Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya mrisho Kikwete akisoma
karatasi ya kupigia kura kabla ya kupia kura kumchagua Mbunge wa Jimbo
la Chalinze kwenye kituo cha kupigia kura cha Zahanati Msoga.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa
kwenye chumba cha kupigia kura wakati wa kupiga kura za kumchagua Mbunge
mpya wa Jimbo la Chalinze.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipiga kura yake ya kumchagua Mbunge mpya wa Jimbo la Chalinze.
Mama Salma Kikwete akiweka kura yake kwenye sanduku la kupigia kura kwenye kituo cha Zahanati Msoga.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze
kupitia Chama Cha AFP Ndugu Ramadhani Mgaya akizungumza na waandishi wa
habarai nje ya kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 1na kusema kuwa
Chama chake kitakubali matokea yeyote na pia kama watashindwa
watajipanga kwa ajili ya uchaguzi wa 2015.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze
Ndugu Mathayo Torongey akizungumza na baadhi ya mawakala alipotembelea
kituo cha Ofisi Mtendaji Kata namba 1, Bwilingu.
Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze
Ndugu Ridhiwani Kikwete akihakiki taarifa zake kabla ya kupiga kura
kwenye kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata namba 3 Bwilingu, Chalinze.
Aziza mtoto wa mgombea wa Ubunge Jimbo
la Chalinze kupitia CCM Ndugu Ridhiwani Kikwete akimsaidia Baba yake
kuweka kura kwenye sanduku la kura ,Ridhiwani alipigia kura yake kwenye
kata ya Bwilingu.
Mkurugenzi wa Uchaguzi Jimbo la
Chalinze Ndugu Samuel Salianga akizungumza na waandishi wa habari nje ya
kituo cha Ofisi ya Mtendaji Kata Bwilingu na kutoa tathmini ya jinsi
zoezi linavyoendelea na kufafanua mambo mbali mbali yanayohusu uhalali
wa wagombea kupiga kura popote ndani ya jimbo la uchaguzi.
wananchi wa jimbo la Chalinze
wamemaliza kupiga kura hivi punde na tayari baadhi ya vituo
matokeo yameanza kujulikana huku katika matokeo hayo ambayo si
rasmi mgombea wa CCM Ridhiwani Jakaya Kikwete anaendelea kuongoza
huku vyama vingine vikimfuata kwa mbali zaidi .
Hata hivyo zoezi hilo limefanyika
katika hali ya amani na utulivu na hadi sasa wananchi wameendelea
kusubiri matokeo hayo kwa hamu kubwa na baadhi ya vituo ambavyo
matokeo yameanza kujulikana wafuasi wa CCM wameanza kushangilia .
Mbali ya wafuasi wa CCM kuonyesha
kuanza kushangilia bado wafuasi wa vyama vikuu kama Chadema na
CUF wameendelea kujipa matumaini makubwa ya kushida katika
uchaguzi huo na kuwa mwisho wa zoezi la kuhesabu kura ndipo watakapo
jua mbichi na mbivu katika mchakato huo
Tayari Mgombea wa Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha AFP Bw Ramadhani Mgaya ametangaza msimamo wa chama chake baada ya matokeo hayo kutangazwa kwa kudai kuwa atakuwa tayari kukubali matokeo hata kama atashindwa katika uchaguzi huo .
Mgaya ambae amekuwa mwanasiasa wa
kwanza wa vyama vya upinzani kuueleza umma kuwa yupo tayari kwa
matokeo hayo na kutangaza kujipanga kwa mwakani 2015 .
Wakati mgombea huyo wa AFP akieleza
hayo kwa upande wa mgombea wa CCM Ridhiwan Kikwete yeye leo
amefanya kituko cha karne baada ya kujipigia kura katika zoezi
hilo na kisha karatasi hiyo ya kupigia kura kumpa mtoto wake
mwenye miaka chini ya minne kuitumbukiza katika kisanduku cha
kuhifadhia kura
uchaguzi huo unafanyika kufuatia
kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia CCM Marehemu Said
Bwanamdogo aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwaka huu .
Chanzo:Fransis G
No comments:
Post a Comment