WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, April 27, 2014

Mkumbo: Vyama vyakosa mwelekeo kwa kutaka kuuvunja Muungano

Dk. Kitila Mkumbo
Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitila Mkumbo, amesema baadhi ya vyama vya upinzani vimekosa mwelekeo kutokana na kubeba ajenda inayoelekea kuvunja Muungano.
Akizungumza katika kongamano la Muungano lilofanyika chuoni hapo jana, Dk. Mkumbo alisema katika mwelekeo uliopo sasa haionyeshi utashi wa vyama hivyo kutaka kuulinda na kujenga Muungano imara, badala yake kuna vita vya kugombea madaraka nje ya Muungano.

Alisema kihistoria hakuna chama kinachoweza kujiweka kando ya Chama cha mapinduzi (CCM) ambapo katika muundo huo wamebeba ajenda ya siri ya kuona Mungano huo unavunjika ili wapate nafasi ya kushika uongozi katika nchi za Zanzibar na Tanganyika zitakazoundwa.

Alisema endapo watafanikiwa jambo hilo, Zanzibar kama nchi haitakuwa kwenye usalama na itasababisha Tanganyika kuwa shakani.

Alisema kosa lilofanyika ni kuweka suala la Muungano kuwa la kisera ndani ya vyama vya siasa, kitu kinaleta mvutano kati ya CCM wanaotaka serikali mbili na wapinzani wanaotaka serikali tatu.

"Tukiamua kama Muungano kuwa sera ya kisiasa tutakosea sana, mambo yote yanayogusa uhai wa nchi lazima yasiingiliwe na chama chochote," alisema Mkumbo.

Alishauri Rasimu ya Katiba mpya itamke wazi kujenga Muungano imara na sio kujenga nchi legelege.

Kongamano hilo liliandaliwa na Umoja wa Wasomi wa Chuo Kikuu hicho (UDASA) ambapo wasomi mbalimbali walijadili mustakabali wa Muungano na nini kifanyike kunusuru usivunjike.
 
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment