Mawimbi
makali na hali mbaya ya hewa baharini imetatiza juhudi za utafutaji na
uokoaji wa takriban watu mia tatu baada ya feri ya abiria kuzama katika
pwani ya Korea Kusini.
Watu
tisa wamethibitishwa kuaga dunia katika mkasa huo.Wengi wa abiria
kwenye meli hiyo walikuwa ni wanafunzi wa shule ya upili. Takriban watu
mia moja sabini wameokolewa. Kapteni wa jeshi la wanamaji la Marekani
Heidi C. Agle anashiriki katika operesheni ya uokoaji.
Ameiambia
BBC kuwa maandalizi yanafanywa kupeleka mtambo wa kuinua chombo hicho.
Wakati huohuo Rais Park Geun-hye, amewataka waokozi kuharakisha juhudi
zao za kuwatafuta manusura wa ajali hiyo.
Rais
Park -- ambaye amejionea meli hiyo mwenyewe, amesema kuwa kila dakika
ni muhimu katika kuhakikisha kuwa manusura wanapatikana.
Wapiga mbizi wamekuwa wakikabiliana na mawimbi makali kujaribu kukifikia chombo hicho kilichozama hapo jana.
Duru zinasema kuwa meli hiyo ilipoteza mwelekeo huku baadhi ya familia za waathriwa zikihoji mwenendo wa nahodha wa meli.
Hata hivyo nahodha huyo Lee Joon-seok aliomba msamaha na kusema ana majuto tele na kuwa hata hajui la kusema.
Dauru
zinseama kuwa miongoni mwa wliofariki ni wanafunzi wanne wenye umri wa
miaka 17 na mwaliamu wao mwenye umri wa miaka 25 pamoja na mfnyakazi
mmoja wa meli hiyo.
Wengine wlaiofariki bado hawajatajwa.Takwimu za hivi karibuni zinasema
kuwa wtu 475 walikuwa kwenye meli hiyo huku 287 wakiwa bado
hawajapatikana.
(CHANZO:BBC)
No comments:
Post a Comment