

Rais Kikwete alifahamisha kwamba takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania inakadiriwa kufikia watu zaidi ya Milioni 51,000,000 ifikapo mwaka 2016 kiwango kisichokidhi mahitaji halisi ya uchumi na mipango mengine.

Dkt. Kikwete alitahadharisha kwamba idadi ya watu imekuwa kwa kiwango kikubwa na ongezeko lijalo linaweza kuwa mzigo mkubwa kwa Taifa ambapo alishauri kuwepo kwa mikakati katika kipindi cha miaka minne ijayo ili kukabiliana na ongezeko hilo.

Alizishauri familia kuzingatia zaidi umuhimu wa suala la kuwa na uzazi wa mpango kwa lengo la kuwawezesha wazazi kuwa na uwezo na mbinu za kuzihudumia familia zao.

Rais Kikwete aliupongeza Umma, Washirika wa Maendeleo pamoja na Viongozi wa nyadhifa tofauti kwa juhudi zao zilizopelekea kufanikisha zoezi ya sense ya watu na makazi na kuviomba vyombo vya habari vilivyotoa mchango mkubwa katika zoezi hilo kuendelea kuelimisha ummamatumizi bora ya Takwimu za sense kwa kudumisha ustawi wa Jamii.

Akimkaribisha Mgeni rasmi katika uzinduzi huo wa awali wa matokeo ya sense ya watu na makazi Mwenyekiti wa Kamati kuu ya Taifa ya Sensa ambae pia ni Waziri Mkuu Mh. Mizengo Peter Pinda alisema asilimia 90% ya gharama za zoezi zima la sense limesimamiwa na Serikali yenyewe.

Mh. Pinda alisema Kiwango hicho kimepindukia asilimia 20% ya gharama za sensa ikilinganishwa na Sensa ya mwaka 2002 ambapo zaidi ya asilimia 70% zilitumika katika zoezi hilo.

Akitoa salamu wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 mwenyekiti Mwenza wa kamati kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu Tanzania Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema matokea ya sense yatakuwa na maana katika Taifa pale Taarifa zake zitakapotumika kikamilifu katika kupanga maendeleo ya Nchi.

Balozi Seif aliwaomba washirika mbali mbali zikiwemo Taasisi za Serikali, Sekta binafsi, washirika wa maendeleo na Wananchi kuzifuatilia takwimu za sense kwa kuzitumia katika kupanga mipango ya maendeleo katika maeneo yao ya kazi.
Alisema hatua hiyo itasaidia kufanikisha malengo ya mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini Tanzania (MKUKUTA) na mpango wa kukukuza uchumi na kupunguza umaskini Zanzibar (MKUZA).

Mwenyekiti huyo mwenza wa Kamati Kuu ya Sensa Tanzania Balozi Seif amewashukuru Viongozi wote wa juu, kati, Wananchi pamoja na washirika wa maendeleo kwa kuitikia wito wa serikali zote mbili wa kuwataka washiriki katikamzoezi la sensa ya mwaka 2012.

Naye kwa upande wake mwakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa hapa Nchini Bibi Maryam Khan alisema Taasisi za Umoja huo zitaendelea kusaidia kitaaluma na uwezeshaji katika kuona Mataifa wanachama yanafanikiwa katika utekelezaji wa Mipango yao ya Maendeleo.

Bibi Maryam Khan alisema sensa ndio msingi muhimu inayotoa mwanga wa mipango ya maendeleo kwa kuimarisha miundo mbinu na kuipongeza Tanzania kwa juhudi zake za kujiletea maendeleo kwa kutambua umuhimu wa kujua idadi ya watu wake.

Mapema Kamishna wa Sensa Tanzania Hajat Amina Mrisho alisema watendaji wa kamati ya sensa watahakikisha machapisho yote ya sensa yatatolewa na kuchapishwa kwa lugha ya Kiswahili na Kiingereza.

Hajat Amina ameelezea faraja yake kutokana na watendaji wake kutimiza ahadi ya kutangaza matokeo ya sensa kama ilivyojipanga na inajivunia ufanisi mkubwa iliyoupata katika zoezi zima la sense ya watu na makazi ya mwaka 2012.

“ Katika kipindi kifupi tumeweza kutoa matokeo ya awali ya sense ambapo inaonyesha umahiri mzuri walionao watendaji wa sense. Uzoefu wa Kitaifa na Kimataifa mara nyingi unaonyesha kuchelewa kwa matokeo ya takwimu za Sensa”. Alifafanua Hajat Amina Mrisho.

---
via ZanziNews blog
Picture
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba leo Desemba 31, 2012 wakati wa kupiga picha baada ya kuzindua matokeo ya sensa ya watun na makazi katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. (PICHA: IKULU)


Source: http://www.wavuti.com

Urais 2015: Chadema sasa vipande viwili



SIKU moja baada ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kumtangaza Dk Willibrod Slaa kuwa ndiye mgombea wa urais mwaka 2015 kwa tiketi ya chama hicho, makada wa chama hicho wamegawanyika baadhi wakimponda na wengine kumuunga mkono.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, baadhi ya makada wa chama hicho walisema mwenyekiti wao amekosea kumtangaza mgombea kabla ya wakati, huku wanaomuunga mkono wakisema hajakosea kwa sababu hatua hiyo itasaidia kuondoa makundi ndani ya chama hicho.
Juzi, Mbowe akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Karatu mkoani Arusha, alisema Katibu Mkuu wa Chadema Dk Willibrod Slaa atapewa fursa ya kuwania tena urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2015, huku mwenyewe akijiweka kando kuwania nafasi hiyo
Hata hivyo, Dk Slaa alipoulizwa iwapo ana nia ya kuwania nafasi hiyo alihoji: “Kwani mwaka 2010 nilijitangaza mwenyewe,? Iwapo wanachama wa Chadema watanipendekeza nitafikiria kufanya hivyo.” Mwasisi wa chama hicho Edwin Mtei, Wajumbe wa Kamati Kuu; Profesa Mwesiga Baregu na Dk Kitila Mkumbo, Naibu Katibu Mkuu Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Bavicha John Heche na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa maoni yanayopingana kuhusu kauli hiyo ya Mbowe.
Wanaounga mkono
Mtei alisema anaunga mkono kauli ya Mbowe akisema kiongozi huyo hajakosea kumtangaza Dk Slaa kuwania urais mwaka 2015.
“Ninaunga mkono Dk Slaa kuwania tena nafasi ya urais mwaka 2015. Mwenyekiti amemtangaza baada ya kupata baraka ya vikao vya chama,” alisema Mtei.
Ingawa Mtei hakuwa tayari kusema ni kikao gani kilichopitisha jina la Dk Slaa kuwania nafasi hiyo, alisisitiza: “Kuna vikao vya Kamati Kuu vimefanyika hivi karibuni, vinaweza kuwa vimefanya uamuzi huo. Mwenyekiti hawezi kuzungumza jambo bila baraka za vikao vya chama.”
Hata hivyo, kauli hiyo ya Mtei inapingana na ile aliyoitoa Oktoba 6, mwaka huu baada ya Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini kutangaza kutogombea tena ubunge badala yake kusema anataka kugombea urais katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Mtei alisema hatua ya Zitto kutangaza kuwania urais mapema kungesababisha  mzozo na mpasuko  ndani ya chama hicho.
Mtei alisema amekuwa akimshauri Zitto mara kwa mara kuhusu hatua yake hiyo akimtaka kuwaunganisha wana Chadema na siyo kuwagawa au kuwavuruga.
“Hakuna shida kuonyesha hisia, lakini unatengeneza mzozo mkubwa sana ukitangaza sasa. Mimi nimeshamshauri sana Zitto, ahakikishe anakiunganisha chama na siyo kukigawa wala kukivuruga.”
Alisema mbunge huyo kutangaza kutogombea tena ubunge na badala yake kujipanga kuwania urais mwaka 2015 kumekuja mapema mno na kuonya kuwa itaibua mzozo ndani ya Chadema.
Mtei ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu enzi za utawala wa Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba wakati mwafaka ukiwadia, Chadema kitaamua ni nani mwenye sifa za kugombea urais  huku akisema kina utaratibu wake wa kuwapata wagombea mbalimbali wa uongozi.
Hata hivyo, Zitto jana alikataa kuzungumzia suala hilo akisema: “Nimesikia hata mimi kwenye vyombo vya habari ila sina cha kuzungumza kuhusu hilo.”
Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha), John Heche alisema kauli hiyo Mbowe siyo yake binafsi, bali ni ya wananchi.

“Ni kauli na maoni ya Watanzania wanaomwamini Dk Slaa kuwa anaweza kumudu kuliongoza taifa hili kama walivyoonyesha kwa kumpigia kura nyingi kuliko mgombea yeyote wa upinzani katika nafasi ya urais (mwaka 2010),” alisema Heche.
Heche alisema ingawa ndani ya Chadema kuna viongozi wengi wenye uwezo wa kuliongoza taifa, nyota ya Dk Slaa bado inang’ara.
Msimamo wa Heche uliungwa mkono na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ambaye alisema ni sahihi Dk Slaa kugombea urais mwaka 2015.
Lema alisema katika historia ya chaguzi za vyama vingi nchini, hakuna mgombea wa upinzani aliyewahi kupata kura nyingi kama Dk Slaa mwaka 2010 akadai kwamba ndiyo maana hivi sasa CCM kinafanya kila njama kumdhoofisha.
Lema alisema hatua ya kumtangaza Dk Slaa kuwa mgombea wa urais mwaka 2015, itaondoa harakati za chinichini zilizokuwa zikifanywa na watu ndani na nje ya Chadema kuwagombanisha viongozi wakuu wa chama hicho, hasa Mbowe na Dk Slaa.
Wanaopinga
Wakati Mtei akieleza kuwa Mbowe amepata Baraka za chama, Profesa Baregu alisema kutangazwa kwa jina la Dk Slaa kuwania urais ni maoni binafsi ya mwenyekiti huyo.
“Hayo ni maoni yake, lakini vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuteua jina la mgombea urais na havijakaa,” alisema Profesa Baregu.
Alipoulizwa maoni yake  kuhusu sababu za Mbowe kumtangaza mgombea urais sasa kabla ya wakati, Profesa Baregu alisema: “Mbowe atakuwa amefanya hivyo kwa sababu watu wengi walikuwa wanadhani kwamba yeye pia anawania nafasi hiyo ya urais.”
“Hivyo ili kuweka mambo sawa ameamua kutangaza mapema kuwa hatawania urais na kwamba Dk Slaa ndiye anayefaa kuwania nafasi hiyo,” alisema.
Profesa Baregu alisema haoni tatizo kwa wanachama wa Chadema kutangaza nia mapema kwa sababu hiyo ni haki yao kwa mujibu wa katiba... “Hata kama watu wengi watatangaza nia ya kuwania urais, siyo jambo baya katika ujenzi wa demokrasia, lakini uamuzi wa mwisho ni wa vikao vya chama.”
Kauli ya Profesa Baregu kuhusu vikao iliungwa mkono na Dk Mkumbo ambaye alisema kwamba anachojua vikao vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho kuhusu uteuzi wa wagombea wa ngazi ya urais.
Dk Mkumbo alionyesha shaka kama kweli Mbowe alimtaja Dk Slaa kuwa ndiye atakayewania nafasi hiyo akisisitiza: “Ninachofahamu ni kwamba yeye ametangaza kuwa hatagombea nafasi hiyo.”
Mwananchi

CHADEMA tunaposigana tunampa nafasi adui CCM - Mbowe, Karatu


Akizungumzia mgogoro ndani ya chama hicho wilayani Karatu, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe aliyegeuka kuwa mpatanishi wa miamba ya kisiasa wilayani Karatu alisema mgogoro huo umewasikitisha wananchi wa wilayani hapo.


Miamba ya siasa iliyokuwa kwenye mgogoro huo ni Mbunge wa Karatu Israel Natse, Mbunge wa Viti Maalum Secilia Pareso, Mwenyekiti wa Halmashauri Lazaro Maasai na Jubileth Mnyenye, ambao walikumbatiana kama ishara ya kumaliza tofauti zao.

Katika mkutano huo Mbowe aliwaambia miamba hiyo kwamba, kitendo chao cha kutofautiana ndani ya chama kimesababisha wananchi kuendelea kuumia na kukosa imani na chama hicho.

“Leo nimekuja kuzungumzia mustakabali wa kisiasa wa Karatu, ninajua mnahofu sana kuhusu mustakabali wa chama chenu. Naomba niseme leo kwamba, chama ninachokiongoza ni chama cha watu chenye kufanya kazi za watu. CHADEMA si mali ya Dkt. Slaa, Mbowe wala mtu yeyote hiki ni mali ya Watanzania wenye uchungu na nchi yao. CHADEMA ni chama chenye kujenga matumaini kwa wananchi,” alisema Mbowe na kuongeza: “CHADEMA hatujengi chama cha kujenga wafalme ndani ya chama, hakuna kiongozi aliyepo juu ya chama, katiba ya chama ndio chombo kinachotuongoza makabila yote ndani ya chama.”

Akizungumzia uamuzi uliofanywa na Kamati Kuu jijini Dar es Salaam ya kuwasimamisha uongozi kwa muda viongozi wa Karatu, ili kupisha uchunguzi, Mbowe alisema baada ya kukaa na kuzungumza nao sasa ameridhika na kuwarejesha kazini viongozi wote.

Alisema kwa muda mrefu sasa chama hicho kimekuwa kikipigania mambo muhimu na ya msingi kwa wananchi hata hivyo katika utekelezaji huo bado wanaamini kwamba, ndani ya CHADEMA pia hakuna malaika wote ni binadamu.

“Kihistoria Karatu ni ngome ya CHADEMA, naomba niwaambie viongozi hampo juu ya chama, inapotokea mmekiumiza chama basi lazima tule sahani moja na nyinyi. Kamati Kuu kule Dar es Salaam tulifanya maamuzi magumu kwamba, hawa wanaume wanaomenyana hapa Karatu hatuwezi kuwavumilia waendelee kukiumiza chama.

“Kiongozi yeyote anayetoka nje ya mstari tuna mchinjia baharini. Naomba viongozi wangu muelewe hivyo ndani ya Chama hakuna aliyepo juu. Hawa tungewachinjia baharini, lakini kwa vile wameifanyia CHADEMA mambo mengi ndani ya Karatu na Arusha, hatuwezi kuwachinjia baharini lazima tuthamini mchango wao. Tumekaa siku tatu tunazungumza na hawa wanaume kwa kina. Napenda kuwatangazia wananchi wenzangu wa Karatu hawa Tembo waliokuwa wakipigana hapa wamewaumiza mpaka Punda milia na Nyati hapa Karatu. Wanachama, kamati mbalimbali na madiwani hapa waligawanyika pande mbili ndani ya chama. CHADEMA tunaposigana tunampa nafasi adui CCM,” alisema Mbowe.

Akiwarushia makombora viongozi hao, Mbowe aliwaambia kwamba kuchaguliwa kwao kuwa viongozi hakumaanishi kwamba Karatu nzima haikuwa na viongozi wanaofaa kuongoza kwa nafasi walizonazo.

“Ndugu wananchi, nimekaa kwa siku tatu hapa Karatu kuzungumzia tofauti hizi, sasa naomba niwaambie kwamba, tumeyamaliza na miamba hii ya kisiasa imekubaliana kufanya kazi pamoja. Sasa naomba niwasimamishe hapa wote ili wawaombe msamaha nyinyi wananchi, kwani waliwakosea sana. Juzi na jana tumekesha hapa kwa ajili ya kuhakikisha tunamaliza tofauti hizi. Sasa kwa mamlaka niliyopewa na Kamati Kuu naomba niwatangazie wananchi kwamba, naurejesha uongozi huu madarakani kama walivyokuwa awali,” alisema. 

Hata hivyo kabla ya kuwasimamisha viongozi hao Mbowe aliwataka watambue kwamba nafasi yao ya kuwa kwenye ofisi za umma, ni kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na kujitumikia wao na maisha yao, “Hawa jamaa wametusumbua sana, hata kama watakuwa na hoja za kweli. Nataka leo wazungumze mbele yenu ujinga wa migogoro basi tena Karatu,” alisema Mbowe.

Akianza kuzungumza mbele ya wananchi hao Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu, Lazaro Maasai aliwaeleza wananchi wa Karatu kwamba, ana msamehe Mnyenye Saba mara Sabini, “Kwa yale yote niliyomkosea namsamehe Saba mara Sabini. Lakini pia kwa wananchi wa Karatu nawaomba mnisamehe kwa kuwakosea na kuwaumiza,” alisema Maasai.

Kwa upande wake Mnyenye aliwaambia wananchi kwamba, hakuna tena uhasama ndani ya Chama hicho Karatu kwani sasa ametambua tofauti kidogo zimeleta madhara kwa wananchi wanaokipenda chama hicho.

“Nimewakwaza sana wananchi wa Karatu na viongozi wangu wa Chama pengine kwa kutojua au kufuatana taratibu za Chama. Hakuna tena uhasama kati yangu na Lazaro. Ninawaomba mkiona ninakwenda tofauti msingoje mpaka Mbowe atoke Dar es Salaam, nipo tayari kujishusha au kuondoka kwenye uongozi,” alisema Mnyenye.

Katika hatua nyingine Mbowe alitumia fursa hiyo pia kuwapatanisha katibu wa wilaya ya Karatu na Mwenyekiti wa wilaya ambao nao walikuwa hawaelewani kiutendaji. Kana kwamba hiyo haikuwa imetosha Mbowe aliwageukia tena Mbunge Natse na Pareso, ambao nao walipandishwa jukwaani kwa ajili ya kuwaomba msamaha wananchi kutokana na tofauti zao, “Nikiri mbele yenu hapa kwamba, nitamsaidia Mbunge Natse kwanza huyu ni sawa na baba yangu, mchungaji wangu,” alisema Mbunge Pareso.

Kwa upande wake, Mchungaji Natse aliwaomba msamaha wananchi waliokuwa wamefurika kwenye viwanja hivyo, kwa kuwaambia kwamba siku zote hupata tabu ya kusimama mbele ya wananchi hao kutokana na kura nyingi walizompatia.

Katika hatua nyingine uwanjani hapo, Mbowe aliongoza harambee ya ujenzi wa ofisi mpya za wilaya za chama hicho kwa kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wananchi pamoja na viongozi wa chama na wabunge.

Mbowe alisema kwamba, amesikitishwa na kitendo cha wilaya hiyo kuendelea kupangisha ofisi wakati ndio wilaya yenye mabadiliko makubwa ya mageuzi ndani ya nchi, “Nimewaambia hawa viongozi waliokuwa kwenye tofauti zao, wao ndio watakuwa wasimamizi wakubwa wa mradi huu na kwa kuanzia mimi nachangia Sh Milioni 10, Dkt. Slaa Sh Milioni 5, Nassari ametoa Sh Milioni 2,” alisema Mbowe.

Mara baada ya kumaliza kuzungumza Mbowe, viongozi waliokuwa katika mgogoro walianza kupitisha bakuli kwa wananchi kwa ajili ya kukusanya fedha hizo ili fedha hizo ziweze kuingizwa katika ujenzi.

---
Taarifa via gazeti la mtanzania


Sunday, December 30, 2012

RAIS KIKWETE AMJULIA HALI PADRI AMBROS MKENDA ALIYEPIGWA RISASI ZANZIBAR


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kufuatia kupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Padri Ambros Mkenda wa Kanisa Katoliki la Mpendae mjini Zanzibar anayeuguza majeraha katika taasisi ya mifupa ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (Moi) jijijini Dar es salaam leo Jumamosi Dsemba 29, 2012 kukupigwa risasi sehemu za mdomoni na watu wasiojulikana mapema wiki hii wakati akisubiri kufunguliwa geti la nyumbani kwake maeneo Kitomondo Mjini Zanzibar akiwa ndani ya gari aliyokuwa akiendesha akiwa pekee yake. Rais Kikwete amempa Padri Mkenda pole nyingi na kumuombea apate nafuu haraka. 
PICHA NA IKULU

Saturday, December 29, 2012

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Atembelea Makazi ya padri Ambrose Mkenda Paroko wa kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar




Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia gari ya Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda ambayo alikuwa akiendesha na kuvamiwa kwa risasi ya watu wasiojuilikana

 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akipata maelezo kutoka kwa Uongozi wa Skuli ya Francis Maria Tomondo ambapo Padre Ambrose Mkenda wa Paroko ya Parokia ya Mpendae alijeruhiwa kwa risasi hivi karibuni


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifuatana na Father Shayo wa Kanisa la Roman Catholic liliopo minara miwili baada kuwafariji na kutoa mkono wa pole kwa uongozi wa huo kufuatia kujeruhiwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Padre Ambrose Mkenda.
---
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alifika katika makazi ya padri Ambrose Mkenda wa Paroko wa parokia ya kanisa katoliki la Mpendae Zanzibar kuupa pole uongozi wa Kanisa hilo pamoja na Familia yake kufuatia ajali ya kupigwa risasi hivi karibuni na watu wasioujulikana. 


Tukio hilo la kusikitisha lililofanywa na watu wawili waliopakiana kwenye Vespa lilitokea langoni mwa Skuli ya Francis Maria iliyopo Tomondo Wilaya ya Magharibi ambapo ndio makaazi ya Padri Ambrose.



Balozi Seif akiufariji Uongozi huo alisema ni jambo baya na la kusikitisha lililofanywa na watu hao ambalo limetoa sura mbaya kwa Taifa na Serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi itaendelea kufanya uchunguzi wa tukio hilo na haitasita kuwachukuliwa hatua za kisheria watu watakaobainika kufanya uhalifu huo.


Alisema Serikali imesikitishwa na kulaani kitendo cha watu hao ambacho kinaashiria uvunjifu wa amani pamoja na kuwaweka wananachi katika hali ya wasi wasi usio wa lazima ndani ya harakati zao za kimaisha. 


Akitoa shukrani kwa niaba ya Uongozi na Familia ya Padre Ambrose Mkenda Kiongozi kutoka Kanisa la Roman Catholic Father Shayo aliiomba Serikali kuendelea kuimarisha ulinzi wa raia wema ili kupunguza hofu iliyotanda mioyoni mwao kutokana na matukio ya uvamizi.


Father Shayo alitahadharisha kwamba hulka mbaya iliyoanzishwa na baadhi ya watu kuwafundisha watoto wadogo tabia ya kukashifu watu wazima kwa sababu ya utofauti wa Kidini inawajengea maisha mabovu watoto hao. “ Watoto wadogo kufundishwa tabia ya kukashifu watu wengine tuelewe kwamba Taifa halitakuwa na muelekeo mwema wa jamii yake ya baadaye”. Alitahadharisha Father Shayo. 

  Na 
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar

source: Haki Ngowi blog

Zitto Kabwe: Utajiri Wa Gesi Asilia: Tuwasikilize Watanzania Wa Mtwara Na Lindi. Tusipuuze




Maandamano ya amani yaliyofanyika mjini Mtwara siku ya alhamis wiki hii yameibua hoja mbali mbali kutoka kwa viongozi, wananchi, vyombo vya habari na mjadala wa siku nzima kwenye mitandao ya kijamii hasa facebook, twitter na JamiiForums. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ameita waandamanaji wapuuzi na Waziri wa Nishati na Madini amewaita watu hatari na wahaini. CHADEMA tumetoa kauli kupitia kwa Waziri Kivuli wa Nishati na Madini kwamba udhaifu wa utendaji serikalini ndio chanzo cha maandamano haya.
Lakini kuna tatizo kubwa zaidi ambalo linaonekana siyo katika sekta hii tu bali pia katika sekta nyingine ambapo tunaona matokeo yake katika maisha ya watu wetu na naweza kusema ni dalili za kushindikana kwa sera za CCM. Sera hizi ndizo ambazo zimelifikisha taifa hili hadi hapa. Kama hadi wananchi wa Mtwara ambako kwa muda mrefu imekuwa ni ngombe ya CCM wanaanza kuhoji matokeo ya sera za chama tawala basi ni dalili kuwa Watanzania wamefungua macho yao na wanaona.
Wanaona katika nishati, wanaona katika utawala bora, wanaona katia elimu (kuanzia ya msingi hadi ya juu kabisa!), wanaona katika afya, wanaona katika utendaji wa jeshi la polisi wanaona katika madini. Sera za CCM zimeshindwa. Zimeshindwa kuinua maisha yao na zinaonekana kuendelea kushindwa.
Mtwara na Lindi wanataka nini?
Watu wa Mtwara wanataka gesi isiondoke Mtwara na badala yake viwanda na mitambo ijengwe Mtwara kisha kama ni umeme au mbolea isafirishwe kupelekwa sehemu nyingine ya nchi. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba Gesi yote na mazao yake vibaki Mtwara na Lindi. Wanasema umeme uzalishwe Mtwara usambazwe nchi nzima. Mbolea izalishwe Mtwara na kusambazwa nchi nzima. Wanataka Bandari ya Mtwara iboreshwe na kuhudumia mikoa ya Kusini. Watu wa Mtwara hawasemi kwamba mapato yote ya Gesi yatumike Mtwara tu la hasha.
Sio dhambi hata kidogo kwa watu wa Mtwara kudai masuala haya. Watu wa Mtwara wamefanya maandamano kwa amani kabisa bila kuharibu mali na kutoa maoni yao. Kwanini tuwasute na kuwasusubika kwa madai yao haya? Kwa nini tusiwasikilize? Kosa lao nini kudai viwanda ili wapate ajira? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ni mikoa masikini kabisa nchini? Tumesahau kuwa mikoa ya Lindi na Mtwara ilitumika kwa ukombozi wa kusini mwa Afrika kiasi cha kuwa katika hatari kabisa? Tumesahau ‘sacrifice’ ya watu wa Mtwara na Lindi dhidi ya usalama wa nchi yetu? Tumesahau kuwa Korosho imekuwa zao kubwa la biashara na linaloingiza mapato mengi sana ya Fedha za kigeni? Waziri Muhongo anasema Mtwara warudishe Fedha za Mkonge na Kahawa. Mbona hataji fedha za Korosho? Mwaka 2011 Korosho ilikuwa zao la pili kwa kuingiza fedha nyingi za kigeni baada ya Tumbaku.
Lakini tujiulize, watu wa Mtwara na Lindi walifadi fedha za Mkonge? Walifaidi fedha za Kahawa? Wamefaidi fedha zao za Korosho? Tumesahau hata Reli iliyoachwa na Mkoloni ya Nachingwea – Mtwara iling’olewa na Serikali huru ya Tanzania?
Tujiulize zaidi, hivi watu wa Nzega wamefaidika vipi na Mgodi wa Resolute pale Lusu? Mgodi umefungwa ukiwa umezalisha na kuuaza dhahabu ya thamani ya dola za marekani 3.3 bilioni. Hivi katika uhai wa mgodi huu Serikali Kuu imekusanya kodi kiasi gani? Halmashauri ya Wilaya ya Nzega imepata ushuru kiasi gani? Watu wa Mtwara wanayaona haya yaliyotokea Nzega na yanayotokea Tarime, Biharamulo, Kahama na Geita. Watu wa Mtwara wana Haki kuandamana kuzuia haya yaliyotokea wenzao yasiwatokee wao kwenye Gesi asilia.
Mtwara na Lindi wanakosea wapi?
Madai yao halali na mimi binafsi na chama changu tunayaunga mkono. Lakini kuna mahala lazima waelimishwe.
Watu wa Mtwara pia wanapaswa kuelewa kuwa juhudi zao zisiwatenganishe na Watanzania wengine kwani bado utajiri wa Taifa unafadisha kikundi cha Watanzania wachache sana. Watu wa Mtwara wanahitaji kuungana na watu wa Mara, watu wa Mwanza, watu wa Shinyanga na watu wa Kagera kudai utajiri wa nchi utumike kwa maendeleo ya watu badala ya kunufaisha kundi dogo la watu. Watu wa Mtwara wanapaswa kuunganisha nguvu na Watanzania wengine kuzuia uporaji wa rasilimali ya nchi dhidi ya kizazi kijacho. Watu wa Mtwara wasijitenge wakawa peke yao na Gesi yao. Nguvu ya mnyonge ni umoja.
Serikali isiyosikia
Serikali ina hoja kuhusu kujenga Bomba la Gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa gharama nafuu. Umeme unaotumiwa na asilimia 14 tu ya Watanzania. Kwa kuwa hii asilimia 14 ndio wenye sauti basi watu wa Mtwara wataonekana hawana hoja kabisa. Lakini Serikali imejiuliza mara mbilimbili kuhusu mradi huu wa Bomba? Tunaambiwa na Wataalamu kwamba kuna uwezekano mkubwa mwakani gesi asilia ya kiasi cha futi za ujazo trillioni 20 itakuwa imegunduliwa katika Kitalu namba 7( block 7) ambacho kipo mkoani Dar es Salaam katika Wilaya ya Temeke. Iwapo gesi nyingi hivi itakuwa hapa Dar karibu kabisa na mitambo ya kuzalisha umeme, mradi huu wa Bomba unaojengwa kwa trillioni za shilingi utakuwa na maana tena? Huu mkopo utakuwa na tija?
Serikali imewaambia watu wa Mtwara gharama za kuleta bomba Dar dhidi ya gharama za kujenga mtambo wa kuzalisha umeme Mtwara na kuusafirisha umeme kwenda maeneo mengine ya Tanzania? Serikali imeangalia faida ya kujenga gridi nyingine badala ya kuwa na gridi moja tu yenye kushikwa na bwawa la Mtera? Leo bwawa la Mtera lisipozalisha hata megawati moja hata Dar es Salaam izalishe megawati alfu kumi umeme hautakuwapo maana uti wa mgongo wa gridi ni Mtera! Kwa nini tusiwe na gridi nyingine yenye uti wa mgongo Lindi au Mtwara?
Tuwasikilize watu wa Mtwara
Watanzania sio mabwege tena. Kuwaita watu wa Mtwara ni wahaini, wapuuzi au watu hatari haisaidii kujenga Taifa moja lenye watu huru. Serikali na wadau wote wa sekta ya Gesi likiwemo Bunge washirikiane na watu wa Mtwara kuhusu miradi ya gesi asilia. Tuwe na Azimio la Mtwara, tamko la kuelekeza namna bora ya kutumia utajiri wetu wa Gesi bila kuathiri umoja wa Taifa letu.
Ujio wa Sera, Maono na Uongozi Mbadala
Sasa hivi wananchi wa Mtwara kama wananchi wa sehemu nyingine wanahitaji maono mbadala, uongozi mbadala, sera mbadala na mwelekeo mbadala wa kitaifa ambao utaangalia mahitaji yao, utazingatia raslimali zilizopo na utaunganisha utendaji wa sekta mbalimbali katika kutengeneza mfumo wa kiutawala na kiuchumi ambao utaliinua taifa zima.
Ni kwa sababu hiyo naamini chama changu ni jibu sahihi kwa matamanio na kiu ya wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine nchini. Ikumbukwe kuwa katika Ilani yetu ya Uchaguzi ya 2010 tulielewa haja ya kuangalia mikoa hii ya Kusini kwa namna ya pekee na kuipa mwelekeo wa kipekee katika sera.  Bado tuna makusudio hayo tunapoelekea 2015 na tukishika Dola wananchi wa Mtwara na sehemu nyingine zote zilizoachwa pembezoni mwa mafanikio wajue kuwa wamepata rafiki na mshirika wa karibu wa kushirikiana nao kuleta maendeleo.
Siyo katika suala la gesi tu bali katika nishati, maji, elimu, miundombinu, kilimo, ufugaji, uvuvi, utalii. Mtwara kama ilivyo mikoa mingine ina raslimali za kutosha kuweza kuwainua wananchi wake kimaisha, na zaidi ya yote kutoa mchango mkubwa wa kiuchumi. Hili ambalo ni kweli kwa Mtwara ni kweli kwa mikoa mingine kama Kigoma, Manyara, Katavi, Lindi n.k.

Lissu amkaanga Profesa Shivji



Fredy Azzah
HATUA ya mwanazuoni wa siku nyingi nchini, Profesa Issa Shivji kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani Tanzania iliyomrejeshea ubunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema imemtia matatani na baadhi ya watu wanasema gwiji huyo wa sheria “huenda amenukuliwa vibaya au hajasoma hukumu husika.”
Jana Wakili wa Lema, Tundu Lissu, alimkosoa Profesa Shivji pamoja na Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, Francis Stolla akisema wanasheria hao wamepotoka katika matamshi yao ya kupinga hukumu ya Mahakama ya Rufani.
Matamshi ya Shivji pia yaliiteka mijadala katika mitandao ya kijamii ya Jamii Forums, Mabadiliko na Facebook ambako wachangiaji  walikuwa wakivutana huku baadhi yao wakisema wazi kwamba msomi huyo amekosea huku wengine wakimtetea kwamba yuko sahihi.
Akizungumza na gazeti hili jana kutoka Songea mkoani Ruvuma, Lissu alipinga vikali hoja zilizotolewa na Profesa Shivji pamoja na Stolla, akisema kuwa hazina mashiko na zinaweza kutolewa tu na mtu ambaye hakufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.
Juzi Profesa Shivji na Stolla walinukuliwa wakiikosoa hukumu ya Mahakama ya Rufani, iliyomrejesha bungeni Lema wakisema hukumu hiyo iliyotolewa na majaji watatu Salum Massati, Bernard Luanda na kiongozi wao Nathalia Kimaro, inapingana na sheria.
Lissu katika maelezo yake alisema uamuzi wa mahakama katika kesi ya Lema umejenga upya msingi bora wa matumizi ya vyombo vya uamuzi, kwani kesi nyingi za kupinga matokeo ya ubunge, zimekuwa zikifunguliwa na watu ambao wamekuwa wakitumwa na vigogo wa kisiasa na watu wenye fedha.
Akizungumza na Mwananchi, Lissu alisema hoja hizo hazina mashiko na kuwa ile iliyotolewa na Profesa Shivji inatokana na msomi huyo kuzungumza kitaalamu bila kuangalia mazingira halisi ya siasa za Kitanzania.
Lissu alisema mahakama ya rufani haikupiga marufuku wapiga kura kufungua kesi za kupinga ila iliwataka tu kufanya hivyo pale haki zao zinapokiukwa.
“Kwanza siyo kweli kwamba mahakama imepiga marufuku wapiga kura kufungua kesi, ilisema watafanya hivyo pale ambapo haki zao zimevunjwa, haki zenyewe ni kupiga kura, kura zao kutohesabiwa ama suala jingine litakalomnyima kupiga kura, hizo ndiyo haki za mpiga kura,” alisema na kuongeza:
“Sasa mwalimu wangu, Profesa Shivji yeye anatazama tu kwa jicho la kitaalamu na kusema haki za binadamu zimekiukwa, kwa muda wanasiasa, matajiri na CCM wamekuwa wakiwatumia wananchi kuwapinga wabunge wa upinzani.”
Uchambuzi wa Lissu
Alitoa mfano akisema katika uchaguzi wa 1995, Dk Willibrod Slaa alishinda ubunge na watu wanaojiita wananchi walifungua kesi kupinga ushindi huo, mwaka 2000 wakampinga tena na hata 2005.
Alisema 1995 Makongoro Nyerere aliposhinda ubunge katika Jimbo la Arusha Mjini kupitia NCCR- Mageuzi, watu wanaojiita wananchi walifungua kesi ambayo matokeo yake yalikuwa mbunge huyo kupoteza kiti chake.
Lissu alisema 2005 aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Marehemu Chacha Wangwe alifunguliwa kesi na watu waliojiita wananchi ambao mwisho wake walishindwa.
“Hawa wananchi ambao wanafungua kesi zenye mawakili wanaolipwa mamilioni ya fedha ni watu ambao hata fedha za kununua viatu hawana,  hawa waliokuwa wakimpinga Marehemu Wangwe nikiwa mahakamani niliwauliza kama wanawajua mawakili waliokuwa wanawatetea, walikuwa hawawajui.
Nikawauliza kama wamewahi kufika Dar es Salaam wakasema hapana, sasa sijui waliwapataje wale mawakili,” alisema na kuongeza:
“Wote hawa  wanakuwa ni watu wanaotumiwa. Mwaka huu kati ya wabunge wote 25  Chadema tulioshinda, 14 tulifunguliwa kesi na kati ya hizi 12 zimefunguliwa na watu wanaojiita wananchi, hii ni kutumiwa,” alisema.
Alisema mara baada ya uchaguzi mwaka 2010 aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliandika waraka kuwataka makatibu wa chama hicho kufungua kesi kwa majimbo yote ambayo chama hicho kiliangushwa jambo alilosema ndilo liliwasukuma kuwatumia wananchi.
Kuhusu hoja kuwa mahakama hiyo ya rufani imeingilia kazi ya kutunga sheria badala ya kuzitafsiri na kuwa imepingana na sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Chediel Mgonja ya mwaka 1980, Lissu alisema hazina mashiko.
“Hiyo ni hoja ya kipuuzi. Hiyo sheria ya kuwa mwananchi yeyote ana haki ya kufungua kesi kuwa imetenguliwa na Mahakama ya Rufani, hata mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa sheria ukimuuliza atakwambia kuwa, amri ya Mahakama Kuu wala ya Mahakama ya Rufani yenyewe haiwezi kuizuia mahakama hiyo ya juu kabisa nchini kufanya uamuzi wake,” alisema.
Akizungumzia hoja ya Stolla kwamba mahakama iliibua jambo jipya la kuhoji kama wajibu rufani walikuwa wapiga kura ama la, alisema Rais wake huyo hana hoja, kwani wakili wa walalamikaji aliibua hoja kama hiyo na alipoulizwa na mmoja wa majaji kuwa “Hata sisi hatuwezi kulizungumzia suala hili, alishindwa kujibu akawa anajikanyaga tu,” alisema.
Aliongeza: “Kwenye rufaa ya kwanza mahakama inaruhusiwa kuibua chochote, sasa hizo ni hoja zinazotolewa na watu ambao marafiki zao wa CCM wameshindwa sasa wanavaa joho la utaalamu kutoa hoja kama hizi zisizo na mashiko.”
Shivji na Stolla
Profesa Shivji kwa upande wake alieleza kushangazwa na maelezo ya Mahakama ya Rufani kuwa mpiga kura hana haki ya kufungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi na kusema hiyo ni sawa na kutunga sheria mpya na si kutafsiri zilizopo.
“Sheria ya Bunge na Mahakama Kuu katika kesi ya Mgonja (Chediel ya mwaka 1980), vinampa haki mpiga kura kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo. Sijaona hoja nzito ya Mahakama ya kufuta haki hiyo ya mpiga kura,” alisema Profesa Shivji.
Kwa upande wake, Stolla alisema: “Nimesikiliza hata maoni ya wanasheria mbalimbali wakizungumzia kutopendezwa na tafsiri ya Mahakama ya Rufani kuhusu haki ya mpiga kura ‘ku-challenge’ (kupinga) matokeo ya uchaguzi mahakamani.
Aliongeza: “Katika uamuzi wa kisheria, inaonekana Mahakama imetunga sheria mpya na wengi tunajiuliza kama siyo, ni sababu gani nyingine inampa haki mpiga kura kupinga matokeo?”
Stolla alisema Sheria ya Bunge ya Uchaguzi ya tangu mwaka 1985, ambayo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2002, kabla ya kutungwa upya mwaka 2005, inampa haki mpiga kura kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani.

Kesi ya Lema
Lema alivuliwa ubunge na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aprili 5, mwaka huu kutokana na kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa CCM, Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel, wakipinga ushindi wake.
Walikuwa wakidai kuwa katika kampeni zake alikuwa akitumia lugha ya matusi, kejeli na ubaguzi wa kijinsia dhidi ya aliyekuwa mgombea wa wadhifa huo kwa tiketi ya CCM, Dk Batilda Buriani.

Mahakama Kuu katika hukumu yake iliyotolewa na Jaji Gabriel Rwakibarila ilimtia hatiani kwa kutumia lugha ya matusi na kutengua matokeo yaliyompa ushindi.

Hata hivyo, alikata rufaa Mahakama ya Rufani kupitia kwa mawakili wake, Method Kimomogoro na Tundu Lissu ambayo Desemba 21, mwaka huu ilimrejesha tena bungeni baada ya kukubali rufaa yake.

Katika uamuzi wake, Mahakama hiyo ilisema kwa kuwa kisheria hayo ni masilahi ya umma kufikishwa mahakamani chini ya Ibara ya 26 (2) ya Katiba na kwamba mlalamikaji anapaswa kuonyesha haki zake au masilahi ambayo yameingiliwa na athari alizozipata.

source: mwananchi

Thursday, December 27, 2012

MAGGID MJENGWA MWANDISHI BORA WA HABARI ZA JAMII WA MWAKA 2012



  • HII KULINGANA NA MAPITIO YALIYOFANYWA NA BLOG YA UKADIRIFU NA MUNGUPAMOJANASI.
Mwanazuoni mmoja aliwahi andika kuwa “I know Mjengwa personally and have always known him to be fair and honest when it comes to news reporting, never even shying from his sometimes very  opinionated columns released in the press”.

Kama umeshawahi kupata na kusoma makala mbalimbali za mwandishi Maggid mjengwa katika magazeti ya Raia Mwema, na Kwanzajamii  kwa kweli utakubaliana na mimi kuwa Ndugu Magid amekuwa ni mwandishi ambaye amesaidia sana kuelimisha jamii katika hoja mbali mbali za maendeleo hata pale hoja zake zilipokuwa zikipingwa na watu wengine lakini aliendelea kusimama katika ukweli kwa faida ya Jamii ya Tanzania na mwisho wa siku ukweli unabaki kuwa ukweli.
Makala zake zimetumiwa na blogs nyingi katika kuhabarisha jamii ya Tanzania waishia popote pale duniani.
Amekuwa ni mwandishi ambaye amekuwa akiandika na kujishughulisha sana na maisha ya jamii za kawaida na wakati na kukosoa utendaji wa serikali katika mazingira yeyote yale bila hata kuuma uma akiwa anasimamia ukweli.
Amekuwa anajitahidi sana kuelimisha jamii bila kusimamia upande wowote wa siasa hata kama anajijua ni mpenzi wa mwanasiasa au chama gani.
Hebu tuangalie baadhi tu ya nakuu zake ambazo zimetokana na kazi zake mbalimbali:

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI: TAFSIRI YA MAGGID MJENGWA ( MAKALA, RAIA MWEMA).

“Kijana, hatukuandika bei, maana, gharama ya ukweli mzima ni uhai wako. Je, uko tayari kulipa?” Kijana yule akatimua mbio. Nyuma aliacha vumbi. Hakuwa tayari kulipa gharama ya ukweli mzima. Yumkini ukweli utakaousema mwanadamu waweza usiwafurahishe wachache, walakini, ukawa wenye kuleta tija, furaha na matumaini kwa walio wengi. Mimi nitasena hapa ukweli wangu, kuwa Baraza jipya la mawaziri ni mabadiliko ya sura ya Baraza lakini si mabadiliko ya mfumo uliosababisha udhaifu wa kiutendaji ikiwamo ‘madudu’ yale tuliyoyaona bungeni hivi karibuni.”
“Ushauri kama huu unafundisha tu si wanasiasa hata jamii kuelewa kuwa hata kama kesho  CUF au CHADEMA wakiingia madarakani kwa mfumo huu huu, nao, kwa kiasi kikubwa, watafanya hivi hivi. Ndio maana ya kusisitiza, kuwa, tulilo nalo sasa ni tatizo la kimfumo ambalo ndiyo chimbuko la utendaji mbovu wa kuanzia mawaziri na walio chini yao. Ni mfumo unaomfanya waziri, awajibike zaidi kwa chama chake badala ya taifa kwa ujumla wake”.
Gulio la mafisadi makala ya Raia mwema/ Spika Makinda ‘amechemsha’ Raia Mwema 217
“Tulipo sasa ni kwa baadhi ya viongozi wetu kuigeuza nchi yetu kuwa gulio la mafisadi. Kwamba kila mwenye uwezo atafute mtaji. Awahi nafasi ya uongozi itakayomsaidia kuingia gulioni. Huko ni mahala pa kufanya biashara, si kuwatumikia wananchi. Kwa bahati mbaya, hata rasilimali zetu wanazipeleka gulioni. Ili kuinusuru nchi yetu, sote kwa pamoja. Bila kujali itikadi zetu za vyama, tuna lazima ya kulifunga gulio hili Sasa”.
Miaka 51 ya Uhuru na maneno ya Mkapa makala Raia Mwema 272
 “Kuwapo kwa amani na usalama katika nchi, hujengeka katika misingi ya haki na usawa, misingi ya kuaminiana. Misingi ya kuheshimu haki na uhuru wa raia kutoa mawazo yao. Ni lazima kuwapo misingi imara ya demokrasia. Wananchi ni vema wakawaamini viongozi wao, na viongozi pia ni vizuri wakawaamini wananchi wao. Na ili viongozi waaminike, ni lazima wawe wakweli na wawazi na Wawe waadilifu”.
Haya ni mambo ya msingi kabisa kuyatafakari. Hii ni nchi yetu. Ni nchi yetu sote. Ni lazima tuaminiane. Tulio wengi tuna mapenzi ya dhati na nchi yetu. Kama taifa, miaka 51 ya Uhuru inatutaka tutafakari kwa kina juu ya mustakabali wa taifa letu”.

Mgomo wa madaktari na Muhimbili kukosa nyuzi za kushonea kwenye upasuaji! 225
 “Maana, haitakuwa busara kuliacha suala hili likapita kama yanavyopita mengine ilihali limegharimu maisha ya Watanzania. Na kubwa zaidi kwa sasa, ni kwa pande zote katika mgogoro huu kutambua; kuwa kwa sasa mvutano unaoendelea hautatoa mshindi, ni kwa vile, katika kilichotokea na kinachoendelea kufanyika sasa, sote, kama Taifa, tumeshindwa”.
“Huu ni wakati wa kutanguliza busara na hekima. Tufanye yote, lakini, njia mujarab ya kutanzua mgogoro huu uliopo sasa ni mazungumzo katika mazingira ya kuheshimiana, basi. Kinachoonekana sasa ni kwa baadhi ya viongozi kuwa mbali na umma. Viongozi kuwa mbali na hali halisi.  Baadhi ya kauli wanazotoa zinadhihirisha umbali huo kati yao na wanaowaongoza”.   
Tanzania ina vyote kasoro Watanzania Toleo la 218
“Nimepata kuandika huko nyuma (Juni 16, 2004) kuwa Tanzania ina vyote, kasoro Watanzania. Niliandika; kuwa Tanzania ni nchi nzuri sana. Ni nchi ya kujivunia. Kwamba Tanzania ni nchi kubwa sana kwa eneo. Ni nchi yenye rasilimali nyingi; ardhi yenye rutuba, mito, maziwa, milima, mabonde, bahari na vivutio vingi vya asili. Hata hivyo, Tanzania ni moja ya nchi masikini sana duniani. Kwa nini? Ndiyo, kikubwa kinachokosekana Tanzania ni Watanzania. Tanzania tunayoijenga sasa ni mkusanyiko tu wa watu wa makundi mbalimbali wenye kwenda kwa staili ya 'kila mtu na lwake'. Idadi ya Watanzania wenye uzalendo na mapenzi kwa nchi yao inazidi kupungua. Ubinafsi umekithiri, na ubinafsi mbaya zaidi ni ule wenye kufanywa na viongozi.”

" Bila Utawala Bora, bila kuwa na demokrasia, bila kuheshimu Haki za Kibinadamu,  mafanikio ya kiuchumi hayatawezekana."
“Hakika hakuna uchumi unaokua bila uwepo wa utulivu wa kisiasa. Kina Jaji Warioba wahakikishe wanaleta Katiba itakayohakikisha, mbali ya mambo ya mengine, inatupa  Tume Huru Ya  Uchaguzi”

CCM Kama Barcelona! ( Makala, Raia Mwema)


“CCM nayo inaamini, siku zote, kuwa kuna njia moja tu ya kuendesha siasa katika nchi hii, na njia hiyo ni ya CCM”!
Hakuna busara nyingine yeyote kwa sasa bali ni kwa CCM kuruhusu na kuendesha kwa salama mchakato wa mabadiliko makubwa yanayotakiwa na umma. Mabadiliko hayaepukiki. Ni hali ya dunia kwa sasa. Ni kama wimbi la maji ya bahari. Limeshajikusanya. Kwa CCM chaguo ni moja tu, kuenenda na wimbi hilo la mabadiliko au kukubali kufunikwa nalo.

Hilo la mwisho laweza kuharakisha kifo cha CCM. Ni jambo baya, maana, hata kama Watanzania watachagua upinzani ifikapo 2015, nchi yetu inahitaji chama imara cha upinzani, na CCM inaweza kuvaa viatu hivyo”. 
“Nchi yetu inapita sasa katika kipindi kigumu tangu tupate uhuru wetu. Ni kipindi kinachowataka viongozi, na hususan viongozi wa kisiasa, kutanguliza hekima na busara badala ya jazba, chuki na visasi. Hayo matatu ya mwisho ni mambo maovu yenye kuambukiza kwa haraka”.
“Kamwe tusiruhusu jazba, chuki na visasi vitawale siasa zetu. Hii ni  nchi yetu. Ni nchi yetu sote. Hakuna mtu, kikundi  au chama cha siasa chenye haki zaidi ya kuongoza nchi hii kuliko wengine wote”.
Mwandishi Ni Mjumbe, Hauawi- Makala Ya Maggid Mjengwa Raia Mwema September 7 2012
“Hii ni nchi yetu. Tutafanya makosa makubwa kuwaachia viongozi wa kisiasa pekee, jukumu la kulinda maslahi ya nchi yetu.  Tunapita sasa katika kipindi kigumu tangu tupate Uhuru.

Dunia imebadilika, na nchi yetu inapitia kwenye kipindi cha mabadiliko. Hakuna  mtu au chama cha siasa kinachoweza kuyazuia mabadiliko  haya. Kufanya hivyo ni kutuletea machafuko na kuvunja amani yetu. Tuna jukumu la kufanya tunayoweza, na kwa kutanguliza busara, kuipitisha salama nchi yetu katika kipindi hiki cha mabadiliko. Maana, tukiingia kwenye machafuko, basi, hakutakuwa na mshindi, maana, sote tutashindwa”.


Dhana ya uandishi wa habari:

Mwandishi Maggid Mjengwa ameendelea kusimamia ukweli kuwa vyombo vyetu vya habari vimekuwa vya kishabiki bila utumiaji wa taaluma ya kiuandishi, na tabia ya vyombo vya habari hususan magazeti kuibuka na vichwa vya habari vinavyoashiria moja kwa moja uchochezi. Maggid alitoa mfano kwamba “inaweza kutokea mtu mmoja ama mwislam au mkristo amefanya jambo la kukashifu dini nyingine. Sasa badala ya kuandika fulani kafanya hiki na kile, magazeti yanaibuka na vichwa vya habari tena kwenye kurasa za mbele vyenye mwelekeo wa kujumuisha kundi zima la dini fulani. Utasikia "Waislam wafanya fujo", au "Wakristo wakasirishwa". Aina hii ya uandishi italipeleka Taifa pabaya;


ukombozi wa waandishi

“Huko nyuma nimepata kuanzisha mjadala wa umuhimu wa kuwepo kwa ruzuku kwa vyombo vya habari ili navyo viweze kupata nguvu ya kuendesha shughuli zao ikiwamo hata uwezo wa kuwasafirisha wanahabari wao kwenye matukio badala ya gharama hizo za usafiri kutegemea ‘ bahasha’ za wanasiasa na wamiliki wa makampuni ya biashara, ambao , masharti yasiyoandikwa ya wao kutoa bahasha zao, ni namna wanahabari hao watakavyoripoti habari za kuwapamba na itakazowafurahisha watoa bahasha”.

“Naam, wanahabari unganeni. Huu si wakati wa kulilia huruma za watawala ikiwamo wanasiasa. Huu ni wakati wa kupambana kudai ruzuku ya Serikali kwa vyombo vya habari. Ni ruzuku, pamoja na mauzo ( kama ni magazeti) na matangazo ndivyo vitakavyo wafanya muwe huru. Vinginevyo, mtaendelea kuachana na jukumu la kuutumikia umma wa Tanzania na badala yake mtabaki kuwatumikia wanasiasa, wafanyabiashara na makampuni makubwa”.

Hatari ya siasa kuchanganyika na dini Raia Mwema 260
Watanzania tuliwashuhudia baadhi ya viongozi wa kidini; Uislamu na Ukristo, wakitumia nyumba za ibada, si kwa kazi ya kiroho, kazi ya kuhubiri yaliyo mema kwa mwanadamu, bali walifanya kazi ya siasa. Kazi ya kuhutubia mambo ya siasa na kutoa maelekezo ya kisiasa ya moja kwa moja.

Hayo yamefanyika misikitini na makanisani. Ni hatari! Jambo hili linaiweka rehani amani ya nchi yetu. Linahatarisha umoja wetu wa Kitaifa. Maana, makanisani na misikitini wanakusanyika Watanzania wa itikadi tofauti za kisiasa, na wengine ni watoto, hawajawa tayari kupokea hotuba za kisiasa, bali watoto wako tayari kupokea mahubiri na mafundisho ya kiroho.

Naam, ni ukweli sasa, kuwa dini imejichanganya na siasa. Na huu si mseto mwema kwa nchi yetu.

Udhaifu wa JK - Tafsiri ya Maggid Mjengwa



“Kuna hoja mezani juu ya udhaifu wa JK, imetokea Bungeni.  Yumkini, kama mwanadamu, JK ana mapungufu na udhaifu wake, nani asiye na mapungufu na udhaifu? Lakini, tukimzungumzia JK kama taasisi ya ’ Urais’, namwona Rais anayejipambanua na waliomtangulia. Ni  kwa kujitahidi kufanya yale yalo nafuu na yenye manufaa kwa nchi yetu  kwenye mfumo dhaifu uliopo.   
 
Wanadamu tunapaswa kuhukumu dhamira ya mtu na si matokeo. Bado namwona JK kama kiongozi mwenye dhamira njema kwa nchi yetu. Nauona ujasiri ndani ya JK. Ni ujasiri wa kufanya yale ambayo, hata ndani ya chama chake hayakupata fanyika”

“Maana, katika jamii, mabadiliko yanapaswa yaendane pia na fikra mpya . Na jamii huingiwa na mashaka na kukosa imani pale fikra mpya zinapotekelezwa na watu wale wale ambao hawataki kabisa kuwaruhusu wengine  kushiriki uongozi wa nchi. Watu ambao bado miongoni mwao wanaamini kuwa tofauti za kifikra ni jambo baya. Kwamba upinzani ni uadui, ni uhaini. Kwamba wapinzani ni wa kuwakatakata na kuwatupa.  Sasa, katika hali ya sasa utawachinja wangapi ukawamaliza? Ni fikra za kiwendawazimu”.

 KATIBA NA UKOMO WA MALI 
“Kiongozi anayefahamu jinsi watu mitaani na vijijini wanavyoathirika na vitendo vya ufisadi hatopata kigugumizi kukemea na kulaani ufisadi kila anapopata fursa ya kufanya hivyo”.
“Tuna baadhi ya viongozi wenye utajiri wa ajabu kushinda hata hao wafadhili wanaotupa misaada. Yote hii inatokana na ubinafsi na uchoyo wa viongozi hawa. Wako tayari nchi inunue vifaa vibovu vya mamilioni ya dola za Marekani ili mradi wao wamehakikishiwa 10% yao. Katiba iweke wazi, kuwa kutakuwapo na ukomo wa kiwango cha fedha ambacho kiongozi wa kuchaguliwa au mtumishi wa umma anaweza kutoa kama zawadi kwa jamii.  Kinyume chake iwe ni kosa la jinai. Naam, Katiba mpya itusaidie kuwafanya viongozi wetu wafukuzie zaidi maendeleo ya wananchi kuliko mikate yao. Inawezekana”

kwa niaba ya Blogs za ukadirifu na mungupamojanasi tunakutakia kila la kheri katika mwaka 2013; uwe ni mwaka mwingine kwako ambao utaendeleza utashi wako na uwezo wako wa uandishi kwa faida ya Jamii ya Tanzania; KEEP IT UP;