Sehemu ya barabara iliyoomole katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele wa kwanza kulia)
akiongozana na Viongozi wengine wakati walipotembelea kukagua sehemu ya
barabara iliyobomoka katika barabara ya Dar – Bagamoyo. Wengine kutoka
kushoto ni; (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam) Suleiman
Kova, (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) Mhe. Said Mick saddik na (Mbunge
Mteule wa Chalinze) Mhe. Ridhiwan Kikwete.
Mawasiliano ya barabara
kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo yamejifunga kutokana na barabara hiyo
kubomolewa na maji katika Daraja la Mpiji mpakani mwa mikoa wa Dar es
Salaam na Pwani.
Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alifanikiwa kufika katika eneo
hilo mara tu baada ya kupokea taarifa za kukatika kwa barabara hiyo.
Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe
pamoja na watendaji wengine kutoka TANROADS, Waziri Magufuli amewaagiza
watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafanyakazi mchana na usiku ili
barabara hiyo muhimu na yeye kupitisha magari mengi ifunguliwe mapema
iwezekanavyo.
Zaidi
ya maelekezo hayo, Mhe. Magufuli pia ameagiza kuahirishwa hadi
itakapopangwa baadaye kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS
ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kuanzia siku ya Jumanne ya tarehe
15 Aprili 2014 huko mkoani Tanga. Hatua hiyo imechukuliwa ili watendaji
hao wabaki katika vituo vyao vya kazi hadi hali ya mvua zinazoendelea
kutulia na taarifa nyingine kutolewa.
Akizungumzia
hali katika eneo hilo la Mpiji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj
Mussa Iyombe kwa upande mwingine alibainisha kuwa kilichozolewa na maji
ni sehemu ya barabara na siyo daraja lenyewe la Mpiji.
Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini
zimesababisha madhara kadhaa kwa upande wa miundombinu ya barabara.
Waziri Magufuli ameendelea kutahadharisha kuhusu shughuli za uchimbaji
wa mchanga zinazofanywa karibu au chini ya madaraja, kwamba kwa maeneo
mengi ndicho chanzo cha
mito kuhama kutoka katika njia yake ya asili na kubomoa barabara. “Kama
manavyoona daraja lenyewe ni zima na linauwezo mkubwa wa kupitisha maji
lakini mto umehama kutokana na uharibifu wa mazingira” alisistiza Mhe.
Magufuli.
Daraja
la Mpiji lilifunguliwa rasmi mwezi Julai 2005 na Mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa.
TANROADS kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za SKOL na Estim Construction Company Limited zote za Dar es Salaam tayari wameanza kazi za kurekebisha sehemu hiyo.(MARTIN NTEMO) (FS)
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment