Mjumbe wa Bunge la Katiba, Tundu Lissu.PICHA|MAKTABA
Mjumbe wa
Bunge la Katiba, Tundu Lissu amesema Tanganyika ilikufa kwa amri
iliyotolewa na Mwalimu Julius Nyerere na siyo kwa makubaliano katika
hati ya Muungano.
Lissu
alitoa kauli hiyo jana alipopata fursa ya kukamilisha dakika 16 za
hotuba yake ya ufafanuzi wa maoni ya walio wachache iliyokuwa
imekatishwa baada ya matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni ya Taifa
(TBC1) kukatika Jumamosi iliyopita.(MM)
Huku
akinukuu maneno yaliyopo katika vitabu vilivyoandikwa na Profesa Issa
Shivji na Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa, Lissu alisema
Jamhuri ya Muungano ilizaliwa bila uhalali wa kisheria kwa kuwa
hayakuwapo makubaliano ya kila upande wa Muungano.
Alisema
Aprili 26, 1964 (Siku ya Muungano), Mwalimu Nyerere alitoa amri ya
masharti ya mpito ya mwaka 1964 ambayo pamoja na mambo mengine iliifuta
Tanganyika. Akichambua kitabu cha '50 Years of Independence: A Concise
Political History of Tanzania' (Miaka 50 ya Uhuru: Historia fupi ya
Tanzania), kilichoandikwa na Msekwa na kuchapishwa Januari mwaka huu,
Lissu alisema:
"Msekwa
anasema katika kitabu hicho kuwa amri hiyo ilichapishwa katika Gazeti la
Serikali la siku hiyo. Kwanza, iliwabadilisha waliokuwa watumishi wa
Serikali ya Jamhuri ya Tanganyika kuwa watumishi wa Serikali ya Jamhuri
ya Muungano."
Alisema
hata Mahakama Kuu ya Tanganyika iligeuzwa kuwa Mahakama Kuu ya Jamhuri
ya Muungano na nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Tanganyika iligeuzwa kuwa
nembo ya Taifa ya Jamhuri ya Muungano.
Alisema
tarehe hiyohiyo, Mwalimu Nyerere alitoa amri ya Katiba ya muda ya mwaka
1964 na ilitangaza kuwa Katiba ya Tanganyika ndiyo iwe Katiba ya muda ya
Jamhuri ya Muungano.
"Kifungu
cha nne cha amri hii ndicho kilichoipatia Serikali ya Muungano majukumu
kuhusu mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano yote na
vilevile kwa mambo yasiyokuwa ya Muungano kwa upande wa Tanganyika,"
alisema Lissu huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo.
Alisema
Juni 15, 1964, Mwalimu Nyerere alitoa amri nyingine iliyoitwa 'Amri ya
Masharti ya Mpito' ambayo ilieleza kwamba mahali popote ambako sheria
zilizokuwapo zimetaja jina la 'Tanganyika' basi jina hilo lifutwe na
badala yake jina la 'Jamhuri ya Muungano' liwekwe.
Huku
akimnukuu Msekwa, Lissu alisema kigogo huyo wa CCM katika kitabu chake
amesema, "Uhai wa Tanganyika ulitolewa kwa njia hiyo ya amri. Athari za
jumla za amri hizi ni kwamba eneo la kisiasa ambalo ndiyo ilikuwa
Tanganyika lilitolewa uhai wake moja kwa moja kwa amri. Hii ndiyo sababu
hata jina la eneo la kijiografia lililojulikana zamani kama Tanganyika
ilibidi libadilishwe na kuwa Tanzania Bara."
Hata
hivyo, alipoulizwa kuhusu kauli hiyo ya Lissu aliyoitoa jana, Msekwa
alisema: "Kitabu kipo na ukikisoma kwa umakini utagundua kuwa
alichokisema Lissu siyo ambacho kimeandikwa. Sasa umhoji kuhusu hayo
aliyoyasema, muulize ameyapata wapi?"Kuhusu Shivji
CHANZO:MWANANCHI
No comments:
Post a Comment