Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha
Movement for Democratic Change MDC kimesema kimemsimamisha kiongozi
wake Morgan Tsvangirai kwa kukiuka kanuni za kidemokrasia.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti kufuatia mkutano wa chama hicho uliofanyika katika mji Mkuu Harare.
Tangu mwaka 2009 hadi 2013 Bwana
Tsvangirai alitumikia taifa la Zimbabwe katika nafasi ya Waziri Mkuu
katika serikali ya umoja wa kitaifa iliyoundwa kwa pamoja na Rais wa
sasa Robert Mugabe.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa ilifikia
kikomo mwezi julai mwaka 2013 baada ya Rais Mugabe kushinda kwa wingi wa
kura katika uchaguzi wa rais na Tsvangirai kususia uchaguzi kwa madai
ya udanganyifu. (J M)
Kushindwa kwake kulipunguza nguvu yake kama kiongozi ambaye alikuwa mshindani mkuu wa Rais Mugabe.
Waangalizi wanasema ndani ya MDC kumekuwa na mgogoro wa kiuongozi kwa miezi kadhaa.
Viongozi wengine wa ngazi za juu
wameripotiwa kusimamishwa katika mkutano huo uliofanyika siku ya
jumamosi na wanachama wengine wa chama hicho watachukua nafasi zao.
source: mjengwa
No comments:
Post a Comment