Amiri
Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Jakaya Mrisho
Kikwete akiingia kwenye uwanja wa Uhuru kuwaongoza watanzania katika
maadhinimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania yanayofanyika kila mwaka
Aprili 26 kusherehekea muungano wa Tanganyika na Zanzibar Aprili mwaka
1964 watanzania wengi wamejitokeza katika maadhimisho hayo wakiwemo
viongozi mbalimbali na marais wa nchi mbalimbali za Afrika na
wawakilishi wa nchi mbalimbali pia katika mataifa mbalimbali ya Ulaya,
Rais
Jakaya Kikwete akisalimiana na Rais Yoweri Mseveni wa Uganda katikati nI
King Mswati wa Swaziland na kushoto ni Rais Piere Nkurunzinza wa
Burundi.
Kikosi
cha Makomandoo kikionyesha ukakamavu na kuonyesha uwezo wake katika
mapambano ya Karatee na mbele ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Kikwete
Na Hudugu Ng'amilo.
Sherehe
za kuhadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyozaa
nchi ya Tanzania zimefanyika leo mjini Dar es Salaam na kupambwa kwa
maonyesho mbali mbali ya kijeshi pamoja na halaiki zilizoandaliwa na
watoto.
Marais wanne wa nchi za Afrika Afrika Mashariki akiwemo Yoweri Museveni wa Uganda, Uhuru Kenyatta wa Kenya na Pierre Nkurunzinza wa Burundi ni miongoni mwa marais waliohudhuria sherehe hizo.
Wengine ni Rais Joyce Banda wa Malawi, Mfalme Mswati III wa Swaziland, mfalme Letsie III wa Lesoto Makamu wa Rais wa Nigeria Mohammed Sambo, Makamu wa Rais wa Zambia Guy Scott, Waziri Mkuu wa Rwanda Piere Habumurenyi, Waziri Mkuu wa Misri Ibrahim Mahlab na Rais Mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki.

Katika maadhimisho yao pia kulikuwa na maonyesho ya silaha mbali mbali za kivita zikiwemo ndege za kivita pamoja na za kiraia.
Hata
hivyo kilichovutia ni kikosi cha makomandoo wa jeshi la Tanzania ambao
walionyesha umahiri wao kupambana na adui bila kutumia silaha na
kuvunja vitu vigumu kwa kutumia kichwa na mikono.
Onyesho
jingine lililotia fora zaidi ni askari wa miamvuli ambao waliruka
kutoka kwenye ndege umbali wa futi elfu arobaini kutoka usawa wa bahari
kwa kutumia miavuli na kutua katikati ya uwanja wa sherehe.
source: mjengwa blog
No comments:
Post a Comment