- TIMIZA WAJIBU WAKO KWA JAMII YA TANZANIA KWA MAISHA YAO BORA na KWA VIZAZI VIJAVYO- falsafa ya kaisari;
Dhana
ya uongozi wa namna yeyote ile unafaa uanzie nyumbani kwa kila mtu
uongozi ni uwezo wa kuweza kuyakabili kwanza yako mwenyewe na kufanya maamuzi
sahihi bila kushawishiwa na mtu mwingine yeyote yule.
kwa
kufanya hivyo utakuwa umefanikiwa kuyatawala maisha yako kulingana utaratibu
ambao wewe mwenyewe umejiwekea kuanzia ndani ya familia yako; ukifanikiwa
hili unakuwa umefaulu katika mtihani huu wa kwanza wa uongozi ndipo jamii
inapoanza kukuona kuwa hata ukipata nafasi ya kuwaongoza wao pia utaweza kufanya
maamuzi sahihi.
Kwa
maneno mengine ni uwezo au njia ya kuweza kuwashawishi watu ili waweze kufanya
kitu au kufikia lengo fulani la kikundi kwa ridhaa yao wenyewe. ili uongozi uwe
bora ni lazima kuwe na kiongozi anayeongoza kundi fulani la watu au jamii
husika.
Katika kila jamii kuna umuhimu wa kuwa na kiongozi
kunatokana na ukweli kwamba watu wanapaswa kuwa na namna ya kuunganisha nguvu
zao ili kufikia malengo yao. Katika kila jamii, ni lazima kuwepo na
mikakati ya kuunganisha nguvu, vipaji, uwezo na stadi mbalimbali za wana
jamii.
Wajibu wa msingi wa kiongozi yoyote ni kusaidia
kuunganisha uwezo wa watu, kuratibu, kusimamia shughuli za watu, na kila
inapobidi aonyeshe njia itakayosaidia kufikia lengo. Hii ndio dhana ya Bunge
letu la Katiba ambalo limejengwa na watu wenye sifa na uzoefu tofauti tofauti
ili watuletee katiba iliyo bora ambayo itaweza kudumu kwa vizazi;
Kwa dhana ya Plato uongozi ni dhana au taaluma
inayompa muhusika madaraka na uwezo wa kuwawezesha wale wanaoongozwa kuunganisha
nguvu, stadi na vipaji vyao na kuvitumia ili kufikia malengo yao. Kuongoza ni
kujua lengo la wale wanaoongozwa na njia ya kufikia lengo lao.
Uongozi bora una mchango mkubwa sana katika uimara
wa jamii. Lakini tufahamu kuwa Ubora wa kiongozi unachangiwa na vitu vingi
lakini tusisahau kuwa vile vile uongozi au kiongozi bora hutoka kwa Mungu.
hivyo ndugu zetu wajumbe wa Bunge maalum la Katiba mjue kuwa mna dhamana nzito
kwani mkiwatendea watanzania ndivyo sivyo adhabu yenu itatoka pande mbili kwa
Mungu na kwa jamii iliyowachagua.
Leo hii wajumbe wa Bunge maalum la katiba ninyi ni
viongozi muhimu sana ambao mtaingia katika vitabu vya kumbukumbu ya Taifa hili
kuhusu katiba bora au mbaya kwa Taifa letu.
swali la kuwauliza wajumbe wa bunge hili je
wanajitahidi kumpa Kaisari yaliyo ya Kaisari au kuwatumikia wananchi
waliowaweka katika nafasi hizo ambazo wanajivunia leo?
Je wajumbe
hawa wa bunge maalum kama viongozi muhimu wa Taifa hili leo hii wanafahamu ukubwa na umuhimu wa maamuzi yao
kwa jamii ya Tanzania?
Je Wajumbe
wetu wa Bunge Maalum wanamalengo ya kufikia hatua ya juu kabisa ya ubora wa
kutupatia Katiba Bora.? Inatakiwa wakumbuke kuwa Ni wajibu wa kiongozi kuwaongoza wana taasisi ili wafikie malengo yao.
Kwa hiyo, kiongozi ni lazima aweze kubuni mikakati na mbinu zitakazoiwezesha
taasisi anayoingoza kufikia malengo yake.
Je viongozi wetu wa bunge maalum wametawaliwa na
maadili gani katika utendaji wa kazi yao hii Muhimu? Ili wakuliane katika hoja
ni lazima wazingatia maadili ya msingi ya kufanikisha muafaka wa kitaifa kwa
kujiepusha na unafiki kuficha hisia zao na kuwa kweli waaminifu katika hoja za
msingi.
Je wajumbe wetu wa Bunge la katiba wamekuwa mifano
miongoni mwao? Njia pekee ya kuonyesha ufano bora ni uwezo wa kuvumiliana katika
hoja hata kama hoja hiyo huitaki tafuta jibu lililo bora, na sio kukataa hoja
kwa kuzomea au kwa matusi huu sio msingi mzuri kwa kufikisha hoja au kufifisha
hoja;
kwa upande mwingine wajumbe wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika
kutimiza wajibu badala ya kujali maslahi yao binafsi yatokanayo na itikadi au
faida ambayo wanafikiria wao tu watanufaika nayo;
- Je wajumbe wa bunge maalum wanajifahamu mwenyewe au wanaburuzwa buruzwa tu kufuatia itikadi wananzofuata?
- wanafahamu wananchi wanatamani nini au katiba iwe vipi?
- wanajua namna katiba hii itaweza kustawisha maisha ya wananchi wao na kuendelea kudumisha amani iliyopo katika pande zote mbili za jamuhuri ya Muungano?
Hebu
tujikumbushe Busara za Baba wetu wa Taifa
Mwalimu Nyerere alipozungumzia dhana ya uongozi, Mwalimu Nyerere
alisema, “uongozi ni kuonyesha njia.” Kwa maana hiyo, viongozi shurti wafahamu
vema matokeo ya uongozi wao. Wasome imani za wanaowaongoza na nyakati zilizopo
ili kutambua matumaini ya umma kimaisha.
TATIZO
LA WAJUMBE WA BUNGE MAALUM LA KATIBA NI
NINI ?
- Wanaelekea zaidi kwenye propaganda za kisiasa zilizojaa kuchafuana huku wakiacha mijadala ya maana bila kuipa kipaumbele. Wamesahau kuwa la msingi hapa ni kuwa kiongozi yeyote anayekuwa tayari kuongoza na anapochaguliwa kuongoza popote, ajuwe anabeba jukumu la kubadilisha hali za watu kuwa nzuri. Atumie stadi za uongozi mwema kuonyesha njia.
- Inaelekea wajumbe wetu wa bunge bunge maalum wamejikita zaidi katika kufikiria zaidi maslahi binafsi. Wanaepuka kutumia stadi za uongozi kusimamia haki za waliowa wafikisha hapo hasa wanyonge. na. Wajikumbushe kuwa kupewa uongozi ni kuchukua ahadi ya kutenda kwa haki.
Mwalimu
Nyerere aliandika miongozo mizuri katika Azimio la Arusha miongoni mwao akisema kwamba ili tuendelee tunahitaji Siasa
Safi na Uongozi Bora. Alitambua mchango wa mambo hayo katika maendeleo ya
mwanadamu. Kupitia siasa safi kila kitu cha kunufaisha wananchi hupatikana.
Bali ni muhimu viongozi wanaotarajiwa kufanikisha ustawi wa wanadamu,
wapatikane kwa njia ya haki. Watokane na ridhaa ya watu wenyewe wanaotaka
kuongozwa.
Hitimisho
Bunge maalum la Katiba lisitawaliwe
na malumbano ya mara kwa mara na
matumizi ya lugha za kejeli na matusi; kwa kuendekeza tabia hiyo wananchi
wanawaona wajumbe hawa wa bunge maalum wako zaidi kim kimasilahi na kiitikadi
na kuto kubadilisha misamamo yao hata pale ukweli unapokuwa wazi.
Tunaendelea kuona kuwa wajumbe wengi
waliochangia hoja wanafikiri malumbano yasiyo na msingi kwa Taifa letu leo hii
na katika kipindi hiki muhimu sana. Itakuwa ni jambo nzuri kama wajumbe watajua
matumizi ya muda ili kuepusha mabaya ya rasilimali. Wanatakiwa kuweka mbele
uzalendo wa Taifa hili na sio maslahi binafsi au ya kiitikadi.
MWENYEZI
MUNGU IBARIKA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA UTUPATIE KATIBA ILIYO BORA
KABISA KWA VIZAZI VYETU VIJAVYO.
No comments:
Post a Comment